Pre GE2025 ‘Watanzania wanyonge’ wataka Paul Makonda agombee na kupewa Urais 2030

Pre GE2025 ‘Watanzania wanyonge’ wataka Paul Makonda agombee na kupewa Urais 2030

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Halafu mtu kama huyu unakuta anampiga vijembe Mwijaku na Baba Levo na wakati kiuhalisia wote hawana tofauti na inawezekana hata hao jamaa wamemuacha jamaa mbali sana. Kama umeamua kuwa chawa kuwa wa faida mtatumika vibaya mpaka mchoke
Hapana ndugu yangu mimi wala sifanyi kazi ya uchawa wala kutumika.mimi naeleza ukweli tu na kuwasilisha sauti ya wanyonge kutoka huku mitaani
 
Acha kuongea vitu usivyo na ushahidi navyo wewe
Nikuulize tu Luca
Ili upate maoni ya watu juu ya jambo fulani lazima utumie njia za kitaalamu kukusanya maoni na mitazamo ili kupata takwimu sahihi zitazoakisi uhalisia na kutoa ushahidi (empirical evidence) nikisema wewe ni mjinga uliyebobea unaweza kutupa tu hata sample ya takwimu ulizokusanya kwa kupitia sample ya mikoa ambayo bashite amepita na hata katika mitandao ya kijamii kutuamonisha kuwa una uhakika na unachokiqndika?

Kwamba sasa tuna kura ya maoni ya uraisi na makonda qnaongoza vesa/vis nani?
Mikoa iliyohusishwa na matokeo ya kura hiyo kwa kulinganisha na idadi ya watanzania kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi?
Unajua hata yeye akisoma anaona aibu?

Remember he has sanctions na 2030 atakuja mgombea ambae wewe na mumeo hamtaamini,
 
manyumbu yakiwa twisted kidogo tu yote yanaelekea ukouko,

yanapotoshwa na kupotoshwa kabsaa kirahisi sana,

Hana ushahidi na hawezi hata kujieleza huyo...
Ndio maana Mbowe aliyadanganya kuwa mwaka 2015 ni lazima CHADEMA ichukue nchi na ikishindwa basi yeye atajiuzulu .lakini cha ajabu mpaka leo ni mwenyekiti na hayajahoji kwanini hatumii ahadi yake ya kujiuzulu .badala yake mbowe kwa kibuli anayatishia na kuyaambia kuwa sumu haionjwi kwa ulimi.
 
Akipewa nchi tutegemee zaidi kunyimwa misaada toka Kwa mashoga
 
Nenda mahakamani utoe ushahidi wako kuwa ulinyang'anywa mali zako na siyo kuleta uongo wako hapa
watu wengine waajabu sana, sasa malalamiko unapewa wewe kweli humu JF?🤣

Kwa mfano sasa hilo jamaa, yaani limenyang'anywa mali zake halafu limekaa kimya, si zuzu hilo 🤣
 
Ndugu zangu Watanzania,

Uchapakazi wa Mheshimiwa Makonda, ujasiri wake, uzalendo wake, kujitoa kwake kutetea wanyonge, ushupavu na umadhubuti wake umewakosha na kukonga mioyo ya watanzania mitaani .ambao kwa sasa wana kiu ya kutaka kuona Paul Makonda anagombea urais na kuchaguliwa kwa kishindo kumpokea kijiti cha urais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan mwaka 2030.

Sauti zinaendelea kupazwa na wananchi kupitia mitandao ya kijamii,vyombo vya habari ,sauti za wananchi vilingeni na magengeni kuona kuwa siku moja Taifa hili linawekwa mikononi mwa Paul Makonda kama mkuu wa nchi, kiongozi wa serikali na Amiri jeshi mkuu wetu.kutokana na kuona namna anavyo chapa kazi bila kuchoka wala kupumzika wala kupata hata muda wa kula chakula cha mchana.muda wote yupo kazini kuwasikiliza wananchi kwa unyenyekevu na upole wa hali ya juu sana na kuchukua hatua papo kwa papo kwa kuwaita watu wa serikali kutoa majibu.

Nami naunga mkono kuwa ili kazi nzuri anazofanya Mheshimiwa Rais ziwe na muendelezo mzuri na kuendelea kwa kasi hii hii ,basi ni vema mwaka 2030 kumpa ushirikiano na kumuunga mkono Paul Makonda kushika nchi. Kwa hakika ndugu zangu nawaambieni ya kuwa kwa huyu Mwamba na jasiri kuwahi kutokea kusini mwa jangwa la sahara hakika nchi itakwenda mchaka mchaka katika maendeleo. Maendeleo yatakimbia kwa kasi na kukimbizwa kama mashindano ya mbio ndefu,.watumishi wa umma watachapa kazi kama nyuki,cheo kitakuwa dhamana na wananchi watabaki mabosi huku kila mtu akifurahia kuzaliwa Tanzania kama ilivyo sasa chini ya uongozi wa Rais Wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan.

Jiulize kama leo ni Mwenezi wa chama anaitetemesha na kuiteka nchi kiasi hiki kwa uchapa kazi wake .vipi Tukimpa Urais ili aendeleze pale alipoishia mama yetu mpendwa na mchapa kazi aliyetukuka? Kwa sababu ni lazima Anapotoka mchapa kazi kama mama Samia tukakikishe Nchi inakwenda katika mikono ya mchapa kazi na jasiri aina ya Makonda ili kazi zisisimake na kusua sua..

Tanzania inamhitaji sana Mheshimiwa Paul Makonda 2030 kuliko wakati mwingine wowote ule. Ndio maana jana nilisema alindwe kwa nguvu zote na gharama zozote zile ili aje kutupatia matokeo makubwa na Chanya Watanzania. Tuendelee kumuombea afya njema tu.

Ni lazima Makonda aandaliwe na kuwekwa tayari kwa nafasi za juu maana amejaliwa kipawa na Kalama ya uongozi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.nyote mnajionea namna kifua chake kilivyojaa ujasiri wa hali ya juu. Angalieni namna mchaka mchaka unavyopigwa huko kwenye ziara zake,angalieni namna watu nyuso zao zilivyo na tabasamu zimuonapo Paul Makonda ,angalieni namna watu wanalivyo na imani na matumaini na Mheshimiwa Makonda. Hapo hata mwaka mmoja tu hajamaliza ofisini.

vipi akipewa miaka kumi kama Rais wa nchi? Mnafikiri Tanzania hiii ya Rais wetu mpendwa Mama Samia itakuwa wapi? Ikumbukwe kwanza atakuta kazi kubwa imefanywa na Mheshimiwa Rais mama Samia,Ambapo atakuta umeme ni wa uhakika baada ya kuwa tayari bwawa la mwalimu Nyerere limeshakamilika.mnafikiri nani ataipita kiuchumi Tanzania Hii yenye rutuba nzuri ya kutosha na yenye kukubali kila aina ya mazao,yenye mlima mrefu barani Afrika,yenye mbuga za wanyama wa kila aina,yenye madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee,yenye madini ya kutosha karibu kila ukanda,yenye rasilimali watu ya kutosha,yenye mito,maziwa na bahari kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji na hata usafiri wa majini.

Yenye bandari kila kanda,yenye faida ya kuzungukwa na nchi zaidi ya saba ambazo zinategemea kupitishia mizigo yao katika bandari yetu,yenye misitu mingi kwaajili ya kutengenezea vitu vya aina mbalimbali badala ya kuagiza nje na hivyo kupunguza hazina ya pesa za kigeni.mnafikiri Tanzania ya kijana jasiri na imara mwamba Paul Makonda itakuwaje?

Mnafikiri Tanzania ya Makonda yenye utajiri wa makaa ya mawe ya kutosha ,vivutio vya utalii ,Kimondo cha pili kwa ukubwa Duniani baada ya kile cha Marekani, hamuoni Tanzania hiyo itatiririsha maziwa na asali katika mabomba yake kwa kila kaya? Kumbuka kwa sasa anacho fanya Rais Samia anaweka mazinginra mazuri ya kiuchumi ambapo ni wakati huo wa Urais wa Makonda miradi ya kimkakati itakuwa imeanza kutoa na kuleta faida.

Tujiandae kumpa nchi Mheshimiwa Paul Makonda mwaka huo wa 2030 ili Dunia ikae chini na kuishangaa Tanzania ikipaa kama ndege vita kiuchumi ,na kupokea wageni watakao kuwa wanapanga foleni na kupishana pale airport wakija kuitembelea Tanzania na kujifunza.

Pual Makonda chapa kazi sana kaka yangu.mama amekuamini na anaimani na matarajio makubwa sana kutoka kwako.chama tunakuamini sana na tuna matarajio makubwa sana kutoka kwako.chapa kazi na kila upitapo waambie wananchi na watanzania mambo makubwa aliyoyafanya mama yetu na Rais wetu Mama Samia.waeleze mabillioni aliyoyapeleka Katika maeneo yao.waambie kila mwezi mama yao na Rais wao anatoa zaidi ya Billion 33 ili watoto wao wasome bure.

Waambie Rais wao ametiririsha zaidi ya Trilioni sita katika Secta ya Afya pekee,waambie Rais wao ameongeza bajeti ya kilimo kufikia Billion mia tisa tisini ili wakulima wapate pembejeo kwa bei nzuri,waambie mama yao ameagiza zaidi ya tani laki moja za sukari kuja kuingiza sokoni,waambie mama yao anawapa mikopo wanafunzi wote wa elimu ya juu wenye sifa bila ubaguzi.waambie mama yao ametoa maelfu ya ajira kwa vijana na muda siyo mrefu anakwenda kumwaga mitaani zaidi ya elfu ishirini na tatu katika Secta ya Elimu na afya.

Waambie watumishi wa umma wachape kazi maana mama yao yupo pamoja nao na ataendelea kuwaongeza misharaha na kuwalipa madai yao ,lakini nao wahakikishe kuwa wanachapa kazi kwa bidii na uadilifu wa hali ya juu na wasifanye kazi kwa mazoea. Waambie mama amefanya mengi ambayo huwezi kumaliza kuyataja.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.


Sio mfuasi wa Samia tena? Humbwa kabisa
 
Nikuulize tu Luca
Ili upate maoni ya watu juu ya jambo fulani lazima utumie njia za kitaalamu kukusanya maoni na mitazamo ili kupata takwimu sahihi zitazoakisi uhalisia na kutoa ushahidi (empirical evidence) nikisema wewe ni mjinga uliyebobea unaweza kutupa tu hata sample ya takwimu ulizokusanya kwa kupitia sample ya mikoa ambayo bashite amepita na hata katika mitandao ya kijamii kutuamonisha kuwa una uhakika na unachokiqndika?

Kwamba sasa tuna kura ya maoni ya uraisi na makonda qnaongoza vesa/vis nani?
Mikoa iliyohusishwa na matokeo ya kura hiyo kwa kulinganisha na idadi ya watanzania kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi?
Unajua hata yeye akisoma anaona aibu?

Remember he has sanctions na 2030 atakuja mgombea ambae wewe na mumeo hamtaamini,
Kwanza acha dharau lako wewe.unaanzaje kuniambia mimi mwanaume maneno ya kunidhalilisha? Kwani ndugu yangu mtanzania huwezi kuandika hoja ikasimama na kujieleza yenyewe bila maneno ya kudhalilishana? Unaanzia wapi kumwambia mwanaume kuwa yeye na mumewe? Unataka nilijibu nini wakati umeonyesha utoto na kukosa ukomavu katika kujadili hoja?
 
Sio mfuasi wa Samia tena? Humbwa kabisa
Mama Samia ndiye Rais wetu mpaka 2030 huo ndio msimamo wangu na wetu watanzania.baada ya hapo ndio Watanzania kwa mamilioni yao wanataka kijiti cha urais apewe Mheshimiwa Paul Makonda kijana mchapa kazi na jasiri kuwahi kutokea kusini mwa jangwa la sahara.
 
Kwanza acha dharau lako wewe.unaanzaje kuniambia mimi mwanaume maneno ya kunidhalilisha? Kwani ndugu yangu mtanzania huwezi kuandika hoja ikasimama na kujieleza yenyewe bila maneno ya kudhalilishana? Unaanzia wapi kumwambia mwanaume kuwa yeye na mumewe? Unataka nilijibu nini wakati umeonyesha utoto na kukosa ukomavu katika kujadili hoja?
Wewe ndiye unayejidhalilisha mwenyewe kiasi kwamba jamii inakutazama katika mrengo huo! Hali kadhalika nilitamani paragraph hii iwe mwishoni baada ya wewe kujibu maswali yangu ya msingi niliyouliza. Kuwa mke sio dhambi hata Elton John ni mke wa mtu! Inategemea na tibia unazozionesha kwa uma qmbazo haziakisi taaluma wala siasa! Niliwahi kuomba wasifu wako kielimu na mambo ya kijamii ni miezi sasa upo kimya
 
watu wengine waajabu sana, sasa malalamiko unapewa wewe kweli humu JF?🤣

Kwa mfano sasa hilo jamaa, yaani limenyang'anywa mali zake halafu limekaa kimya, si zuzu hilo 🤣
Inatakiwa nalo lipelekwe mahakamani na kupewa kifungo cha maisha kabisa maana halijitambui kabisa 😀😀😀
 
Mama Samia ndiye Rais wetu mpaka 2030 huo ndio msimamo wangu na wetu watanzania.baada ya hapo ndio Watanzania kwa mamilioni yao wanataka kijiti cha urais apewe Mheshimiwa Paul Makonda kijana mchapa kazi na jasiri kuwahi kutokea kusini mwa jangwa la sahara.
Kuna watu walisema Magufuli ni rais wa millele na Mungu amshukuru Maugufuli kuondoa corona mkakenua meno! ATAKE ASITAKE ATAGOMBEA
Nakukumbusha tu mfano Ally Kesi- Job Ndugai na Afande Shana!

Unaacha kumtanguliza Mungu unashupaza shingo. Unaweza kusema Magufuli yuko wapi sasa?
 
Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe kwa mikono yetu na juhudi zetu.
Are you sure? Mbona wewe ni mjinga hivi?

Viongozi wako kila siku wanasema mama anazunguka duniani kutafuta hela- huku extent ya embezzlement ikipaa kila siku na hakuna anayewajibishwa. Wewe ndio kila siku unasifia kwamba tanzania imepewa misaada tanzania imepewa mikopo- hujitambui
 
Back
Top Bottom