Na ndio sababu tuna visingizio na lawama nyingi !!
Ukiangalia maisha yetu kwa karibu, utaona hii tabia ipo kwenye maeneo mengi.
Deadline ikikaribia ndio kazi inaanza.
Mtihani ukikaribia ndio kusoma kunaanza.
Mgonjwa akizidi ndio tunakimbilia hospitali.
Gari likiharibika kabisa ndio tunakumbuka service.
Ndoa ikianza kuyumba ndio tunaanza kutafuta namna ya kuirekebisha.
Kwa nini?
Sehemu ya jibu inaweza kuwa kwenye namna wengi wetu tulivyolelewa.
Tulikuzwa kwenye nidhamu ya kulazimishwa zaidi kuliko nidhamu ya kujiongoza.
Ukiamka kuchelewa - Kugombezwa, adhabu, viboko
Usipofanya homework, Kugombezwa, adhabu, viboko
Ukifanya kosa, Kugombezwa, adhabu, viboko
Usipofuata maagizo, Kugombezwa, adhabu, viboko
Mtoto anajifunza kufanya kitu kwa sababu anaogopa adhabu, si lazima kwa sababu ameelewa umuhimu wa kukifanya mapema.
Matokeo yake, tunakua na mindset ya: “Nifanye nini nisije nikapata shida?”
Badala ya“Nifanye nini sasa ili nisije nikapata shida baadaye?”
Hapo ndipo tofauti ya Reactive na Proactive inapoonekana.
Reactive mindset inasubiri pressure.
Proactive mindset inahitaji self-discipline.
Reactive anasubiri mwalimu aseme, “Kesho mtihani.”
Proactive anajua mtihani upo na anaanza maandalizi mapema.
Reactive anasubiri ndoa iwe kwenye hatari ndipo aanze kuwasiliana.
Proactive anaijenga ndoa kabla haijafika kwenye crisis.
Reactive anasubiri mwili umwambie “Boss, tumekwisha.” 😂
Proactive anaangalia afya kabla tatizo halijawa kubwa.
Na hii haimaanishi kila kitu tunachofanya kwa kuchelewa kimetokana na malezi. Maisha yana sababu nyingi. Lakini kuna jambo la kutafakari:
Je, tumewahi kufundishwa kweli kujiongoza, au tulifundishwa zaidi kuogopa matokeo ya kutokutii?
Kwa sababu ukimfundisha mtu nidhamu kwa hofu pekee, akiondolewa anayemwangalia anaweza kuacha nidhamu.
Lakini ukimfundisha mtu kujiongoza, hata hakuna anayemwangalia, bado anafanya kinachotakiwa.
Labda tunahitaji kuacha kulea kizazi kinachosubiri moto uwake ndipo kitafute maji.
Tujifunze kuona moshi mapema.
Hiyo ndiyo Proactive mindset.