Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Ka
Salaam Wakuu,

Japheth Maganga aliyetuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera akataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya alioteuliwa na Rais Samia hivi karibuni.

Japhet kasema, baada ya Kushauriana na Familia yake, alimuandikia rais Samia kumshukuru kwa kumteua pia na kumuomba atengue uteuzi wake na achaguliwe mtu Mwingine.

Wateule wengine ambao wamekataa uteuzi ni:

Leah Ulaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mkoa wa Geita na na Dina Mathamani aliyeteuliwa kwenda Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma

Wote waliokataa Uteuzi wa Rais Samia ni Viongozi wa juu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Leah Ulaya ni rais wa CWT, Dinah Mathamani ni Makamu wa Rais wa CWT huku Japheth Maganga akiwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)

======

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japheth Maganga ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ameshiriki kuongoza mkutano wa viongozi wa chama hicho jijini Tanga huku akisema kwa sasa hawezi kueleza kwanini hajaripoti katika wilaya aliyopangiwa ya Kyerwa, mkoani Kagera.

Vilevile, Maganga alihojiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga zaidi ya dakika 50 lakini si yeye wala wanausalama hao walioweka wazi sababu za mahojiano hayo.

Maganga na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa wiki iliyopita na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wakuu wa wilaya lakini wakati wenzao wakiapishwa kwenye maeneo yao leo Jumatatu, Januari 30, 2023 wao wapo Tanga wakiongoza mkutano wa viongozi wakuu wa CWT.

Ulaya aliteuliwa kuwa DC wa Mbogwe, Mkoa wa Geita ambapo wenzake wanaapishwa leo Jumatatu na Mkuu wa Mkoa huo, Martin Shigela.

Mara baada ya kumaliza kuhojiwa na polisi kuanzia saa 4:36 hadi saa 5:24 asubuhi nje ya ukumbi wa mkutano huo unaofanyikia katika Hoteli ya Regal Naivera, Mtaa wa Bombo jijini Tanga Maganga alirejea ukumbini na baadaye kidogo alitoka nje.

Nje ya ukumbi ambapo Mwananchi Digital limeweka kambi, Magamba amesema, “kwa sasa nimeziba mdomo labda usubiri tutakapomaliza kikao ndipo nitazungumza kuhusu nafasi ya U-DC na CWT."

Wakati Maganga akisema hayo, Rais wa CWT hakutoka ndani ya ukumbi wa mkutano huo huku maofisa wa CWT wakisema hajaruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.

Kitendo cha viongozi wakuu hao wa CWT kuonekana Tanga wakati wenzao wakiapishwa kimezua mjadala mitandaoni na kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba wameomba wateuliwe wengine kwenye nafasi hizo za U-DC ili kuwawezesha kuendelea na majukumu yao katika chama cha walimu.

Chanzo: DC mteule ahojiwa na polisi dakika 50, Rais CWT…
Mkama Ana uhakika wa kuongiza hyo cwt kwa takrban miaka 5 bas Ana haki ya kukataa kuendelea
 
UDC ni dili sana kwa Machawa wenye njaa! Katibu Mkuu wa CWT ni mtu mzito sana kimajukumu na hata kimapato!
Hivi vyeo vya Wakuu wa Wilaya havina impact kwenye maisha ya Wananchi na ni matumizi mabaya tu ya Kodi za Wananchi!
Kuna Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri au Manispaa ambaye ni mtaalamu na pia kuna Meya au Mwenyekiti wa Halmashauri, sasa Mkuu wa Wilaya wa nini?!

Kuna watu wanajuaga kuteuliwa tuu bila kujua wanachenda kukifanya
Au kupima hasira ya wanachokiacha ili wakawe madc au maded
Ni vizuri wakapewa taarifa na kutoa mrejesho kabla ya kuteuliwa
 
WAALIMU WAJIPANGA KUJIKOMBOA KUTOKA CCM ?

Safi ni dalili ya mwanga unaoangaza wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kutaka kujikomboa kutoka kucha za chama dola na kukataa kuwa Jumuiya ya CCM kama zilivyo UVCCM, UWT, WAZAZI

16 December 2022
Dodoma, Tanzania

VURUGU ZAIBUKA MKUTANO WA CHAMA CHA WALIMU, WAMTIMUA KAIMU RAIS Bi. Dinah Mathamani
huku Bi. Leah Ulaya .....



Kwa sasa CWT inaongozwa na Kaimu Rais Dinah Mathamani na Kaimu Katibu Mkuu Japheth Maganga baada ya viongozi wa juu kusimamishwa kwa nyakati tofauti.

CWT kimesakamwa sana kama TLS chama cha mawakili Tanganyika kwa muda mrefu ili kiwe pamoja na CCM

Mwaka 2017:
1675093326538.png


Waalimu wamekuwa wakirushiwa lawama kukubali kutumika na CCM ili ibaki madarakani huku waalimu mazingira yao ya kufanya kazi ni magumu mfano darasa moja lina wanafunzi 200 na anatakiwa awafunze watoto hao ili wafaulu vizuri wakati ni vigumu.
1675094323855.png

Inatakiwa wastani wa Mwalimu kwa darasa iwe 1 : 30 yaani darasa lisizidi wanafunzi 30 ili mwalimu aweze kutoa elimu sahihi kwa watoto na kuweza kusahihisha kazi zao n.k n.k


Lakini serikali ya CCM haioni hilo la mzigo mkubwa kwa waalimu na wanafunzi kutofanya vizuri ktk mitihani yao ya ngazi mbalimbali na mwisho wa siku wanalaumiwa waalimu kwa kutofundisha wanafunzi wapate alama nzuri.
mwananchi.co.tz
https://www.mwananchi.co.tz › kitaifa
ELIMU: Darasa moja, wanafunzi 370


9 Mar 2021 — Wanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Nyamarere mkoani Geita wakiwa darasani.....
 
CWT ni kichaka cha wizi,Rushwa, UFISADI na UBADHIRIFU!

Tunaomba Serikali ishushe makato ya ya CWT hayana tija KWA walimu tuliopo Field huku!

Ndio Maana Hata taaluma inashuka nchini Kwasababu ya kupe kama hao! mishahara haipandi halafu makato yanapanda KWA asilimia!

Wizi na UFISADI wa CWT umefanya wahusika wadharau uteuzi wa RAIS!

Nina imani SERIKALI itashughulika na CHAMA HIKI!
 
Ni wakati sasa Rais amkumbuke Paskali Myala.
Aisee, humu huwa tunamtania tu Pascal Mayalla kumhusisha na hizi nafasi. Msije mkachulia kuwa watu wakisema wapo serious. The guy is the living legend na heshima yake ni kubwa sana kuwa associated na kumsaidia rais katika ngazi ya such positions. Ni heri aendelee kumsaidia rais kulipa kodi kuliko kwenye nafasi hizo
 
Back
Top Bottom