Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Mateso niliyoyapitia kayumba sitaki mwanangu ayapitie kitaeleweka tu.
Mimi nimesoma kayumba, niko mtaani sasa hivi na teammates wangu wengi wamesoma private. Mazungumzo yao ni fulani alifungua kampuni ya logistics, huyu tangu aende Canada hajawahi rudi, huyu amekopa milioni 50 kashindwa marejesho, huyu duka lake liliungua sasa hivi tunamchangia aanze kidogo upya.

Class langu la STD 7 na lile la Form 4 mwenye degree ni mmoja tu, story zao ni huyu kamkimbia mke wake, huyu kaiba TV, huyu kapata kazi unesi Nachingwea. Alafu nina walevi wa visungura wengi.

Kayumba wenzangu wamezalisha wanawake vibaya mno uko mtaani. Hainikai akilini mwanangu nikimpata naye aende amebeba vidumu shule kama mimi.
 
Kuna tofauti kubwa ya tuition na shule. Shule mnatumia muda mwingi na maongezi yanakua marefu,tuition muda mchache,mtoto kachoka hivyo umakini unapungua.

Ila akirudi nyumbani anaongea Kiswahili.

Walimu wanao mfundisha , English Sio lugha Yao na wanawasiliana Kwa Kiswahili on daily basis.

It doesn't make any sense
Mamilioni ni mbwembwe tu za wazazi. Ndo maana unaona mtu anasomesha shule za mamilioni bado anamtafutia mwanae connection za kazi mfano mzuri mwigulu,mwanae yupo feza international ila bado anamhangaikia vinafasi uvccm ya watoto

Mtoa Mada anawazungumzia watanzania wenye kipato cha chini wanao jistress kulipa mamilioni kwenye Ems
 
Huu ndio uhalisia
 
Nyumbani mnakaa nae muda mchache hivyo haina madhara kwake kuongea kiswahili au kilugha. Mcheki mtoto wa mwijaku,home mzee wake full kiswahili ila binti anapiga ung'eng'e kumzidi biden

Sio mbaya wacha wateseke si wamependa wenyewe au ndo vile wameshaona mateso waliyoyapata kwa kusoma kayumba hivyo wanalipa kwa watoto wao kusoma ems
 
Mkuu mpeleke janja shule za maana acha janja janja mtani.
 
Umefanya vizuri sana.
 
Big up Sana mkuu.

You are the true son of your father
 
Hao wegi wanaotetea Kayumba wamesoma Kayumba zile angalau zenye Hali nzuri, Mimi nimesoma Kayumba secondary mpaka naingia kwenye paper la form two sikuwahi kumuona mwalimu chemistry wala biology halafu mtu Yuko serious mwanae anaempenda akasome shule hizo..

Hao walimu wenyewe wa kayumba watoto zao wanawakimbiza huku private..
Hakuna kiongozi mwanae anasoma huko serikalini
Ukiona mtoto anafaulu Kayumba ni mtoto mwenyewe tu ana akili za kuzaliwa.
Hawa watoto wengine akili zao mbili zinazohitaji ukaribu wa walimu wanaambulia 0.

Mtu anasema mtoto aende tuition kama siyo kuchosha watoto kashakaa shule masaa 8, kwanini aende tuition na ELIMU ya kayumba ni Bora kwanini akitoka shule afanye majukumu ya nyumbani mengine au apumzike baadae ajisomee Yale aliyofundishwa shule...
 
Siku zote tunawaambia mtafute pesa muache kujifariji ujinga!

Mngekuwa mna amani na maamuzi yenu msingekuwa mnashinda huku kutueleza mambo yenu.

Mlipowapeleka huko EM mbona hamkutuambia?
So wewe ni tajiri mkuu?

Matajiri wanaongeaga hivyo?


Kama na wewe ni tajiri Basi there is no hope to the future.

Mwenzako ka share story Yake Kwa sababu anataka kuwasaidia na watanzania wenzake wanao poteza pesa zao bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…