Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Salaam Wakuu,

Japheth Maganga DC wa Kyerwa akataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya alioteuliwa na Rais Samia hivi karibuni.

Japhet kasema, baada ya Kushauriana na Familia yake, alimuandikia rais Samia kumshukuru kwa kumteua pia na kumuomba atengue uteuzi wake na achaguliwe mtu Mwingine.

Wateule wengine ambao wamekataa uteuzi ni:

Leah Ulaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mkoa wa Geitana na Dina Mathamani aliyeteuliwa kwenda Wilaya ya Uvinza

======

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japheth Maganga ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ameshiriki kuongoza mkutano wa viongozi wa chama hicho jijini Tanga huku akisema kwa sasa hawezi kueleza kwanini hajaripoti katika wilaya aliyopangiwa ya Kyerwa, mkoani Kagera.

Vilevile, Maganga alihojiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga zaidi ya dakika 50 lakini si yeye wala wanausalama hao walioweka wazi sababu za mahojiano hayo.

Maganga na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa wiki iliyopita na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wakuu wa wilaya lakini wakati wenzao wakiapishwa kwenye maeneo yao leo Jumatatu, Januari 30, 2023 wao wapo Tanga wakiongoza mkutano wa viongozi wakuu wa CWT.

Ulaya aliteuliwa kuwa DC wa Mbogwe, Mkoa wa Geita ambapo wenzake wanaapishwa leo Jumatatu na Mkuu wa Mkoa huo, Martin Shigela.

Mara baada ya kumaliza kuhojiwa na polisi kuanzia saa 4:36 hadi saa 5:24 asubuhi nje ya ukumbi wa mkutano huo unaofanyikia katika Hoteli ya Regal Naivera, Mtaa wa Bombo jijini Tanga Maganga alirejea ukumbini na baadaye kidogo alitoka nje.

Nje ya ukumbi ambapo Mwananchi Digital limeweka kambi, Magamba amesema, “kwa sasa nimeziba mdomo labda usubiri tutakapomaliza kikao ndipo nitazungumza kuhusu nafasi ya U-DC na CWT."

Wakati Maganga akisema hayo, Rais wa CWT hakutoka ndani ya ukumbi wa mkutano huo huku maofisa wa CWT wakisema hajaruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.

Kitendo cha viongozi wakuu hao wa CWT kuonekana Tanga wakati wenzao wakiapishwa kimezua mjadala mitandaoni na kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba wameomba wateuliwe wengine kwenye nafasi hizo za U-DC ili kuwawezesha kuendelea na majukumu yao katika chama cha walimu.

Chanzo: DC mteule ahojiwa na polisi dakika 50, Rais CWT…
Kwa nini wanawateua bila kushauriana nao?

Kwanza huko mtaani watu wanadharau cheo Cha DC kwamba hakina maslahi, unadhani wangeteuliwa kuwa Ma DED wangekataa?

Wanayofanya vetting ni wapuuzi Kwa sababu huwezi mtoa mtu sehemu yenye ulaji umpeleke huko kusiko na ulaji..

Hizo nafasi wawape watu wenye vyeo na ulaji mdogo tena wako wengi tuu.
 
Kama habari yako ni kweli. Mbona rahisi tu, si waandikiwe barua za kujiuzuru vyeo vyao vya CWT wapelekewe wasaini hizo barua. Halafu tuone watakavyokataa u-DC. Waombe tu wasifanyiwe hivyo baada mama kuteua wengine kuziba nafasi zao. " Mama juzi katoka kukopa,, nchi hii itapigwa Mnada".
 
UDC ni dili sana kwa Machawa wenye njaa! Katibu Mkuu wa CWT ni mtu mzito sana kimajukumu na hata kimapato!
Hivi vyeo vya Wakuu wa Wilaya havina impact kwenye maisha ya Wananchi na ni matumizi mabaya tu ya Kodi za Wananchi!
Kuna Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri au Manispaa ambaye ni mtaalamu na pia kuna Meya au Mwenyekiti wa Halmashauri, sasa Mkuu wa Wilaya wa nini?!
Naunga mkono hoja, hizi post za DC ni muendelezo tuu wa colonial legacy, but in reality the post is redundancy, just wastage of time, money and resouses za Watanzania masikini wa kutupa wanaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea.
P
 
Salaam Wakuu,

Japheth Maganga aliyetuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera akataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya alioteuliwa na Rais Samia hivi karibuni.

Japhet kasema, baada ya Kushauriana na Familia yake, alimuandikia rais Samia kumshukuru kwa kumteua pia na kumuomba atengue uteuzi wake na achaguliwe mtu Mwingine.

Wateule wengine ambao wamekataa uteuzi ni:

Leah Ulaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mkoa wa Geita na na Dina Mathamani aliyeteuliwa kwenda Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma

Wote waliokataa Uteuzi wa Rais Samia ni Viongozi wa juu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Leah Ulaya ni rais wa CWT, Dinah Mathamani ni Makamu wa Rais wa CWT huku Japheth Maganga akiwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)

======

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japheth Maganga ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ameshiriki kuongoza mkutano wa viongozi wa chama hicho jijini Tanga huku akisema kwa sasa hawezi kueleza kwanini hajaripoti katika wilaya aliyopangiwa ya Kyerwa, mkoani Kagera.

Vilevile, Maganga alihojiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga zaidi ya dakika 50 lakini si yeye wala wanausalama hao walioweka wazi sababu za mahojiano hayo.

Maganga na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa wiki iliyopita na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wakuu wa wilaya lakini wakati wenzao wakiapishwa kwenye maeneo yao leo Jumatatu, Januari 30, 2023 wao wapo Tanga wakiongoza mkutano wa viongozi wakuu wa CWT.

Ulaya aliteuliwa kuwa DC wa Mbogwe, Mkoa wa Geita ambapo wenzake wanaapishwa leo Jumatatu na Mkuu wa Mkoa huo, Martin Shigela.

Mara baada ya kumaliza kuhojiwa na polisi kuanzia saa 4:36 hadi saa 5:24 asubuhi nje ya ukumbi wa mkutano huo unaofanyikia katika Hoteli ya Regal Naivera, Mtaa wa Bombo jijini Tanga Maganga alirejea ukumbini na baadaye kidogo alitoka nje.

Nje ya ukumbi ambapo Mwananchi Digital limeweka kambi, Magamba amesema, “kwa sasa nimeziba mdomo labda usubiri tutakapomaliza kikao ndipo nitazungumza kuhusu nafasi ya U-DC na CWT."

Wakati Maganga akisema hayo, Rais wa CWT hakutoka ndani ya ukumbi wa mkutano huo huku maofisa wa CWT wakisema hajaruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.

Kitendo cha viongozi wakuu hao wa CWT kuonekana Tanga wakati wenzao wakiapishwa kimezua mjadala mitandaoni na kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba wameomba wateuliwe wengine kwenye nafasi hizo za U-DC ili kuwawezesha kuendelea na majukumu yao katika chama cha walimu.

Chanzo: DC mteule ahojiwa na polisi dakika 50, Rais CWT…
Hawa si wametajwa kuwa na tuhuma lukuki!!!
 
Watoke tu hapo CWT, Kuna ukaguzi wa hesabu unakuja hapo muda si mrefu. Wamekaa wanawaza kuiba tu Hela za waalimu, serikali imefanya kuwatoa kwa staha, ila kama hawataki, watatokea kisutu.

Tunajua kinachofanya wagombane ni wizi wa Hela za waalimu, na wao ndio wezi wakuu
Aisee
 
Back
Top Bottom