Watawala wa Tanzania, labda siku moja mtapenda mpewe haki ya kusikilizwa Mahakamani pia!

Watawala wa Tanzania, labda siku moja mtapenda mpewe haki ya kusikilizwa Mahakamani pia!

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,583
Reaction score
27,838
Walioweka mfumo wa Mihimili 3 yaani Serikali, Mahakama na Bunge hawakuwa wajinga, walijua wanafanya nini na walikuwa na nguvu za Umungu lkn bado waliona umuhimu wa kuwa na Mahakama na Sheria kwamba kila Binadamu ana haki ya kusikilizwa na ndo maana hata wauwaji wanafikishwa Mahakamani na kusikilizwa na siyo kuuliwa papo kwa papo kwa kuwa tu wameuwa.

Leo hii mnajiona mna nguvu na kuhukumu Watanzania bila ya kuwapa haki yao ya msingi ya kuwasilikiza kwa kuwachapa viboko hadharani,mnajisahau! Kesho na kesho kutwa mambo yanaweza kubadilika, na amini nawaambia mtaomba kupewa haki ya kusikilizwa pia na siyo kuadhibiwa papo kwa papo kama mnavyowafanyia Watanzania.

Mfano mzuri ni Rais wa zamani wa Ufaransa Nikolas Sarkozy, alikuwa powerful man zaidi yenu. Raisi wa powerful country leo hii amefikishwa Mahakamani kwa makosa aliyoyatenda alipokuwa madarakani na anapewa fair trial Mahakamani. Mnanajua ni kwanini? Ni kwa sababu hata yeye alipokuwa Rais wa nchi hakuchapa watu viboko hovyo bali aliruhusu yeyote aliyefanya kosa apewe haki ya kusikilizwa na kufikishwa Mahamani.

Sina nia ya kumtisha yeyote, ila haya maisha huwezi jua nini kitatokea kesho.

Rais Magufuli kama unaruhusu Watanzania kuchapwa viboko hadharani bila ya kuwafikisha Mahakamani unapandikiza chuki kwa Wananchi dhidi yako na hiyo siyo akili ukiwa kama Kiongozi mwenye Madaraka makubwa. Siku moja watataka revenge na utahitaji Mahakama kukusikiliza amini nawambia.

Wapeni Watanzania haki ya kusikilizwa Mahakamani, kwani hata ninyi mnaweza kuja kuihitaji pia.
 
Tanzania ya leo!😬😬😬
5532890.jpg
 
...Rais Magufuli kama unaruhusu Watanzania kuchapwa viboko hadharani bila ya kuwafikisha Mahakamani unapandikiza chuki kwa Wananchi dhidi yako na hiyo siyo akili ukiwa kama Kiongozi mwenye Madaraka makubwa. Siku moja watataka revenge na utahitaji Mahakama kukusikiliza amini nawambia.
... hashtakiki popote akiwa na baada ya kutoka madarakani; hana hofu yoyote na wala hapaswi kuwa nayo maana sisi wananchi kwa umoja wetu tumetunga Katiba ya kumlinda kipenzi chetu na madhila yoyote yale wakati wowote ule!

Actually, tumemwomba sana Mungu na amekubali Katiba yetu haiwezi kubadilishwa kwa sababu yoyote ile maana amemtuma Gabrieli ahudumuye mbele ya Kiti cha Enzi aisilibe kwa mihuri ya moto toka Juu ili iwe agano la milele kati Mungu na watanzania. Asomaye na afahamu.
 
Taratibu mmeanza kuelewa nyie wapiga debe wa jiwe na utawala wake, tulikuwa tunawaambia kipindi kile utawala wa huyu mtu una matatizo mengi hamkuwa mnatuelewa mkaona kam haya yatatukuta sisi tu mkadhani nyie mpo salama lakini sasa naona ufahamu unaanza kuwarudi nina hakika siku moja tutaimba wote wimbo mmoja.

Sasa mpaka muda huu hakuna aliekemea kitendo hicho ambacho sio mara ya kwanza kufanywa na hawa wakuu wa wilaya na mwingine ashawahi kuwachapa viboko waalimu kule mkoani Kagera na yeye sasa ni top leader kwa hiyo tutegemee matukio kama haya kutokea zaidi, na sasa ni viboko ila ipo siku itakuwa ni adhabu kali zaidi.
 
... hastakiki popote akiwa na baada ya kutoka madarakani; hana hofu yoyote na wala hapaswi kuwa nayo maana sisi wananchi kwa umoja wetu tumetunga Katiba ya kumlinda kipenzi chetu na madhila yoyote yale wakati wowote ule!..
Uzuri wote kama sii wengi waliopitisha mabadiliko hayo , wajumbe wamepita nao, hivyo wote ni damu mpya na hata kujua walichofanya wenzao kimeacha shida nyingi, huenda hawana habari na hawatakaa wawe nayo. Na walio nje ya mfumo hawana ujanja Tena wa kufanya chochote hata kama wakitambua walikosea.
 
Umeanza kuuona ukweli ukiwa umechelewa. Unaanza kuukemea uovu uliokuwa unatetea muda wote. Ulichokuwa unakutetea ukiwa kwenye maslahi, ndio hicho hicho kinachofanyika sasa baada ya maslahi yako kupotea.
 
Back
Top Bottom