Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Nadhani inabidi ujitafakari sana kukubali kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya, kwa sababu inabidi ujitoe kabisa kwenye profession yako na kujiondoa uwezo wa kufikiri ili uweze kwenda sambamba na makada wa chama. Ukijifanya intellectual utagombana nao kila siku, hasa unapokuta mtu wa darasa la saba na ndio anakupa maagizo wakati wewe una degree zako nne!

Hayo mambo ni kuwaachia watu wa aina ya kina Hapi na Muro.

Halafu Samia aache tabia ya kuteua watu kabla ya kuwauliza kwanza, ataumbuka sana. Nyerere akitaka kukuteua alikuwa anakuuliza kwanza, utaweza? Ukisema siwezi anakuacha. Ndio maana Malecela alipoulizwa ataweza kuwa PM, akasema ndio, akafanya sherehe kabla ya kutangazwa rasmi, alitemwa.
Sio kweli Habari zako; Malecela hakutemwa kwa sababu hiyo kwani Alisha kuwa Waziri mkuu!!
 
Salaam Wakuu,

Japheth Maganga aliyetuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera akataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya alioteuliwa na Rais Samia hivi karibuni.

Japhet kasema, baada ya Kushauriana na Familia yake, alimuandikia rais Samia kumshukuru kwa kumteua pia na kumuomba atengue uteuzi wake na achaguliwe mtu Mwingine.

Wateule wengine ambao wamekataa uteuzi ni:

Leah Ulaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mkoa wa Geita na na Dina Mathamani aliyeteuliwa kwenda Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma

Wote waliokataa Uteuzi wa Rais Samia ni Viongozi wa juu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Leah Ulaya ni rais wa CWT, Dinah Mathamani ni Makamu wa Rais wa CWT huku Japheth Maganga akiwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)

======

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japheth Maganga ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ameshiriki kuongoza mkutano wa viongozi wa chama hicho jijini Tanga huku akisema kwa sasa hawezi kueleza kwanini hajaripoti katika wilaya aliyopangiwa ya Kyerwa, mkoani Kagera.

Vilevile, Maganga alihojiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga zaidi ya dakika 50 lakini si yeye wala wanausalama hao walioweka wazi sababu za mahojiano hayo.

Maganga na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa wiki iliyopita na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wakuu wa wilaya lakini wakati wenzao wakiapishwa kwenye maeneo yao leo Jumatatu, Januari 30, 2023 wao wapo Tanga wakiongoza mkutano wa viongozi wakuu wa CWT.

Ulaya aliteuliwa kuwa DC wa Mbogwe, Mkoa wa Geita ambapo wenzake wanaapishwa leo Jumatatu na Mkuu wa Mkoa huo, Martin Shigela.

Mara baada ya kumaliza kuhojiwa na polisi kuanzia saa 4:36 hadi saa 5:24 asubuhi nje ya ukumbi wa mkutano huo unaofanyikia katika Hoteli ya Regal Naivera, Mtaa wa Bombo jijini Tanga Maganga alirejea ukumbini na baadaye kidogo alitoka nje.

Nje ya ukumbi ambapo Mwananchi Digital limeweka kambi, Magamba amesema, “kwa sasa nimeziba mdomo labda usubiri tutakapomaliza kikao ndipo nitazungumza kuhusu nafasi ya U-DC na CWT."

Wakati Maganga akisema hayo, Rais wa CWT hakutoka ndani ya ukumbi wa mkutano huo huku maofisa wa CWT wakisema hajaruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.

Kitendo cha viongozi wakuu hao wa CWT kuonekana Tanga wakati wenzao wakiapishwa kimezua mjadala mitandaoni na kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba wameomba wateuliwe wengine kwenye nafasi hizo za U-DC ili kuwawezesha kuendelea na majukumu yao katika chama cha walimu.

Chanzo: DC mteule ahojiwa na polisi dakika 50, Rais CWT…
* Zile Gari za wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wanaziacha wakistaafu au wanaondoka nazo?*
 
Aliyewaambia wanataka kuwa viongozi wa kisiasa ni nani? Haya maisha jifunze kuwa huru usipende kuburuzwa kipumbavu. Nafasi ya hawa viongozi wa CWT kiajira wao ni walimu hawakwenda SONGEA TTC kusomea ukuu wa wilaya walienda wawe walimu na kazi zote za majukumu ya ualimu, Kugomea teuzi sio kosa kisheria kama ni kosa Nipe kifungu sio maneno matupu.

Mwajiri wa mwalimu ni mkurugenzi maana wapo chini ya serikali za mitaa (halmashauri) na sio Rais acheni ubabaishaji hakuna Mwajiri namba moja Wala namba kumi Mwajiri ni mmoja tu MKURUGENZI nahakuna kipengere chochote cha mkataba kinasema ni kosa Kugomea uteuzi bali Kuna kipengere kinasema utakuwa tayari kufanya kazi ya ualimu na majukumu mengine utakayopangiwa maana ake yale tu ndani ya proffesion na uwanja wako wa kazi kama kuwa mtaaluma, mkuu wa shule na mengineyo
Msimamo wangu upo pale pale!

KWA katiba iliyopo kila mtumishi wa umma ni mwanasiasa!tena anatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi CCM hakuna uzi MKUBWA unaotenganisha Kati ya SIASA na SERIKALI !

Wapeni Moyo!Labda Rais awachukulie poa KWA kumdharau YEYE na MAAMUZI yake!

SHERIA mama ya kikatiba inampa Mamlaka Rais kuvunja hata hizo SHERIA ndogo ndogo KWA ukubwa wa kiti CHAKE!MSIJIDANGANYE WAKUU

HHuyo mkurugenzi unaejidaia ni mtumishi wa Rais wa kuteuliwa!

Ndio MAANA ccm ukiona kuna haja ya katiba Mpya na Sasa wametangaza marekebisho yake!

Kama Rais Anaweza akaamua asipandishe MISHAHARA hata Miaka KUMI na hakuna sheria ya kufanya lolote sembuse kukataa UTEUZI Wake!!?

KATIBA NDIO KILA KITU KINACHOMPA KIBURI RAIS KUFANYA LOLOTE!!

UNAFIKIRI NDANI YA CWT HAKUNA SIASA!!?TENA SIASA CHAFU ZA RUSHWA NA UBADHIRIFU WA KILA AINA!

MSIJIDANGANYE NDANI YA CHAMA CHA WALIMU HAKUNA SIASA ZIPO ZA KUTOSHA NA NZITO!!

TUENDELEE KUSUBIRIA!
 
Kuwa Rais siyo kwmba ni kigezo cha kukamilika watu wanayo haki ya kukataa mawazo au maamuzi yako pia.
Huu uteuzi umekaa kifitna fitna kuwamwagia ugali wao hao jamaa, wapoteze hizo 7M kwa mwezi waende kwenye 3M alafu wapigwe chini, wakija kurud huku kwenye 7M wakute nafasi zao zimechukuliwa na watu wengine.

Sasa wahuni wameshtuka hakuna anaetaka kumwagiwa chakula chake
 
Watoke tu hapo CWT, Kuna ukaguzi wa hesabu unakuja hapo muda si mrefu. Wamekaa wanawaza kuiba tu Hela za waalimu, serikali imefanya kuwatoa kwa staha, ila kama hawataki, watatokea kisutu.

Tunajua kinachofanya wagombane ni wizi wa Hela za waalimu, na wao ndio wezi wakuu
Huo ni uchawi acheni kuwazulia watu mambo ambayo hayana uhakika.hii tabia ya MACCM kuzulia watu mambo mabaya ni kawaida yao ndo maana yamekaa kichawachawa.kwani kama mtu unakataa uteuzi shida ni nini!ni lazima mtu kukubali uteuzi?acheni roho mbaya.
 
Nani aliyekwambia kukubali uteuzi ndiyo kunamuweka huru dhidi ya shutuma alizo nazo? Tangu lini wakuu wa Wilaya wana kinga ya kutoshitakiwa?
Kwani ni kipi kilichomtokea aliyekua Mkurugenzi wa Halmashauri huko Ruangwa? Alipiga hela alipokuwa Mkurugenzi wa Halmashauri. Baadaye akateuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya, juzijuzi tu hapa TAKUKURU wamemfungulia Mashitaka akiwa kwenye nafasi yake ya ukuu wa Wilaya hali iliyopelekea rais kutengua uteuzi wake.

Au kama ana hizo shutuma halafu akang'ang'ania kubaki kwani kunampa kinga ya kutochunguzwa na kushitakiwa?
Mbon tunaongea vitu bila kutumia vyema ufahamu wetu?
Una kichwa kigumu sana. Nimeandika kuna ugumu kuendesha mashtaka wewe unasema kunamuweka huru dhidi ya shutuma. Vitu viwili tofauti mno.

Ditopile alipomuua dereva daladala mchana kweupe kwa risasi alifungwa? Chukua bastola nawe mpige risasi mtu mchana kwenye foleni uone kama hatujakusahau. Unakaza fuvu badala ya kuelewa context ya ninachomaanisha.

Mkuu wa wilaya gani aliwahi fungwa tuseme kuanzia awamu ya nne? Wakati kibao walikuwa na tuhuma mbalimbali
 
Vyovote iwavyo hili swala me nalichukulia kama ni mpango wa kukiyumbisha na kukiharibu hicho chama Cha maticha.

Huwezi kwa wkt mmoja kuwaondoa kwenye nafasi zao katibu, Naibu katibu pamoja na Rais wa hicho chama kwa kigezo Cha uteuzi tena wa ukuu wa wilaya.

Nikweli inaweza ikawa sio vyema sn kukataa uteuzi wa Rais lkn tuangalie nyuma ya pazia uteuzi huo una agenda gani ya Siri nyuma yake kwa chama Cha maticha?
Amuombee chawa Pascal Mayala hiyo nafasi maana karibia ataokota makopo huku JF kwa shauku ya kuteuliwa.
 
mi nawashangaa mnaoimba katiba mpya !

hivi katiba ni kiumbe kwamba isipotekelezwa itasema ?

mbona sheria zetu ni nzuri sana ila raia bado tu tunapata tabu sana ?

katiba mpya ni makaratasi tu ila msoto utakua pale pale
Hujui usemalo wala ujualo..

Kubali kujifunza kwa wengine juu ya nini wanaelewa kuhusu katiba na mahusiano yake na maisha ya Kila siku..!
 
Unaona kazi ya U-DC ni ya maana sana, na rais kwako ni Mungu, hivyo mtu akichaguliwa kuwa mkuu wa wilaya inabidi atetemekee nafasi hiyo. Hiyo ni kazi ya majobless, na watu wanaojipendekeza.
Zamani madereva wa TANU wakikaribia kustaafu walipewa uDC
 
Mjambiani ni mpuuzi wa wapuuzi unawapaje watu ka,i bila ya wao kukuambia kuwa wanataka hiyo kazi au wanauwezo nayo ...ni sawa sawa umsajiri fei toto kuwa kipa [emoji849][emoji849] tukisema huyu ajuza kanya akili na kubakisha kinyesi watu wanasema tunatukana ...mfano unamwamisha joketi wakati unajua ndiyo katoka kujifungua hivi majuzi
kwanini unamtukana mkuu..
 
Hata ingekuwa ww ungelikataa . Kutoka kupokea mshahara 7.8 ml hadi 3 milion??? Kisa tu mkuu wa wilaya ya huko kyerwa ?!!? Mji kuu wa wilaya ni Nkwenda .. [emoji23][emoji23][emoji23]
Kwani CWT si ipo chini ya serikali ama? maana kama ni hivo mishahara unabaki pale pale
 
Salaam Wakuu,

Japheth Maganga aliyetuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera akataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya alioteuliwa na Rais Samia hivi karibuni.

Japhet kasema, baada ya Kushauriana na Familia yake, alimuandikia rais Samia kumshukuru kwa kumteua pia na kumuomba atengue uteuzi wake na achaguliwe mtu Mwingine.

Wateule wengine ambao wamekataa uteuzi ni:

Leah Ulaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mkoa wa Geita na na Dina Mathamani aliyeteuliwa kwenda Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma

Wote waliokataa Uteuzi wa Rais Samia ni Viongozi wa juu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Leah Ulaya ni rais wa CWT, Dinah Mathamani ni Makamu wa Rais wa CWT huku Japheth Maganga akiwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)

======

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japheth Maganga ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ameshiriki kuongoza mkutano wa viongozi wa chama hicho jijini Tanga huku akisema kwa sasa hawezi kueleza kwanini hajaripoti katika wilaya aliyopangiwa ya Kyerwa, mkoani Kagera.

Vilevile, Maganga alihojiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga zaidi ya dakika 50 lakini si yeye wala wanausalama hao walioweka wazi sababu za mahojiano hayo.

Maganga na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa wiki iliyopita na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wakuu wa wilaya lakini wakati wenzao wakiapishwa kwenye maeneo yao leo Jumatatu, Januari 30, 2023 wao wapo Tanga wakiongoza mkutano wa viongozi wakuu wa CWT.

Ulaya aliteuliwa kuwa DC wa Mbogwe, Mkoa wa Geita ambapo wenzake wanaapishwa leo Jumatatu na Mkuu wa Mkoa huo, Martin Shigela.

Mara baada ya kumaliza kuhojiwa na polisi kuanzia saa 4:36 hadi saa 5:24 asubuhi nje ya ukumbi wa mkutano huo unaofanyikia katika Hoteli ya Regal Naivera, Mtaa wa Bombo jijini Tanga Maganga alirejea ukumbini na baadaye kidogo alitoka nje.

Nje ya ukumbi ambapo Mwananchi Digital limeweka kambi, Magamba amesema, “kwa sasa nimeziba mdomo labda usubiri tutakapomaliza kikao ndipo nitazungumza kuhusu nafasi ya U-DC na CWT."

Wakati Maganga akisema hayo, Rais wa CWT hakutoka ndani ya ukumbi wa mkutano huo huku maofisa wa CWT wakisema hajaruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.

Kitendo cha viongozi wakuu hao wa CWT kuonekana Tanga wakati wenzao wakiapishwa kimezua mjadala mitandaoni na kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba wameomba wateuliwe wengine kwenye nafasi hizo za U-DC ili kuwawezesha kuendelea na majukumu yao katika chama cha walimu.

Chanzo: DC mteule ahojiwa na polisi dakika 50, Rais CWT…
Haya weeeeee
 
Back
Top Bottom