Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Ndo madhala ya kuteua watu wenye ma vitengo yao tayari ya kupiga fedha (MICHANGO ya walimu nchi nzima) .
Kwani yeye ndo anafaa kuliko vijana wengine. Mtu mmoja anacover sehemu mbili as if nchi ina underpopulation ya skilled people. NDO maana watu wanataka kuchagua upinzani sio kwamba wao ni wema watatutendea mema la hasha tunataka kubadili walaji wa mali za nchi hii Kupitia KOFIA ya siasa
Usikariri.

Uteuzi ni kama JOB OFFER,

Unaweza kukataa.

Ally Miswanya alimkatalia JOM pia.

PUNGUZENI UCHAWA
 
Hii nafasi angeonjeshwa ELIA WILINASI tuone kama ataikataa.
 
UTOVU WA NIDHAMU!

NANI AIJUAYE KESHO!!?

UKUU WA WILAYA NI FURSA YA KUPATA UWANJA WA KUONYESHA LEADERSHIP SKILLS!!!

MSHAHARA MKUBWA NA POSHO KUBWA SIO KILA KITU WAKUU!

CV,CONNECTION AND INTERACTON WITH V.I.PS OF THE STATE MATTERS MOST!

HUWEZI UKAWA MTUMISHI WA UMMA UKAGOMEA UTEUZI TOKA KWA NAMBA MOJA KISA MISHAHARA NA MARUPU RUPU LABDA KAMA ANGEKUWA KWENYE KAMPUNI AU PRIVATE SECTORS!!

WAMEONYESHA ULIMBUKENI NA USHAMBA PIA!
Tulia mwl tutafute michango yako acha wivu
 
Natoa angalizo kwa Mamlaka za Ulinzi na usalama za Tanzania kuhakikisha kwamba , watu watatu waliokataa teuzi za Ukuu wa Wilaya wanalindwa, tusisikie kwamba wamepotea ama wametekwa.

Kukataa uteuzi ni haki ya kikatiba na pia ni fursa ya kuteua watu wengine, hivyo waliokataa teuzi hizo wasichukuliwe kama Maadui wa Taifa.

Waacheni wafanye kazi wanazozitaka
 
kuyaondoa haya ni mpaka katiba mpya
mi nawashangaa mnaoimba katiba mpya !

hivi katiba ni kiumbe kwamba isipotekelezwa itasema ?

mbona sheria zetu ni nzuri sana ila raia bado tu tunapata tabu sana ?

katiba mpya ni makaratasi tu ila msoto utakua pale pale
 
Salaam Wakuu,

Japheth Maganga aliyetuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera akataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya alioteuliwa na Rais Samia hivi karibuni.

Japhet kasema, baada ya Kushauriana na Familia yake, alimuandikia rais Samia kumshukuru kwa kumteua pia na kumuomba atengue uteuzi wake na achaguliwe mtu Mwingine.

Wateule wengine ambao wamekataa uteuzi ni:

Leah Ulaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mkoa wa Geita na na Dina Mathamani aliyeteuliwa kwenda Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma

Wote waliokataa Uteuzi wa Rais Samia ni Viongozi wa juu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Leah Ulaya ni rais wa CWT, Dinah Mathamani ni Makamu wa Rais wa CWT huku Japheth Maganga akiwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)

======

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japheth Maganga ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ameshiriki kuongoza mkutano wa viongozi wa chama hicho jijini Tanga huku akisema kwa sasa hawezi kueleza kwanini hajaripoti katika wilaya aliyopangiwa ya Kyerwa, mkoani Kagera.

Vilevile, Maganga alihojiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga zaidi ya dakika 50 lakini si yeye wala wanausalama hao walioweka wazi sababu za mahojiano hayo.

Maganga na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa wiki iliyopita na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wakuu wa wilaya lakini wakati wenzao wakiapishwa kwenye maeneo yao leo Jumatatu, Januari 30, 2023 wao wapo Tanga wakiongoza mkutano wa viongozi wakuu wa CWT.

Ulaya aliteuliwa kuwa DC wa Mbogwe, Mkoa wa Geita ambapo wenzake wanaapishwa leo Jumatatu na Mkuu wa Mkoa huo, Martin Shigela.

Mara baada ya kumaliza kuhojiwa na polisi kuanzia saa 4:36 hadi saa 5:24 asubuhi nje ya ukumbi wa mkutano huo unaofanyikia katika Hoteli ya Regal Naivera, Mtaa wa Bombo jijini Tanga Maganga alirejea ukumbini na baadaye kidogo alitoka nje.

Nje ya ukumbi ambapo Mwananchi Digital limeweka kambi, Magamba amesema, “kwa sasa nimeziba mdomo labda usubiri tutakapomaliza kikao ndipo nitazungumza kuhusu nafasi ya U-DC na CWT."

Wakati Maganga akisema hayo, Rais wa CWT hakutoka ndani ya ukumbi wa mkutano huo huku maofisa wa CWT wakisema hajaruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.

Kitendo cha viongozi wakuu hao wa CWT kuonekana Tanga wakati wenzao wakiapishwa kimezua mjadala mitandaoni na kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba wameomba wateuliwe wengine kwenye nafasi hizo za U-DC ili kuwawezesha kuendelea na majukumu yao katika chama cha walimu.

Chanzo: DC mteule ahojiwa na polisi dakika 50, Rais CWT…
Cwt 😅😅😅😅
 
Kukataa kazi ya Rais unayopewa bila ya kuomba wala kuihitaji ni nusu ya Uhaini Tanzania
 
Katib
mi nawashangaa mnaoimba katiba mpya !

hivi katiba ni kiumbe kwamba isipotekelezwa itasema ?

mbona sheria zetuni nzuri sana ila raia bado tu
KAtiba mpya ndio mwarobaini kama unaikataa basi wewe Chawa
 
Nadhani inabidi ujitafakari sana kukubali kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya, kwa sababu inabidi ujitoe kabisa kwenye profession yako na kujiondoa uwezo wa kufikiri ili uweze kwenda sambamba na makada wa chama. Ukijifanya intellectual utagombana nao kila siku, hasa unapokuta mtu wa darasa la saba na ndio anakupa maagizo wakati wewe una degree zako nne!

Hayo mambo ni kuwaachia watu wa aina ya kina Hapi na Muro.

Halafu Samia aache tabia ya kuteua watu kabla ya kuwauliza kwanza, ataumbuka sana. Nyerere akitaka kukuteua alikuwa anakuuliza kwanza, utaweza? Ukisema siwezi anakuacha. Ndio maana Malecela alipoulizwa ataweza kuwa PM, akasema ndio, akafanya sherehe kabla ya kutangazwa rasmi, alitemwa.
Cwt imejaa makada. Ndio maana haina tija
 
Salaam Wakuu,

Japheth Maganga aliyetuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera akataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya alioteuliwa na Rais Samia hivi karibuni.

Japhet kasema, baada ya Kushauriana na Familia yake, alimuandikia rais Samia kumshukuru kwa kumteua pia na kumuomba atengue uteuzi wake na achaguliwe mtu Mwingine.

Wateule wengine ambao wamekataa uteuzi ni:

Leah Ulaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mkoa wa Geita na na Dina Mathamani aliyeteuliwa kwenda Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma

Wote waliokataa Uteuzi wa Rais Samia ni Viongozi wa juu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Leah Ulaya ni rais wa CWT, Dinah Mathamani ni Makamu wa Rais wa CWT huku Japheth Maganga akiwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)

======

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japheth Maganga ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ameshiriki kuongoza mkutano wa viongozi wa chama hicho jijini Tanga huku akisema kwa sasa hawezi kueleza kwanini hajaripoti katika wilaya aliyopangiwa ya Kyerwa, mkoani Kagera.

Vilevile, Maganga alihojiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga zaidi ya dakika 50 lakini si yeye wala wanausalama hao walioweka wazi sababu za mahojiano hayo.

Maganga na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa wiki iliyopita na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wakuu wa wilaya lakini wakati wenzao wakiapishwa kwenye maeneo yao leo Jumatatu, Januari 30, 2023 wao wapo Tanga wakiongoza mkutano wa viongozi wakuu wa CWT.

Ulaya aliteuliwa kuwa DC wa Mbogwe, Mkoa wa Geita ambapo wenzake wanaapishwa leo Jumatatu na Mkuu wa Mkoa huo, Martin Shigela.

Mara baada ya kumaliza kuhojiwa na polisi kuanzia saa 4:36 hadi saa 5:24 asubuhi nje ya ukumbi wa mkutano huo unaofanyikia katika Hoteli ya Regal Naivera, Mtaa wa Bombo jijini Tanga Maganga alirejea ukumbini na baadaye kidogo alitoka nje.

Nje ya ukumbi ambapo Mwananchi Digital limeweka kambi, Magamba amesema, “kwa sasa nimeziba mdomo labda usubiri tutakapomaliza kikao ndipo nitazungumza kuhusu nafasi ya U-DC na CWT."

Wakati Maganga akisema hayo, Rais wa CWT hakutoka ndani ya ukumbi wa mkutano huo huku maofisa wa CWT wakisema hajaruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.

Kitendo cha viongozi wakuu hao wa CWT kuonekana Tanga wakati wenzao wakiapishwa kimezua mjadala mitandaoni na kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba wameomba wateuliwe wengine kwenye nafasi hizo za U-DC ili kuwawezesha kuendelea na majukumu yao katika chama cha walimu.

Chanzo: DC mteule ahojiwa na polisi dakika 50, Rais CWT…
Walioteuliwa Kindondoni na Ilala hawajagomea?
 
Back
Top Bottom