Watanzania wasema Rais Samia anatosha na hakuna sababu ya kufanyika kwa uchaguzi wa Rais 2025

Unataka nipasue jipu.
Ajenda zenu mnazo dhania ni siri zinavuja kila Leo.
Na huo mwaka amini hakuna watakao Haribu Kula wala uchaguzi bila kusahau kile mmepanga "Waigize kususia Uchaguzi" ili mtoboe kifala fala
Yeyote atakaye ingia uwanjani kushindana na CCM uchaguzi ujao Ni lazima avune aibu ya Karne,maana kwa CCM Hii imara na madhubuti hakuna mwenye uwezo wa kushindana nayo Wala kupata kura mbele yake
 
mbili mbolea ilikua inauzwa 56000 bila ruzuku enzi za jpm sas 100000 na inaruzuki
 
tatu mradi wa umeme rufiji ulikua asilimia 56 wamevunja bodi tendaji wamemtoa kaleman mradi wanadai uko asilimia 37
 
nne ununuzi wa mabehewa ya mtumba na angali order ilikua inatoka south korea wasupply exburet train
 
mbili mbolea ilikua inauzwa 56000 bila ruzuku enzi za jpm sas 100000 na inaruzuki
Bei ya mbolea ilipanda katika soko la Dunia,Hata hivyo Rais Samia n serikali Yake alifanya juhudi na uamuzi wa kishujaa uliowashinda Marais wengi kwa kuamua kutoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika mbolea na hivyo kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu
 
tatu mradi wa umeme rufiji ulikua asilimia 56 wamevunja bodi tendaji wamemtoa kaleman mradi wanadai uko asilimia 37
Hali ya mradi inaendelea vizuri kabisa na utakamilika kwa wakati ili kuliangazia Taifa letu na kuchochea uchumi wetu
 
Hata mm natamani iwe hivyo, lakini katiba inasemaje?
 
Wewe utakuwa ndugu wa yule askari wa kwenye ile connection akifumuliwa marinda
 
Teuzi za mwaka huu zimeisha, ila ongeza bidii kuna siku watakupigia simu
 

Wacha uongo, sema wewe ndio unapenda iwe hivyo.
 
...............watanzania kwa wingi wao hawaoni sababu ya kupoteza mamilioni ya Fedha kwa ajili ya kuchapisha karatasi za nafasi ya Urais wakati......................
Bila katiba mpya 2025 hakuna hata haja ya uchaguzi, aendelee tu regardless ni kweli ama sio kweli.
 
Wahi mirembe tayari umeshawehuka
 
Hii Nchi inaongozwa kwa sheria na Taratibu za Kikatiba , 2025 mama yetu apumzike amelishalivusha Taifa hili kwenye kipindi kigumu cha kumpoteza kipenzi chetu Jemadari wa Vita Hayati DR. John pombe Magufuli ....Sasa tumahitaji kijana mmoja mwenye moyo wa kizalendo kama wa JPM arudishe heshima ya Taifa letu ...
 
Luca,ukishashiba makatapera unakuwa mjinga sana.Hapo unapiga mbwewe tu.
 
Bila ya kufanya utafiti shirikishi wa kina, tena kwa kutumia sampuli kubwa yenye kuwakilisha makundi yote muhimu ya Watanzania wote wapatao milioni 61 huwezi kukimbilia kutoa hoja ambayo umeileta hapa jukwaani.

Lucas kukimbilia kuleta mada nyingi kama hizi za kichawa hapa jukwaani, na pia kutokana na mapungufu makubwa ya kimantiki, kimaudhui na kimuktadha ndani yake, hii ndiyo sababu Ndg. Chongolo anawaasa vijana mliomaliza vyuo vikuu mjipange tena ili muende VETA kwa ajili mafunzo ya stadi za ufundi. Hii inaonyesha haridhisjwi kabisa na "analytical skills" za vijana kama wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…