Kwani mh rais hakuwasiliana nao kabla ya kuwatangaza. Au rais anaweza kunitangaza kuwa kuanzia sasa Stonecutter ni mkuu wa wilaya flani pasipo kunitaarifu mimi niridhie au nimkatalie kabla ya kulitangaza kwa umma, jambo ambalo halitaleta fedheha na kumvunjia heshima mkuu wa watu. Na kama alitangaza tu na wateuliwa wakaskia kwa mara ya kwanza kwenye media, basi ni haki yao kuamua waliyoyaamua. Lakini kwa wateule wote wanaotoka cwt kukataa, inaleta viulizo kwenye uhusiano kt ya serikali na chama cha walimu.