Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Hujui usemalo wala ujualo..

Kubali kujifunza kwa wengine juu ya nini wanaelewa kuhusu katiba na mahusiano yake na maisha ya Kila siku..!
kwanza katiba yenyewe ni kikafir hata nikijifunza hainisaidii kitu duniani na akhera zaidi ya kulalalisha alivyoharamisha Mwenyezi Mungu 😏
 
Kuna ubaya gani kukataa nafasi ambayo unaona kwako, hutaimudu au hutakuwa na furaha nayo.
Nadhani watu ni wachochezi kwamba mtu akikataa nafasi aliyopewa anamdharau aliyempa hiyo kazi. Mtu naweza kuipenda kazi fulani sio kwa sababu ya maslahi ya cheo na mengineyo. Kazi ya kuteuliwa si ya kudumu, muda wo wote unaweza kuondolewa na yule aliyekuteua. Ukiangalia hivyo mtu mwingine anaweza kuona hapana hata kama ni kiongozi anayemheshimu amempa, lakini nikifukuzwa au kuondolewa baada ya muda mfupi itakuwaje.
Naamini Rais ni mwelewa haya mambo sio mara ya kwanza kutokea. Atachukuliana nao tu.
Nafikiri labda ingekuwa nzuri hao walioteluliwa kabla ya kutangazwa waarifiwe kama wanakubali au la. Kuliko kushtushwa kwenye vyombo vya habari.
 
Hii ni nzuri sana.

Mtu unateuliwa kwa mbwembwe unaacha shughuki zako baada ya mwaka unatupwa nje ya uteuzi kwa aibu. Hizi nafasi za uteuzi waachiwe majibless na makada tu hazina maana ni kuharibiana maisha kwa kutenguana hivyo hovyo.
Wazo Bora la mwezi January.
 
31 January 2023
Dodoma, Tanzania

Waziri Jenista Mhagama azungumzia sakata la viongozi wa juu Chama wa Walimu Tanzania kukacha U-DC

Waziri wa serikali ya Muungano amesema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Rais amepewa madaraka ya kukasimu majukumu yake ya utendaji wakazi ndani ya Serikali kwa watu mbalimbali kwa kutumia sifa na vigezo walivyonavyo.

Waziri, Ofisi ya Rais - Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama amesema kuwa wizara yake inasubiria taarifa rasmi kuhusu watumishi wawili ambao ni viongozi wa CWT ambao hawakuapishwa baada ya kuteuliwa na Rais samia kuwa wakuu wa wilaya.

“Kwa hiyo taarifa tutakazoletewa kwenye wizara zinazohusika na sisi tutaangalia taratibu zetu zikoje, miundo yetu ya kiutumishi inasema nini? Taratibu za kisheria zinasema nini kupata taarifa rasmi kutoka kutoka wizara wanazowajibika,” amesema.

Amesema baada ya hapo kama kutakuwa jambo lolote ambalo litatokana na wao basi watawataarifu Watanzania.


Mhagama amesema hayo leo Jumanne Januari 31,2023 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
 
Ila si ni ajira ya kudumu?
DCs/RCs ni post za kisiasa na ukifutwa unarudi kwako chap kwa haraka. Ni DEDs tu ndio wakitumbuliwa hubaki Serikalini, provided hakufukuzwa kwa kosa la jinai linalowezs kumfanya akatupwa lupango
 
Hii ni nzuri sana.

Mtu unateuliwa kwa mbwembwe unaacha shughuki zako baada ya mwaka unatupwa nje ya uteuzi kwa aibu. Hizi nafasi za uteuzi waachiwe majibless na makada tu hazina maana ni kuharibiana maisha kwa kutenguana hivyo hovyo.
Kama ni mtumishi wa umma ukitenguliwa unarudi kwenye kibarua chako
 
kwanza katiba yenyewe ni kikafir hata nikijifunza hainisaidii kitu duniani na akhera zaidi ya kulalalisha alivyoharamisha Mwenyezi Mungu 😏
Haa haa🥺 haa🥺🥺🥺

Wee jamaa ni jiwe kwelikweli lisilofikiri wala kujua lolote.

Wewe hata ukifika akhera lazima utapokelewe langoni kwa hamsa kama 70 hivi kwa kuwa "mjinga" duniani kwa kudharau na kupuuza mambo ya msingi.!
 
Haa haa🥺 haa🥺🥺🥺

Wee jamaa ni jiwe kwelikweli lisilofikiri wala kujua lolote.

Wewe hata ukifika akhera lazima utapokelewe langoni kwa hamsa kama 70 hivi kwa kuwa "mjinga" duniani kwa kudharau na kupuuza mambo ya msingi.!
hakuna mambo ya msingi hapa hata hao wanaojiita viongozi jehannam inawangoja kwa kuacha sheria za Mwenyezi Mungu na kutengeneza za kwao(katiba ya kikafir) na kuhalalisha alioyaharamisha Mwenyezi Mungu.

kama humuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho huwezi kunielewa
 
Kwa heri, usiku mwema ndugu yangu
 
Wanacheza na state hao.
 
Wengine wanasema G. Mongella wakati wa MWINYI.
 
Hv Mhe. Rais kwa nn usiniteue Mimi nikakusaidie Majukumu kwa watanzania wenzangu waliopo huko? kukataa uteuzi wa Mhe. Rais ni Ishara ya ujeuri.
 
Huko kwenye chama chao wana uhakika wa kulamba asali wapendavyo na watakavyo sasa huku kwa mama mara leo upo mara ksho umetenguliwa, mara chawa wakuandame, shida yote ya nini, kwenye chama cha walimu kuna michango na pesa ya bure ambayo hata bunge haliingilia, hawa wote watatu wamekaa kwa pamoja na hawa kwa pamoja ndio wanalamba asali ya walimu kiulaini, nadhani waangaliwe kwa jicho la tatu, si bure kukataa kwao kuna kitu nyuma ya pazia.
 
Posho za safari ya kwenda wapi tena wakati amepangiwa kutumika ndani ya wilaya husika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…