Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Matatizo ya waalimu kazini yanayotetewa na CWT lakini serikali haioni umuhimu kwa vile watoto wa vigogo hawasomi shule za kata au vijijini mfano wingi kupitiliza wa wanafunzi ktk darasa moja mfano darasa lina wanafunzi 370 huku lina mwalimu mmoja. Hilo unalizungumziaje ?
Hakuna kitu hapo!

Makato yashushwe!

Huo utetezi haujitaji makato ya asilimia mbili ya mshahara!
 
KINA MAMA WANASIMAMIA UKWELI NA KUFIKISHA UJUMBE BILA KUYUMBA

Dina Mathamani - Tunafuatilia waalimu walionyanganywa barua zao



Dina Mathamani asisitiza mamlaka husika kuzingatia haki za waalimu mfano Likizo, mafunzo, matibabu na mazingira mazuri ya kazi kwa waalimu yatizamwe kwa karibu ..
 
Hakika viongozi wanawake hawataki kuburuzwa, hongera kwa viongozi wa CWT

13April 2021


Bi Leah Ulaya rais wa Chama Cha Waalimu Tanzania atoa angalizo kwa sheria inayowahusu waalimu iliyopitishwa na Bunge.

Rais wa CWT anaonesha mapungufu ya sheria iliyopitishwa na bunge kwa sababu za msingi zifuatazo ...



Chama cha waalimu Tanzania CWT kimesisitiza kuwa hakikubaliani na uanzishwaji wa Bodi ya waalimu kwani utendaji kazi wake licha ya kufanana majukumu na Tume ya Utumishi wa Walimu pia inamkandamiza mwalimu kwa kumbebesha garama za uendeshaji. Rais wa chama cha waalim Tanzania Mwalim Leah Ulaya amesema wakati wa uundwaji wa Sheria inaunda bodi hiyo mapendekezo yaliyotolewa na waalimu hayakuzingatiwa hivyo bodi hiyo inamkandamiza mwaalimu

Hamna kitu hapo! CWT iondolewe HAINA tija KWA Mwalimu!!!

HAINA mchango wowote KWA MSTAKABALI wa walimu nchini!

Makato makubwa AMBAYO hayana tija KWA walimu!
 
KATIBU MKUU WA CWT Bw. Japhet Maganga ahaidi wajumbe wa mkutano wa CWT kuwa kauli mbiu ya kwenda pamoja, kuwa wamoja na mshikamano ataitekeleza bila kuyumba ...

 
Asante sana Mkuu PakiJinja, kiukweli mtu kuteuliwa kumsaidia rais kwa kuwa DC ni heshima kubwa, hivyo wengi wanatamani uteuzi ili kupata heshima, ukubwa, na maslahi ya u DC, naomba nisimtaje mshahara wa ma DC humu nikaonekana nawavunjia watu heshima!, lakini kuna akina sisi watu wa type ya kozi mwana mandanda kulala njaa kupenda, ni masikini jeuri!, kwetu u DC sio dili!, hiyo mishahara ya ma DC tunawalipa ma DC 3, RC 2 na Mkurugenzi 1 kwa kodi yetu!.
P
Si kweli, unautamani usiku na mchana!
 
Salaam Wakuu,

Japheth Maganga aliyetuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera akataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya alioteuliwa na Rais Samia hivi karibuni.

Japhet kasema, baada ya Kushauriana na Familia yake, alimuandikia rais Samia kumshukuru kwa kumteua pia na kumuomba atengue uteuzi wake na achaguliwe mtu Mwingine.

Wateule wengine ambao wamekataa uteuzi ni:

Leah Ulaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mkoa wa Geita na na Dina Mathamani aliyeteuliwa kwenda Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma

Wote waliokataa Uteuzi wa Rais Samia ni Viongozi wa juu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Leah Ulaya ni rais wa CWT, Dinah Mathamani ni Makamu wa Rais wa CWT huku Japheth Maganga akiwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)

======

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japheth Maganga ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ameshiriki kuongoza mkutano wa viongozi wa chama hicho jijini Tanga huku akisema kwa sasa hawezi kueleza kwanini hajaripoti katika wilaya aliyopangiwa ya Kyerwa, mkoani Kagera.

Vilevile, Maganga alihojiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga zaidi ya dakika 50 lakini si yeye wala wanausalama hao walioweka wazi sababu za mahojiano hayo.

Maganga na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa wiki iliyopita na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wakuu wa wilaya lakini wakati wenzao wakiapishwa kwenye maeneo yao leo Jumatatu, Januari 30, 2023 wao wapo Tanga wakiongoza mkutano wa viongozi wakuu wa CWT.

Ulaya aliteuliwa kuwa DC wa Mbogwe, Mkoa wa Geita ambapo wenzake wanaapishwa leo Jumatatu na Mkuu wa Mkoa huo, Martin Shigela.

Mara baada ya kumaliza kuhojiwa na polisi kuanzia saa 4:36 hadi saa 5:24 asubuhi nje ya ukumbi wa mkutano huo unaofanyikia katika Hoteli ya Regal Naivera, Mtaa wa Bombo jijini Tanga Maganga alirejea ukumbini na baadaye kidogo alitoka nje.

Nje ya ukumbi ambapo Mwananchi Digital limeweka kambi, Magamba amesema, “kwa sasa nimeziba mdomo labda usubiri tutakapomaliza kikao ndipo nitazungumza kuhusu nafasi ya U-DC na CWT."

Wakati Maganga akisema hayo, Rais wa CWT hakutoka ndani ya ukumbi wa mkutano huo huku maofisa wa CWT wakisema hajaruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.

Kitendo cha viongozi wakuu hao wa CWT kuonekana Tanga wakati wenzao wakiapishwa kimezua mjadala mitandaoni na kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba wameomba wateuliwe wengine kwenye nafasi hizo za U-DC ili kuwawezesha kuendelea na majukumu yao katika chama cha walimu.

Chanzo: DC mteule ahojiwa na polisi dakika 50, Rais CWT…
Mh
 
KATIBU CWT ACHARUKA - "MNATOA KIPAUMBELE UJENZI WA MADARASA MNASAHAU NYUMBA ZA WALIMU


CWT kinaomba yafuatayo yakatiliwa mkazo - Maslahi ya waalimu mfano Increment / nyongeza ya mishahara, posho ya muda wa ziada kwani darasa lina wanafunzi 100 ambalo lilitakiwa darasa kuwa na waalimu wawili kwa idadi hiyo ya wanafunzi darasani, teaching allowance na nyumba za walimu zikijengwa basi waalimu watafanya kazi vizuri zaidi anamalizia Katibu wa CWT wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma
 
Back
Top Bottom