Watanzania watia moto vifaranga wengine 5,000 kutoka Kenya

Tanzania kwa mara nyengine tena imechoma vifaranga 5,000 vya kuku vinavyodaiwa kuingizwa nchini humo kupitia mpaka wa Kaskazini wa Namanga kutoka Kenya.

Kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya, katibu katika wizara ya mifugo nchini Tanzania Maria Mashingo, amesema kuwa mfanyibiashara aliyeingiza vifaranga hao nchini Tanzania hakuwa na vibali vinavyohitajika .

Tanzania imesema kuwa hatua ya kuwachoma kuku hao inalenga kuzuia kuenea kwa homa ya ndege.

''Hakuna haja ya kuathiri sekta yote ya kuku kwa sababu ya vifaranga 5000'', Mashingo alinukuliwa na gazeti hilo akisema.

Takriban miezi mitatu iliopita, Tanzania ilichoma vifaranga 6,400 vya kuku wenye thamani ya shilingi 577,000 waliopatikana katika mpaka huohuo , hatua ilioshutumiwa na wanaharakti wa wanyama kutoka mataifa yote mawili.

Uamuzi huo pia ulisababisha vita vya kibiashara kati ya mataifa hayo jirani.

Kuku hao walichomwa na maafisa wa wizara ya mifugo na uvuvi wakishirikiana na maafisa wa usalama baada ya kukamatwa katika mpaka wa Namanga

Mkurugenzi wa shirika linalopigania haki za wanyama nchini Tanzania Thomas Kahema alisema kuwa kuna njia nyengine madhubuti za kukabiliana na tatizo kama hilo na ingekuwa bora kuwarudisha kuku hao nchini Kenya badala ya kuwachoma kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania likiongezea kuwa kumekuwa na hisia kali katika mitandao ya kijamii.

Mfanyiabiashara Mary Matia, 23, aliwaingiza kuku hao wenye thamani ya $5000 kutoka Kenya na aliangalia kwa uchungu mkubwa na kutoamini wakati vifaranga hao walipochomwa , alisema mwandishi wa BBC Balthazar Nduwayezu kutoka mji wa Namanga.

Tanzania ilipiga marufuku uingizaji wa kuku yapata muongo moja uliopita kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa homa ya ndege katika eneo la Afrika mshariki.

Chanzo BBC
 
Tena??
 
Tena mm laiti ningekuwa waziri wa mifugo, ningepiga marufuku ufugaji wa kuku wa kisasa nchi yetu ilivyokubwa hatuhitaji vyakula vya kubahatisha tena vyenye madhara kwa binadamu kama kuku wa kisasa.
 
Alafu tule nini?
 
Habari hii kamanikweli, inamana hao wafanyabiashara wanatujaribu amavipi.

Kwanini wanakiuka utaratibu unaohitajika, inamana hawajui au wanafanya makusudi ili kulaumuwatu tu.
 
Ni maswali ambayo najiuliza pia
 
Ile mutaa ya Kariobangi na Korokocho. Najua hiyooo? Basi kama nafika ulisia mimi nakuta pale. Half chicken with Ingiima only 3 bob
Hiyo mitaa hadi 46 south ni mwendo wa sima na githeri tu. Maharage na kachumbari pembeni na bei yake..hahaha...

Kwa karisi..。see u again!
 
Mtu akiona maneno yako atadhani we ndo mhuni uliyechoma moto hao vifaranga. Kumbe labda hata mende huezi ua!
Lengo ni kutaka kukuonyesha kwamba Tanzania inaweza kuifanya Kenya vyovyote vile na Kenya haiwezi kulipiza wala kufanya lolote dhidi ya Tanzania.
 
Magendo ndio uchome?! Bora wangezigawa mashuleni watoto wakafuga kwenye poultry zao na at the same time wanapata kitoweo
Naona we ndio unaamka, hebu kapate uji kwanza. Hivi wakigawa watakuwa wamezuia nini?
 
Ni ngumu kuzuia biashara ya magendo hasa kwa mfanyabiashara mzoefu wa magendo.

Hapo ujue vifaranga vinavuka kila siku maelfu kwa maelfu ila wanakamata hivyo kama ushahidi tu kuwa wanafanya kazi.

Ukitaka hiyo biashara ife waache uzalishaji Kenya.....
 
Back
Top Bottom