Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
- Thread starter
- #141
Hakika ni lazima tuhakikishe kuwa Mheshimiwa Makonda anaingia ikulu kuliongoza Taifa letuCHAGUA MAKONDA 2030
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakika ni lazima tuhakikishe kuwa Mheshimiwa Makonda anaingia ikulu kuliongoza Taifa letuCHAGUA MAKONDA 2030
Kwa hiyo wewe ndio CHAWA rasmi wa Paul Makonda a.k.a DAUDI ALBERT BASHITE?Ndugu zangu Watanzania,
Uchapakazi wa Mheshimiwa Makonda, ujasiri wake, uzalendo wake, kujitoa kwake kutetea wanyonge, ushupavu na umadhubuti wake umewakosha na kukonga mioyo ya watanzania mitaani .ambao kwa sasa wana kiu ya kutaka kuona Paul Makonda anagombea urais na kuchaguliwa kwa kishindo kumpokea kijiti cha urais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan mwaka 2030.
Sauti zinaendelea kupazwa na wananchi kupitia mitandao ya kijamii,vyombo vya habari ,sauti za wananchi vilingeni na magengeni kuona kuwa siku moja Taifa hili linawekwa mikononi mwa Paul Makonda kama mkuu wa nchi, kiongozi wa serikali na Amiri jeshi mkuu wetu.kutokana na kuona namna anavyo chapa kazi bila kuchoka wala kupumzika wala kupata hata muda wa kula chakula cha mchana.muda wote yupo kazini kuwasikiliza wananchi kwa unyenyekevu na upole wa hali ya juu sana na kuchukua hatua papo kwa papo kwa kuwaita watu wa serikali kutoa majibu.
Nami naunga mkono kuwa ili kazi nzuri anazofanya Mheshimiwa Rais ziwe na muendelezo mzuri na kuendelea kwa kasi hii hii ,basi ni vema mwaka 2030 kumpa ushirikiano na kumuunga mkono Paul Makonda kushika nchi. Kwa hakika ndugu zangu nawaambieni ya kuwa kwa huyu Mwamba na jasiri kuwahi kutokea kusini mwa jangwa la sahara hakika nchi itakwenda mchaka mchaka katika maendeleo. Maendeleo yatakimbia kwa kasi na kukimbizwa kama mashindano ya mbio ndefu,.watumishi wa umma watachapa kazi kama nyuki,cheo kitakuwa dhamana na wananchi watabaki mabosi huku kila mtu akifurahia kuzaliwa Tanzania kama ilivyo sasa chini ya uongozi wa Rais Wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan.
Jiulize kama leo ni Mwenezi wa chama anaitetemesha na kuiteka nchi kiasi hiki kwa uchapa kazi wake .vipi Tukimpa Urais ili aendeleze pale alipoishia mama yetu mpendwa na mchapa kazi aliyetukuka? Kwa sababu ni lazima Anapotoka mchapa kazi kama mama Samia tukakikishe Nchi inakwenda katika mikono ya mchapa kazi na jasiri aina ya Makonda ili kazi zisisimake na kusua sua..
Tanzania inamhitaji sana Mheshimiwa Paul Makonda 2030 kuliko wakati mwingine wowote ule. Ndio maana jana nilisema alindwe kwa nguvu zote na gharama zozote zile ili aje kutupatia matokeo makubwa na Chanya Watanzania. Tuendelee kumuombea afya njema tu.
Ni lazima Makonda aandaliwe na kuwekwa tayari kwa nafasi za juu maana amejaliwa kipawa na Kalama ya uongozi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.nyote mnajionea namna kifua chake kilivyojaa ujasiri wa hali ya juu. Angalieni namna mchaka mchaka unavyopigwa huko kwenye ziara zake,angalieni namna watu nyuso zao zilivyo na tabasamu zimuonapo Paul Makonda ,angalieni namna watu wanalivyo na imani na matumaini na Mheshimiwa Makonda. Hapo hata mwaka mmoja tu hajamaliza ofisini.
vipi akipewa miaka kumi kama Rais wa nchi? Mnafikiri Tanzania hiii ya Rais wetu mpendwa Mama Samia itakuwa wapi? Ikumbukwe kwanza atakuta kazi kubwa imefanywa na Mheshimiwa Rais mama Samia,Ambapo atakuta umeme ni wa uhakika baada ya kuwa tayari bwawa la mwalimu Nyerere limeshakamilika.mnafikiri nani ataipita kiuchumi Tanzania Hii yenye rutuba nzuri ya kutosha na yenye kukubali kila aina ya mazao,yenye mlima mrefu barani Afrika,yenye mbuga za wanyama wa kila aina,yenye madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee,yenye madini ya kutosha karibu kila ukanda,yenye rasilimali watu ya kutosha,yenye mito,maziwa na bahari kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji na hata usafiri wa majini.
Yenye bandari kila kanda,yenye faida ya kuzungukwa na nchi zaidi ya saba ambazo zinategemea kupitishia mizigo yao katika bandari yetu,yenye misitu mingi kwaajili ya kutengenezea vitu vya aina mbalimbali badala ya kuagiza nje na hivyo kupunguza hazina ya pesa za kigeni.mnafikiri Tanzania ya kijana jasiri na imara mwamba Paul Makonda itakuwaje?
Mnafikiri Tanzania ya Makonda yenye utajiri wa makaa ya mawe ya kutosha ,vivutio vya utalii ,Kimondo cha pili kwa ukubwa Duniani baada ya kile cha Marekani, hamuoni Tanzania hiyo itatiririsha maziwa na asali katika mabomba yake kwa kila kaya? Kumbuka kwa sasa anacho fanya Rais Samia anaweka mazinginra mazuri ya kiuchumi ambapo ni wakati huo wa Urais wa Makonda miradi ya kimkakati itakuwa imeanza kutoa na kuleta faida.
Tujiandae kumpa nchi Mheshimiwa Paul Makonda mwaka huo wa 2030 ili Dunia ikae chini na kuishangaa Tanzania ikipaa kama ndege vita kiuchumi ,na kupokea wageni watakao kuwa wanapanga foleni na kupishana pale airport wakija kuitembelea Tanzania na kujifunza.
Pual Makonda chapa kazi sana kaka yangu.mama amekuamini na anaimani na matarajio makubwa sana kutoka kwako.chama tunakuamini sana na tuna matarajio makubwa sana kutoka kwako.chapa kazi na kila upitapo waambie wananchi na watanzania mambo makubwa aliyoyafanya mama yetu na Rais wetu Mama Samia.waeleze mabillioni aliyoyapeleka Katika maeneo yao.waambie kila mwezi mama yao na Rais wao anatoa zaidi ya Billion 33 ili watoto wao wasome bure.
Waambie Rais wao ametiririsha zaidi ya Trilioni sita katika Secta ya Afya pekee,waambie Rais wao ameongeza bajeti ya kilimo kufikia Billion mia tisa tisini ili wakulima wapate pembejeo kwa bei nzuri,waambie mama yao ameagiza zaidi ya tani laki moja za sukari kuja kuingiza sokoni,waambie mama yao anawapa mikopo wanafunzi wote wa elimu ya juu wenye sifa bila ubaguzi.waambie mama yao ametoa maelfu ya ajira kwa vijana na muda siyo mrefu anakwenda kumwaga mitaani zaidi ya elfu ishirini na tatu katika Secta ya Elimu na afya.
Waambie watumishi wa umma wachape kazi maana mama yao yupo pamoja nao na ataendelea kuwaongeza misharaha na kuwalipa madai yao ,lakini nao wahakikishe kuwa wanachapa kazi kwa bidii na uadilifu wa hali ya juu na wasifanye kazi kwa mazoea. Waambie mama amefanya mengi ambayo huwezi kumaliza kuyataja.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.
Mimi nimesema hoja za ukweli kabisa tofauti na wewe ambaye unamuita mwanaume kuwa ni mwanamke.je unaona upo sawa ndugu yangu Dolphin T?Labda nikusaidie ametumia jukwaa huru la jamii Forums ambalo "we dare to talk" kesho kamwambie Rais analea wabadhirifu uone kama utakaa uraiani! Wewe ni mjinga na sijui kwanini huwa hufikiri! Moja wapo ya ahadi za mwanaccm ni kuwa "Binadamu wote ni sawa'" sasa unapoita kundi la watu fulani Nyumbu kisa hamfanani mtizamo na itikadi hufai kuwa hata mwanachama wa ccm. Kwa maana unapomfananisha binadamu mwenzio na mnyama ni rahisi kuutwaa uhai wake! Na tukisema ninyi ni miongoni mwa kikundi cha watu wachache ndani ya chama kisichothqmini uhai wa binadamu hili linajidhihirisha wazi.
Mama Samia ndiye Rais wetu mpaka 2030 huo ndio msimamo wangu na wetu watanzania.baada ya hapo ndio Watanzania kwa mamilioni yao wanataka kijiti cha urais apewe Mheshimiwa Paul Makonda kijana mchapa kazi na jasiri kuwahi kutokea kusini mwa jangwa la sahara.
Mimi nimeleta kile wanachokihitaji watanzania.mimi ni kama mjumbe tu wa watanzania. Mjumbe hauwawi.
Ni Rais wa watanzania mwaka 2030.tuombe uzima utayakumbuka maneno haya pale Mheshimiwa Makonda atakapokuwa anaapishwa.Rais wako
kumbe?Maamuzi mengi hufanywa na akina Mwijaku kama Hujui 😄
Maendeleo sio nadharia au vitu vya kufikirika- maendeleo ni Tangible issues na yanaonekana huhitaji kutumia nguvu kubwa kuyasemea! Baba akijenga nyumba nzuri hana haja ya kuitisha kikao cha watoto kuwaeleza kuwa yeye ndio amejenga! Kwa sababu wanaona juhudi zake- so we don't need kumsemea the so called mama- yule ni Rais wa nchi anayesimamia serikali na sio kwamba anafanya kwa hisani no! Because the government is having a contract with a public under her control! Muite Rais ili akikosea uweze kumwajibisha.Mheshimiwa Makonda atatufaa sana rafiki na ndugu yangu choice variable.suala la kudumu hapa Duniani linabaki mikononi mwa Mwenyezi Mungu mwenyewe.maana unaweza usiwe na msimamo wa kizalendo na bado ukafa mapema kabisa na kuwaacha wengine. Lakini ni bora ukafanya kazi kubwa na ya kizalendo na kuandikwa jina kwako kwa wino wa dhahabu katika mioyo ya watu na kukumbukwa vizazi na vizazi.
Naomba pia tuendelee kumsemea Rais wetu mama Samia kwa kazi kubwa anazofanya hapa nchini .bila kumsahau dada yetu wa Taifa Mheshimiwa Dr Tulia Acksoni Mwansasu kiboko ya yule mhuni Sugu aliyekuwa amelichelewesha jimbo kwa maendeleo.
Ila usijali choicevariable mimi na wewe tuendelee kukisemea chama chetu na kazi kubwa inayoendelea kufanywa na chama na serikali yetu .ambapo sasa amekuja Mwamba Mwenyewe Paul Makonda.
😛 😛 😛CDF yuko sahihi Hata huyu Lucas anatokea Ndola Zambia 😂
nchi ya machawa kupe na kunguni.Kwa uchawa wake usishangae akawa DC
Nimechekea chooni! Wewe ndio cc ya chama au?Ni Rais wa watanzania mwaka 2030.tuombe uzima utayakumbuka maneno haya pale Mheshimiwa Makonda atakapokuwa anaapishwa.
Ogopa nchi ikiwa na wajinga wengi wanaweza kuchagua raisnchi ya machawa kupe na kunguni.
Mkuu huyo na elimu yake ya MEMKWA hawezi kuelewa yeye akili yake inamtosha kuvukia barabara,kuvaa nguo na kwenda chooni tu si zaidi ya hapo.Nikuulize tu Luca
Ili upate maoni ya watu juu ya jambo fulani lazima utumie njia za kitaalamu kukusanya maoni na mitazamo ili kupata takwimu sahihi zitazoakisi uhalisia na kutoa ushahidi (empirical evidence) nikisema wewe ni mjinga uliyebobea unaweza kutupa tu hata sample ya takwimu ulizokusanya kwa kupitia sample ya mikoa ambayo bashite amepita na hata katika mitandao ya kijamii kutuamonisha kuwa una uhakika na unachokiqndika?
Kwamba sasa tuna kura ya maoni ya uraisi na makonda qnaongoza vesa/vis nani?
Mikoa iliyohusishwa na matokeo ya kura hiyo kwa kulinganisha na idadi ya watanzania kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi?
Unajua hata yeye akisoma anaona aibu?
Remember he has sanctions na 2030 atakuja mgombea ambae wewe na mumeo hamtaamini,
Uwongo ukisemwa sana mwishowe unakua ukweli! Respond to the facts! Mwalimu aliposema kuna wanasiasa wana tabia za kimalaya malaya hukumaanisha kuwa wanaisasa hao ni malaya wanaojiuza la haha. And so your writtings reflects a woman who tries to romanticise her husband why shouldn't I refer you to a woman basing on your writtings bwana Luca.Mimi nimesema hoja za ukweli kabisa tofauti na wewe ambaye unamuita mwanaume kuwa ni mwanamke.je unaona upo sawa ndugu yangu Dolphin T?
Kila mtanzania mwenye akili Timamu na asiye kipofu wa akili na macho anaona kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu,imara na madhubuti wa Rais Dr Mama Samia Suluhu Hasssan.ukienda kwenye Elimu unakuta kazi kubwa imefanywa mpaka sasa wanafunzi wote wanaokuwa wamefaulu kidato cha kwanza wanaripoti wote kwa wakati mmoja, kwa kuwa serikali imejenga vyumba vya madarasa ya kutosha,ukienda katika afya unaona namna serikali ilivyofanya mapinduzi makubwa katika sekta ya afya,vituo vya afya kila sehemu.ndio maana leo inafika hatua mpaka nchi inapeleka madaktari bingwa nchini zambia kutoa huduma na kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto chini ya umri wa miaka 15,leo huduma zilizokuwa zinapatikana katika hospitali ya ApolloMaendeleo sio nadharia au vitu vya kufikirika- maendeleo ni Tangible issues na yanaonekana huhitaji kutumia nguvu kubwa kuyasemea! Baba akijenga nyumba nzuri hana haja ya kuitisha kikao cha watoto kuwaeleza kuwa yeye ndio amejenga! Kwa sababu wanaona juhudi zake- so we don't need kumsemea the so called mama- yule ni Rais wa nchi anayesimamia serikali na sio kwamba anafanya kwa hisani no! Because the government is having a contract with a public under her control! Muite Rais ili akikosea uweze kumwajibisha.
Waziri mkuu wa uingereza Magreth Thatcher hakuwahi kuitwa Mother bali PM. Huu upumbavu wenu wa kuwafanya viongozi kuwa sehemu ya familia ndio unawapa ugumu kuwawajibisha pale wanpokosea.
Hahaha hapana sidhani hivyo! Naamini elimu anayo ila ameamua kuiweka pembeni na kutumia sehemu ya ujinga kwa maana ya kivuli badala ya mwanga! Leo happy qkiteuliwa utaona uzi- subiri apandishe uzi wa upend penezq. Ila ungemwambia awaandikie wakiwa nje ya chama utashangaa na watu wakushangae! Huyu ni...Mkuu huyo na elimu yake ya MEMKWA hawezi kuelewa yeye akili yake inamtosha kuvukia barabara,kuvaa nguo na kwenda chooni tu si zaidi ya hapo.
Mimi sina Elimu ya memkwa kama yako.mimi nipo vizuri kielimu , kifikra na kimaono.Mkuu huyo na elimu yake ya MEMKWA hawezi kuelewa yeye akili yake inamtosha kuvukia barabara,kuvaa nguo na kwenda chooni tu si zaidi ya hapo.
Kama unampenda sana mzalie watoto.Kila mtanzania mwenye akili Timamu na asiye kipofu wa akili na macho anaona kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu,imara na madhubuti wa Rais Dr Mama Samia Suluhu Hasssan.ukienda kwenye Elimu unakuta kazi kubwa imefanywa mpaka sasa wanafunzi wote wanaokuwa wamefaulu kidato cha kwanza wanaripoti wote kwa wakati mmoja, kwa kuwa serikali imejenga vyumba vya madarasa ya kutosha,ukienda katika afya unaona namna serikali ilivyofanya mapinduzi makubwa katika sekta ya afya,vituo vya afya kila sehemu.ndio maana leo inafika hatua mpaka nchi inapeleka madaktari bingwa nchini zambia kutoa huduma na kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto chini ya umri wa miaka 15,leo huduma zilizokuwa zinapatikana katika hospitali ya Apollo
kule india unaona zikipatika hapa hapa nchini.
Kila utakakokwenda na kila Secta unaona hatua kubwa na mafanikio makubwa yamepatikana .angaliia kwa sasa hata ile mikoa ambayo ilikuwa haijaunganishwa katika grid ya Taifa sasa zimeunganishwa na kupata mwanga wa umeme