Watatezi wa makahaba, ndio mnataka Tanzania yetu iendelee kuwa hivi? Rais Samia mpandishe Bomboko cheo

Huyo mama yako unaetaka kumpandisha huyo mwendawizimu cheo Mbona analiuza taifa kuliko wanavyojiuza hao Malaya?
Hii bihashara inafanyika kwa sababu hawana kazi za kufanya.
 
Unajua kinachohojiwa au unakurupuka tu?
 
Ngoja wazee wa democray na agano jipya waje
Unaweza kabisa kabisa kupigana na ukahaba bila kuvunja haki za watu. Hivi inakujia akilini mtu kwenye kwenye nyumba ya kulala wageni, ukikurupusha watu chumba kwa chumba, huk umefuatiana na wahuni wanaojiita waandishi wa habari waki-record kila kitu? Kwa nini msako usifanyike kwa utaalam na bila uhuni?
 
Wewe ni mpumbavu,hakuna mtu anayeshabikia ukahaba,ila inafaa tuchague mahali pa kuweka nguvu zetu.
Tangu enzi za yesu makahaba walikuwepo Luka 36 -50 na ni biashara ambayo haitakaa ikome hadi mwisho wa dunia.

Kuna changamoto nyingi ambazo yafaa viongozi wapambane nazo kuliko kukimbizana na mtu anayeuza uchi wake kwasababu ni sawa na kufukuza upepo ,hakuna mwisho.Wilaya ya ubungo ina kero lukuki hazifanyii kazi anakimbizana na wauza uchi
 
Malaya walishashindikana tangu enzi za Yesu Kristu ni sehemu ya maisha ya jamii.

Kuna clip ya Nyerere baba wa taifa akiwa mtawala, itafute you tube ilitoa tafsiri sahihi ya umuhimu wa watu hao kuwepo katika jamii na namna wanavyoliponya taifa.

Kwanza jiulize kwanini hakuna sheria kali ya maana inayowabana, wakitiwa nguvuni wanashitakiwa kwa uzururaji, haujiulizi?

Ukiona jambo halitiliwi maanani katika kulipiga kwake vita sawasawa na kisha kulitokomeza, elewa jambo hilo linakubalika kwa mlango wa nyuma, ndiyo maana mataifa ya werevu yanawatambua na yanawatoza kodi halali.

Sehemu ya jamii ambayo hata ikipigwa vita isiyoisha milele na milele, elewa vita hivyo vilishashindwa na iliyobaki ni usumbufu na kuvuta attention ya kijamii tu kwa kutaka sifa.

Haya, mmekamata malaya wa Sinza sijui Kinondoni, je wa maeneo mengine ya mji ama miji mingine nchini mtawadhibiti vipi, hauoni kuwa huo ni u double standard?

Operesheni hiyo ni ya kiuonevu na yenye kuleta taharuki zisizokuwa na ulazima wowote.

Tulishachoka kusikia habari hizo za kidhalilishaji zilizokwishakushindikana.
 
Asante mkuu. Ubungo kero za kutosha kabisa. Uchafu Kama wote, maji shida, miundombinu imechoka..Ila huyu DC aliyeshiba kodi zetu anakuja na ujinga kama huu.

Hata angeanza na mkakati wa kupanda miti, Usafi nk.

Hivi mama Samia hawa watu anawatoa wapi? They are simply out of ideas.
 
Mwambie aende na Hyatt regency na Serena hotel
 
Haki kama zipi?
 
Serikali ipambane na wanunuaji. Muuzaji ana kosa gani kama mnunuaji yupo.
 
Wabadilishe kwanza sheria ndilo jambo la msingi. Tusiruhusu kiongozi afanye kwa matakwa yake. Leo atafanya jambo litakalokufurahisha nje ya sheria utafurahi, kesho akifanya lisilokufurahisha nje ya sheria utalalamika. Bunge libadilishe au litunge sheria ambazo zitahalamisha hii biashara.
 
jamaa alitakiwa awavamie ,awatandike bakora za kutosha na kuwachania hivo vinguo
basi na aswakamate kutengeneza ushahidi
imekula kwake
hao watu hawafanyi poa, jinsi ya kudeal nao ndo inahitaji akili la sivyo wapenda haki watakunyoosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…