Pre GE2025 ‘Watanzania wanyonge’ wataka Paul Makonda agombee na kupewa Urais 2030

Pre GE2025 ‘Watanzania wanyonge’ wataka Paul Makonda agombee na kupewa Urais 2030

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Leo umeanzisha nyuzi ngapi za kumsifia na kumtukuza mwanaume mwenzio? Unajidhalilisha bro, Bora ungekuwa unamsifu baba Yako ungepata baraka
Baba yangu hajapendekezwa na watanzania nafasi ya Urais 2030.aliyependekezwa nafasi ya Urais na watanzania ni Mheshimiwa Makonda.
 
Kila mtanzania mwenye akili Timamu na asiye kipofu wa akili na macho anaona kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu,imara na madhubuti wa Rais Dr Mama Samia Suluhu Hasssan.ukienda kwenye Elimu unakuta kazi kubwa imefanywa mpaka sasa wanafunzi wote wanaokuwa wamefaulu kidato cha kwanza wanaripoti wote kwa wakati mmoja, kwa kuwa serikali imejenga vyumba vya madarasa ya kutosha,ukienda katika afya unaona namna serikali ilivyofanya mapinduzi makubwa katika sekta ya afya,vituo vya afya kila sehemu.ndio maana leo inafika hatua mpaka nchi inapeleka madaktari bingwa nchini zambia kutoa huduma na kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto chini ya umri wa miaka 15,leo huduma zilizokuwa zinapatikana katika hospitali ya Apollo
kule india unaona zikipatika hapa hapa nchini.

Kila utakakokwenda na kila Secta unaona hatua kubwa na mafanikio makubwa yamepatikana .angaliia kwa sasa hata ile mikoa ambayo ilikuwa haijaunganishwa katika grid ya Taifa sasa zimeunganishwa na kupata mwanga wa umeme
Naanza kukwambia wewe ni mjinga.
Hakuna mwanafunzi anayefaulu kwenda kidato cha kwanza. Wote wanatakiwa kwenda kidato cha kwanza kwa sababu elimu ya kuanzia chekechekea mpaka kidato cha nne ni ya msingi na lazima (basic and compulsory) kwa mujibu wa sera ya elimu ya tanzania (TETP 2015) na kwa Takwa la UN kupitia UNESCO kwamba elimu ni moja wapo ya haki za binadamu na Tanzania mojawapo ya signatories wa mikataba hiyo ya utekelezaji. Ndio mana wakati wa magufuli mlitaka kumuua zito alipowashtaki UN Kuhusu kunyima haki ya wasichana walozaa kurudi shule.

Ni wajibu wa serikali za nchi signatories kuhakikisha kuwa wanaadhere to makubaliano ndio mana tukakopa hela za so called UViko kujenga maharasa shule za sekondari na msingi- mpango wa shule za kata ambao upo ndani ya (SEDEP) na upanuzi wa shule za msingi ((PEDEP) na huu ni mwendelezo tu wa kile alichoanza kufanya JK na ENLOWASA. AMKA DUDUMIZI WEWE
 
Baba yangu hajapendekezwa na watanzania nafasi ya Urais 2030.aliyependekezwa nafasi ya Urais na watanzania ni Mheshimiwa Makonda.
Nikisema wewe ni mjinga utakasirika- haya liambie jukwaa kupititia kikao kipi lini na wapi na nani alishiriki na kukusanya maoni?
 
Mimi sina Elimu ya memkwa kama yako.mimi nipo vizuri kielimu , kifikra na kimaono.
Ili kujua mtu yuko vizuri kifikra kielimu na kimaono basically wanaomsikiliza na kuona afanyayo ndio husema ila sio yeye kujisemea.

Wanasema kaa kimya ufiche ujinga wako au ongea tujue ujinga na upumbavu wako. Umeelewa? Hii ni elimu ndogo sana
 
Nikisema wewe ni mjinga utakasirika- haya liambie jukwaa kupititia kikao kipi lini na wapi na nani alishiriki na kukusanya maoni?
Kwa sasa Dunia ni kama kijiji tu.maendeleo ya teknolojia yamekua na kuongezeka sana.ndio maana saizi mtu husubiri kuangalia taarifa ya habari saa mbili usiku .maana kwa sasa watu wanazipata habari kwa uharaka sana kutoka eneo la tukio moja kwa moja.hii yote ni kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.
 
Nitasema kweli Daima fitina kwangu mwiko!

Naomba mwabia Dada Mwashambwa kuwa ccm imetunga sheria kuifanya TISS kuwa Jeshi kamili- Mwambie ccm imetunga sheria ya kinga ya kutoshtakiwa na viongozi wa umma wenye maamuzi yanayoliangamiza taifa kwa ubadhirifu- Mwambie serikali ya ccm imetunga sheria ngumu za habari kuunyima umma kureport mambo nyeti yanayofanywa na serikali ambayo hayana afya kwa nchi! Mambo ni mengi!
Lucas mwashambwa ni sehemu ya hayo madhila. Yeye anaamini hatujui mchezo anaoucheza kutuhadaa
 
Lucas mwashambwa ni sehemu ya hayo madhila. Yeye anaamini hatujui mchezo anaoucheza kutuhadaa
Anadhani hatujaelewa kauli ya Mwenyekiti akiongea na Makamanda wa Jeshi. Tena akitanguliza kuwa kuna uchaguzi- akaongezea kuwa ujao ndio zaidi sana wakae standby kama wanavyofanya kule visiwani?
Mtu huyo huyo:

Rais wa Nchi ya vyama vingi
Amiri Jeshi Mkuu
Mwenyekiti wa Chama
Mkuu wa utumishi wa umma
Mwajiri wa Mwenyekiti &Mkurugenzi wa uchaguzi
Mteuzi wa majaji wote
Mteuzi wa katibu wa Bunge
Mteuzi wa Jaji mkuu!
Mteuzi wa mwanasheria mkuu
Mwishoni ni mgombea wa URAIS kwenye uchaguzi wa vyama vingi
 
Kwa sasa Dunia ni kama kijiji tu.maendeleo ya teknolojia yamekua na kuongezeka sana.ndio maana saizi mtu husubiri kuangalia taarifa ya habari saa mbili usiku .maana kwa sasa watu wanazipata habari kwa uharaka sana kutoka eneo la tukio moja kwa moja.hii yote ni kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Mama Keagan popote ulipo njoo huku kuna mjane anamtega mumeo
 
Kwa sasa Dunia ni kama kijiji tu.maendeleo ya teknolojia yamekua na kuongezeka sana.ndio maana saizi mtu husubiri kuangalia taarifa ya habari saa mbili usiku .maana kwa sasa watu wanazipata habari kwa uharaka sana kutoka eneo la tukio moja kwa moja.hii yote ni kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Kama ni hivyo kuna haja gani ya kutumia gharama kubwa kumsemea mama! Haya tanzania ime_inovate nini katika sayansi hiyo ya tehama? Unasifia vya wenzio halafu unajipiga ngumi kifuani! Nataka statistical analysis bro baada ya kupata findings nitakubaliana na ww otherwise wewe unashindana ma mama Keagan
 
Anadhani hatujaelewa kauli ya Mwenyekiti akiongea na Makamanda wa Jeshi. Tena akitanguliza kuwa kuna uchaguzi- akaongezea kuwa ujao ndio zaidi sana wakae standby kama wanavyofanya kule visiwani?
Mtu huyo huyo:

Rais wa Nchi ya vyama vingi
Amiri Jeshi Mkuu
Mwenyekiti wa Chama
Mkuu wa utumishi wa umma
Mwajiri wa Mwenyekiti &Mkurugenzi wa uchaguzi
Mteuzi wa majaji wote
Mteuzi wa katibu wa Bunge
Mteuzi wa Jaji mkuu!
Mteuzi wa mwanasheria mkuu
Mwishoni ni mgombea wa URAIS kwenye uchaguzi wa vyama vingi
Undenied facts.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Uchapakazi wa Mheshimiwa Makonda, ujasiri wake, uzalendo wake, kujitoa kwake kutetea wanyonge, ushupavu na umadhubuti wake umewakosha na kukonga mioyo ya watanzania mitaani .ambao kwa sasa wana kiu ya kutaka kuona Paul Makonda anagombea urais na kuchaguliwa kwa kishindo kumpokea kijiti cha urais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan mwaka 2030.

Sauti zinaendelea kupazwa na wananchi kupitia mitandao ya kijamii,vyombo vya habari, sauti za wananchi vilingeni na magengeni kuona kuwa siku moja Taifa hili linawekwa mikononi mwa Paul Makonda kama mkuu wa nchi, kiongozi wa serikali na Amiri jeshi mkuu wetu. Kutokana na kuona namna anavyo chapa kazi bila kuchoka wala kupumzika wala kupata hata muda wa kula chakula cha mchana.muda wote yupo kazini kuwasikiliza wananchi kwa unyenyekevu na upole wa hali ya juu sana na kuchukua hatua papo kwa papo kwa kuwaita watu wa serikali kutoa majibu.

Nami naunga mkono kuwa ili kazi nzuri anazofanya Mheshimiwa Rais ziwe na muendelezo mzuri na kuendelea kwa kasi hii hii, basi ni vema mwaka 2030 kumpa ushirikiano na kumuunga mkono Paul Makonda kushika nchi. Kwa hakika ndugu zangu nawaambieni ya kuwa kwa huyu Mwamba na jasiri kuwahi kutokea kusini mwa jangwa la sahara hakika nchi itakwenda mchaka mchaka katika maendeleo. Maendeleo yatakimbia kwa kasi na kukimbizwa kama mashindano ya mbio ndefu, watumishi wa umma watachapa kazi kama nyuki,cheo kitakuwa dhamana na wananchi watabaki mabosi huku kila mtu akifurahia kuzaliwa Tanzania kama ilivyo sasa chini ya uongozi wa Rais Wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama Samia Suluhu Hasssan.

Jiulize kama leo ni Mwenezi wa chama anaitetemesha na kuiteka nchi kiasi hiki kwa uchapa kazi wake .vipi Tukimpa Urais ili aendeleze pale alipoishia mama yetu mpendwa na mchapa kazi aliyetukuka? Kwa sababu ni lazima Anapotoka mchapa kazi kama mama Samia tukakikishe Nchi inakwenda katika mikono ya mchapa kazi na jasiri aina ya Makonda ili kazi zisisimake na kusua sua..

Tanzania inamhitaji sana Mheshimiwa Paul Makonda 2030 kuliko wakati mwingine wowote ule. Ndio maana jana nilisema alindwe kwa nguvu zote na gharama zozote zile ili aje kutupatia matokeo makubwa na Chanya Watanzania. Tuendelee kumuombea afya njema tu.

Ni lazima Makonda aandaliwe na kuwekwa tayari kwa nafasi za juu maana amejaliwa kipawa na Kalama ya uongozi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.nyote mnajionea namna kifua chake kilivyojaa ujasiri wa hali ya juu. Angalieni namna mchaka mchaka unavyopigwa huko kwenye ziara zake,angalieni namna watu nyuso zao zilivyo na tabasamu zimuonapo Paul Makonda ,angalieni namna watu wanalivyo na imani na matumaini na Mheshimiwa Makonda. Hapo hata mwaka mmoja tu hajamaliza ofisini.

vipi akipewa miaka kumi kama Rais wa nchi? Mnafikiri Tanzania hiii ya Rais wetu mpendwa Mama Samia itakuwa wapi? Ikumbukwe kwanza atakuta kazi kubwa imefanywa na Mheshimiwa Rais mama Samia,Ambapo atakuta umeme ni wa uhakika baada ya kuwa tayari bwawa la mwalimu Nyerere limeshakamilika.mnafikiri nani ataipita kiuchumi Tanzania Hii yenye rutuba nzuri ya kutosha na yenye kukubali kila aina ya mazao,yenye mlima mrefu barani Afrika,yenye mbuga za wanyama wa kila aina,yenye madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee, yenye madini ya kutosha karibu kila ukanda, yenye rasilimali watu ya kutosha,yenye mito,maziwa na bahari kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji na hata usafiri wa majini.

Yenye bandari kila kanda,yenye faida ya kuzungukwa na nchi zaidi ya saba ambazo zinategemea kupitishia mizigo yao katika bandari yetu,yenye misitu mingi kwaajili ya kutengenezea vitu vya aina mbalimbali badala ya kuagiza nje na hivyo kupunguza hazina ya pesa za kigeni.mnafikiri Tanzania ya kijana jasiri na imara mwamba Paul Makonda itakuwaje?

Mnafikiri Tanzania ya Makonda yenye utajiri wa makaa ya mawe ya kutosha ,vivutio vya utalii ,Kimondo cha pili kwa ukubwa Duniani baada ya kile cha Marekani, hamuoni Tanzania hiyo itatiririsha maziwa na asali katika mabomba yake kwa kila kaya? Kumbuka kwa sasa anacho fanya Rais Samia anaweka mazinginra mazuri ya kiuchumi ambapo ni wakati huo wa Urais wa Makonda miradi ya kimkakati itakuwa imeanza kutoa na kuleta faida.

Tujiandae kumpa nchi Mheshimiwa Paul Makonda mwaka huo wa 2030 ili Dunia ikae chini na kuishangaa Tanzania ikipaa kama ndege vita kiuchumi, na kupokea wageni watakao kuwa wanapanga foleni na kupishana pale airport wakija kuitembelea Tanzania na kujifunza.

Paul Makonda chapa kazi sana kaka yangu.mama amekuamini na anaimani na matarajio makubwa sana kutoka kwako.chama tunakuamini sana na tuna matarajio makubwa sana kutoka kwako.chapa kazi na kila upitapo waambie wananchi na watanzania mambo makubwa aliyoyafanya mama yetu na Rais wetu Mama Samia.waeleze mabillioni aliyoyapeleka Katika maeneo yao.waambie kila mwezi mama yao na Rais wao anatoa zaidi ya Billion 33 ili watoto wao wasome bure.

Waambie Rais wao ametiririsha zaidi ya Trilioni sita katika Secta ya Afya pekee,waambie Rais wao ameongeza bajeti ya kilimo kufikia Billion mia tisa tisini ili wakulima wapate pembejeo kwa bei nzuri,waambie mama yao ameagiza zaidi ya tani laki moja za sukari kuja kuingiza sokoni, waambie mama yao anawapa mikopo wanafunzi wote wa elimu ya juu wenye sifa bila ubaguzi. Waambie mama yao ametoa maelfu ya ajira kwa vijana na muda siyo mrefu anakwenda kumwaga mitaani zaidi ya elfu ishirini na tatu katika Secta ya Elimu na afya.

Waambie watumishi wa umma wachape kazi maana mama yao yupo pamoja nao na ataendelea kuwaongeza misharaha na kuwalipa madai yao, lakini nao wahakikishe kuwa wanachapa kazi kwa bidii na uadilifu wa hali ya juu na wasifanye kazi kwa mazoea. Waambie mama amefanya mengi ambayo huwezi kumaliza kuyataja.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Unakaribia kuokota makopo hakika
 
Back
Top Bottom