Pre GE2025 ‘Watanzania wanyonge’ wataka Paul Makonda agombee na kupewa Urais 2030

Pre GE2025 ‘Watanzania wanyonge’ wataka Paul Makonda agombee na kupewa Urais 2030

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mgao wa umeme unakwenda kuisha muda siyo mrefu na kubaki katika Historia ndugu yangu
Hata 2014 tuliambiwa mgao wa umeme utakuwa ni historia bomba la gas likifika Dar. Leo hii bomba la gas liko Dar, mgao ndio kama huu. Saa hii mnahamisha magoli! Hao wananchi wajinga wanaokubali chama Cha hivyo wako ccm tu.
 
Hata 2014 tuliambiwa mgao wa umeme utakuwa ni historia bomba la gas likifika Dar. Leo hii bomba la gas liko Dar, mgao ndio kama huu. Saa hii mnahamisha magoli! Hao wananchi wajinga wanaokubali chama Cha hivyo wako ccm tu.
Mama Samia akisema lazima atekeleze .kwa hiyo uwe na imani na mama yetu maana mambo yanakwenda kuwa safi kabisa muda siyo mrefu hadi utafurahi mwenyewe
 
Subiri uwone CCM wanavyo tuchezesha,na hili linawezekani likawa,dalili naziona,na Waziri wake.Mkuu atakua Biteko! Game ya CCM mbona iko wazi toka mwanzo kama unawafatilia!!
Panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu Mheshimiwa Paul Makonda ndiye Rais wetu 2030
 
Ndugu zangu Watanzania,

Uchapakazi wa Mheshimiwa Makonda, ujasiri wake, uzalendo wake, kujitoa kwake kutetea wanyonge, ushupavu na umadhubuti wake umewakosha na kukonga mioyo ya watanzania mitaani .ambao kwa sasa wana kiu ya kutaka kuona Paul Makonda anagombea urais na kuchaguliwa kwa kishindo kumpokea kijiti cha urais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan mwaka 2030.

Sauti zinaendelea kupazwa na wananchi kupitia mitandao ya kijamii,vyombo vya habari ,sauti za wananchi vilingeni na magengeni kuona kuwa siku moja Taifa hili linawekwa mikononi mwa Paul Makonda kama mkuu wa nchi, kiongozi wa serikali na Amiri jeshi mkuu wetu.kutokana na kuona namna anavyo chapa kazi bila kuchoka wala kupumzika wala kupata hata muda wa kula chakula cha mchana.muda wote yupo kazini kuwasikiliza wananchi kwa unyenyekevu na upole wa hali ya juu sana na kuchukua hatua papo kwa papo kwa kuwaita watu wa serikali kutoa majibu.

Nami naunga mkono kuwa ili kazi nzuri anazofanya Mheshimiwa Rais ziwe na muendelezo mzuri na kuendelea kwa kasi hii hii ,basi ni vema mwaka 2030 kumpa ushirikiano na kumuunga mkono Paul Makonda kushika nchi. Kwa hakika ndugu zangu nawaambieni ya kuwa kwa huyu Mwamba na jasiri kuwahi kutokea kusini mwa jangwa la sahara hakika nchi itakwenda mchaka mchaka katika maendeleo. Maendeleo yatakimbia kwa kasi na kukimbizwa kama mashindano ya mbio ndefu,.watumishi wa umma watachapa kazi kama nyuki,cheo kitakuwa dhamana na wananchi watabaki mabosi huku kila mtu akifurahia kuzaliwa Tanzania kama ilivyo sasa chini ya uongozi wa Rais Wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan.

Jiulize kama leo ni Mwenezi wa chama anaitetemesha na kuiteka nchi kiasi hiki kwa uchapa kazi wake .vipi Tukimpa Urais ili aendeleze pale alipoishia mama yetu mpendwa na mchapa kazi aliyetukuka? Kwa sababu ni lazima Anapotoka mchapa kazi kama mama Samia tukakikishe Nchi inakwenda katika mikono ya mchapa kazi na jasiri aina ya Makonda ili kazi zisisimake na kusua sua..

Tanzania inamhitaji sana Mheshimiwa Paul Makonda 2030 kuliko wakati mwingine wowote ule. Ndio maana jana nilisema alindwe kwa nguvu zote na gharama zozote zile ili aje kutupatia matokeo makubwa na Chanya Watanzania. Tuendelee kumuombea afya njema tu.

Ni lazima Makonda aandaliwe na kuwekwa tayari kwa nafasi za juu maana amejaliwa kipawa na Kalama ya uongozi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.nyote mnajionea namna kifua chake kilivyojaa ujasiri wa hali ya juu. Angalieni namna mchaka mchaka unavyopigwa huko kwenye ziara zake,angalieni namna watu nyuso zao zilivyo na tabasamu zimuonapo Paul Makonda ,angalieni namna watu wanalivyo na imani na matumaini na Mheshimiwa Makonda. Hapo hata mwaka mmoja tu hajamaliza ofisini.

vipi akipewa miaka kumi kama Rais wa nchi? Mnafikiri Tanzania hiii ya Rais wetu mpendwa Mama Samia itakuwa wapi? Ikumbukwe kwanza atakuta kazi kubwa imefanywa na Mheshimiwa Rais mama Samia,Ambapo atakuta umeme ni wa uhakika baada ya kuwa tayari bwawa la mwalimu Nyerere limeshakamilika.mnafikiri nani ataipita kiuchumi Tanzania Hii yenye rutuba nzuri ya kutosha na yenye kukubali kila aina ya mazao,yenye mlima mrefu barani Afrika,yenye mbuga za wanyama wa kila aina,yenye madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee,yenye madini ya kutosha karibu kila ukanda,yenye rasilimali watu ya kutosha,yenye mito,maziwa na bahari kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji na hata usafiri wa majini.

Yenye bandari kila kanda,yenye faida ya kuzungukwa na nchi zaidi ya saba ambazo zinategemea kupitishia mizigo yao katika bandari yetu,yenye misitu mingi kwaajili ya kutengenezea vitu vya aina mbalimbali badala ya kuagiza nje na hivyo kupunguza hazina ya pesa za kigeni.mnafikiri Tanzania ya kijana jasiri na imara mwamba Paul Makonda itakuwaje?

Mnafikiri Tanzania ya Makonda yenye utajiri wa makaa ya mawe ya kutosha ,vivutio vya utalii ,Kimondo cha pili kwa ukubwa Duniani baada ya kile cha Marekani, hamuoni Tanzania hiyo itatiririsha maziwa na asali katika mabomba yake kwa kila kaya? Kumbuka kwa sasa anacho fanya Rais Samia anaweka mazinginra mazuri ya kiuchumi ambapo ni wakati huo wa Urais wa Makonda miradi ya kimkakati itakuwa imeanza kutoa na kuleta faida.

Tujiandae kumpa nchi Mheshimiwa Paul Makonda mwaka huo wa 2030 ili Dunia ikae chini na kuishangaa Tanzania ikipaa kama ndege vita kiuchumi ,na kupokea wageni watakao kuwa wanapanga foleni na kupishana pale airport wakija kuitembelea Tanzania na kujifunza.

Pual Makonda chapa kazi sana kaka yangu.mama amekuamini na anaimani na matarajio makubwa sana kutoka kwako.chama tunakuamini sana na tuna matarajio makubwa sana kutoka kwako.chapa kazi na kila upitapo waambie wananchi na watanzania mambo makubwa aliyoyafanya mama yetu na Rais wetu Mama Samia.waeleze mabillioni aliyoyapeleka Katika maeneo yao.waambie kila mwezi mama yao na Rais wao anatoa zaidi ya Billion 33 ili watoto wao wasome bure.

Waambie Rais wao ametiririsha zaidi ya Trilioni sita katika Secta ya Afya pekee,waambie Rais wao ameongeza bajeti ya kilimo kufikia Billion mia tisa tisini ili wakulima wapate pembejeo kwa bei nzuri,waambie mama yao ameagiza zaidi ya tani laki moja za sukari kuja kuingiza sokoni,waambie mama yao anawapa mikopo wanafunzi wote wa elimu ya juu wenye sifa bila ubaguzi.waambie mama yao ametoa maelfu ya ajira kwa vijana na muda siyo mrefu anakwenda kumwaga mitaani zaidi ya elfu ishirini na tatu katika Secta ya Elimu na afya.

Waambie watumishi wa umma wachape kazi maana mama yao yupo pamoja nao na ataendelea kuwaongeza misharaha na kuwalipa madai yao ,lakini nao wahakikishe kuwa wanachapa kazi kwa bidii na uadilifu wa hali ya juu na wasifanye kazi kwa mazoea. Waambie mama amefanya mengi ambayo huwezi kumaliza kuyataja.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

Unyonge ni wewe mwenyewe
 
Hivi huwa hauna mambo ya kufanya. Hivi hauna familia, tusiwe tunakulaumu kumbe tunaongea na mtoto anaeishi kwa wazazi wake. Kwa mfano, Makonda mwenyewe akikuuliza km kakutuma utajibu nini. Au vipi hao watu wamekutuma? Ndo
Maana mnachukiwa wa watu wenye akili timamu, tabia za kutanguliza mbele njaa sio sawa kabisa, utawaambukiza ujinga watoto wako huko mbeleni. Badilika bwana.
Kwani wapi uliposikia Mheshimiwa Makonda anataka Urais? Tanzania ni kama Duka ambapo Watanzania ndio wamiliki ambao wanawajibu na haki ya kumtafuta muuza duka.kwa hiyo wao wanaona Mheshimiwa Makonda anaweza na ni mtu sahihi kusimamia Duka lao la kikaleta faida nakulinda mtaji wao. Kwa hiyo hiyo ni kiu ya watanzania kutaka kuona siku moja Taifa likiongozwa na Mheshimiwa Makonda kutokana na ujasiri alionao,uzalendo wake,kujituma kwake na uchapa kazi wake uliotukuka.
 
Wewe unaanzia wapi kusema ni maigizo wakati unaona namna anavyotatua kero za wananchi?
Narudia tena watu wajinga aina yako ndio wanaamini huo utoto wa huyo muhalifu ndio kutatua matatizo. Huko kote kumejaa viongozi wa ccm washindwe kutatua matatizo yao, Hadi apite huyo muhalifu kwa siku moja ndio atatue matatizo yao? Na unaamini hizo mbinu za kijinga bado zinawapumbaza watu?

Huu ujinga ndio ulichangia dhalimu magu kupora uchaguzi, maana aliamini amekubalika kwa mafuriko ya kutengenezwa na nguvu ya Dola, ila ilipofika wakati wa kampeni huku akiwa amehakikisha wapinzani hawapati airtime, aliona ukweli ambao hakuamini, akaishia kuugua Kila mara. Hii habari ya kutengeneza propaganda na kuiamini mwenyewe hufanywa na watu wajinga wa aina yenu.
 
Narudia tena watu wajinga aina yako ndio wanaamini huo utoto wa huyo muhalifu ndio kutatua matatizo. Huko kote kumejaa viongozi wa ccm washindwe kutatua matatizo yao, Hadi apite huyo muhalifu kwa siku moja ndio atatue matatizo yao? Na unaamini hizo mbinu za kijinga bado zinawapumbaza watu?

Huu ujinga ndio ulichangia dhalimu magu kupora uchaguzi, maana aliamini amekubalika kwa mafuriko ya kutengenezwa na nguvu ya Dola, ila ilipofika wakati wa kampeni huku akiwa amehakikisha wapinzani hawapati airtime, aliona ukweli ambao hakuamini, akaishia kuugua Kila mara. Hii habari ya kutengeneza propaganda na kuiamini mwenyewe hufanywa na watu wajinga wa aina yenu.
Acha kumchafua Mheshimiwa kwa vimaneno vya kuokoteza visivyo na ushahidi wa aina yoyote ile.kama una ushahidi wa hayo uzungumzayo nenda mahakamani ukafungue mashitaka na utoe ushahidi wako wa kutisha ili aje kujibu hoja zako uchwara.
 
Mama Samia akisema lazima atekeleze .kwa hiyo uwe na imani na mama yetu maana mambo yanakwenda kuwa safi kabisa muda siyo mrefu hadi utafurahi mwenyewe
Tena huyo ndio bure kabisa. Muulize kwanini asitumie umeme wa gas ambao chama chake kilisema bomba la gas likifika tu hapa Dar mgao utakuwa ni historia? Hapo ndio utajua uko kwenye chama Cha wajinga wenye uongo wa kitoto.
 
Back
Top Bottom