Watanzania watu wa ajabu, wanapenda maendeleo lakini hawataki kugharamia hayo maendeleo kwa kodi

Nchi hii ina vilaza wengi sana wenye uelewa finyu katika masuala basic kama hili la kodi.
Hawajui kabisa kanuni bora za kodi matokeo yake ni kujivisha uzalendo uchwara tu.
 
Mpaka wakati huu kila mwananchi analipa kodi. Hawa wote wanalipa kodi[emoji117]Wanaonua kalamu na daftari kwa watoto, wanaonunua nguo mpya, wanaonunua sukari/mafuta/, wasafiri wote wa gari za abiria, wanaonunua maji ya kunywa n.k
 
Mkuu toa jina lako na tin number yako pia na nida namba yako ili tuone wewe umeshalipa Bei gani ama ndio waliovimbewa
 
Tozo ya 18% kwa biashara yoyote utakayoilipia/lipwa.
Hiyo tozo ya 18% unayoikusanya kwa niaba ya serikali, unaiwakilisha Idara ya mpatao ndani ya mwezi mmoja.
Ni vyema kuanzia leo ufahamu hii 18% huwa inalipwa na mlaji/mteja/mnunuzi wa bidhaa au huduma.
 
Wa ajabu ñi wewe ambaye unataka watanzania walipe kodi ila kuna watu wanakula hela za umma kama za urithi wa familia zao. Kisha mkaguzi mkuu wa serikali anasema hela zimeliwa , vyombo ambavyo ninatakiwa kushughulikia ubadhirifu vinakaa kimya. Wakienda hospitali wanashindwa kutibiwa kisa wameshindwa kulipia gharama, harafu kuna watu wanaoitwa waheshimiwa wakiwasha magari ya umma hawayazimi mpaka watakarudi kulala. Mfumuko wa bei kila kukicha ila mshahara wake wa mwaka 47, unategemea huyu mtanzania atakuwa na morali wa kulipa kodi? Mkishiba dengu mnajiona mna akili na kuwakejeli watanzania.😤😤😤
 
Ni vyema kuanzia leo ufahamu hii 18% huwa inalipwa na mlaji/mteja/mnunuzi wa bidhaa au huduma.
Mkuu kama huna habari, kuna kodi zaidi ya 56 za TRA, na VAT ni kodi moja tu kati ya hizo, ambayo haiwezi kukidhi matakwa mapato ya kuendesha nchi.
 
Mkuu ukishindwa kujiendesha ndio unaona sasa "wahisani" wanahamia nyumbani kwao na kukuamrisha ufanye nini kimandeleo, kiufupi wanakutawala.
 
Mkuu toa jina lako na tin number yako pia na nida namba yako ili tuone wewe umeshalipa Bei gani ama ndio waliovimbewa
Kodi inatakiwa kulipwa na KILA MTU, uvimbiwe au usivimbiwe, uwe tajiri au masikini.
 
Umenena sawa. Lakini tatizo ni fikra au mindset ya uongozi wa nchi yenyewe ambayo ilikuwa imebadilika baada ya kiikubali sera ya uchumi wa soko yaani ushindani, kuwa ndiyo dira kuu ya kuongoza uzalishaji wa bidhaa na huduma katika nchi na siyo ukiritimba wa Serikali ambao hauna tija kwa sababu hauendani na hulka ya binadamu; pia uamuzi wa kurudisha serikali ifanye shughuli hizo hauendani na jinsi wenzetu wanaotuzidi kwenye maendeleo wanavyofanya. Ila sisi na wahanga wachache wenzetu tumeng'ang'ania kuingiza usultani katika kuendesha uchumi! Hata teuzi za wakuu wa shughuli za uchumi hazifikiwi kwa kuwashindanisha ili kupata wale wenye uwezo, tunawateua tunaowapenda ati ni zamu yao nao!
 
Wewe unaona double taxation,ni sawa tu kisa zinajenga madaraka? Huko ndo kujikomba!!!! Sasa hivi unaoneka utakuwa utamaduni wa mta nzania " KUJIKOMBA"
 
Kodi inatakiwa kulipwa na KILA MTU, uvimbiwe au usivimbiwe, uwe tajiri au masikini.
Mbunge halipi mkuu hata akiagiza gari sio Kama wewe mwenye njaa. Nimeongea kwa Nia nzuri tupatie details zako ili tucheki hapa tra umeshalipa ngapi ama ndio niamini kuwa talk is cheap.
Anyone can talk even dog but actions only real and courageous few can do it
 
Tatizo lako na wengi ni ufupi wa maono.
Bila watanzania wenyewe kujiongeza katika shughuli za uchumi na biashara tutendelea kuwa tegemezi.
 
Tatizo lako na wengi ni ufupi wa maono.
Bila watanzania wenyewe kujiongeza katika shughuli za uchumi na biashara tutendelea kuwa tegemezi.
Mie nimekuomba details hapa Niingize ili tuone Kama kweli unalipa kwani shida iko wapi. Naomba tuone urefu wako wa akili. Sawa mimi na watanzania wengi Ni ufupi mie Nimeshakubaliana Ila Sasa naomba tuone urefu wa akili yako ama na wewe unajiona Kama na ellite na huku haupo kwenye royal family
 
Ni kweli maendeleo hugharimiwa na tukiyataka lazima tuyalipie kwa njia ya kodi. Tatizo linakuja pale maskini anatakiwa agarimie zaidi kuliko tajiri. Kodi nyingi TZ zinalipwa na maskini. Serkali imetengenezaji njia ambazo masikini siku zote atabanwa na atalipa tu. Kuanzia vijijini kwenye magulio, masoko, minada ukiuza uji, mayai, kuku, mbuzi n.k. unapambana na kodi. Kana kuwa hiyo haitoshi ukiomba silingi 10 kwa mtoto au ndugu akakutumia kwa simu unapmbana na kodi. Kodi zimekuwa nyingi, kiasi serkali imeona izipe majina ya ufiho ili watu wasijuwe ni kodi. Sasa hivi kuna kodi, tozio, ushuru, makato, ankra, n.k, lakini zote ni kodi. Majina ni ya kufica ukweli kuwa hizo ni kodi. Kijeremani zinaitwa "direkte (Einkommen) und indirekte (andere) Steuern".
 
Mbona huna akili za kukutosha.
It is actually stupid ku personalize hili tatizo la kodi.
Pili nikuhakikishie kuwa naajiri watu kama wewe ngingi tu, na hapo unaweza kukadiria kodi yangu.
Nne refer kwa sheria za JF.
 
Ukiniajiri Kodi nalipa mie kutokana na salary nayopata kwako so usitufanye Kama hatujui Kodi inavyolipwa. Wewe utalipa Kodi kama mkurugenzi wa kampuni yako ya apple. Sawa? Kuna faida ya kampuni yako na iyo serikali inapochukua Kodi.


Mbona Kama unaleta vitisho kuwa unaajiri watu wengi Kama mie kwani umeona wewe ndio wa kwanza kuajiri ama mie siajiriwi.


Simpo ishu let's TIN tukuone kweli Kama unalipa Kodi.
kukadiria kodi yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…