Samahani ndugu, una ushahidi na unachoongea...? ni maneno ya Tweeter?Huyu mzee naye huwa simwelewi hata kidogo ndiyo maana anapambana kupaka nywele rangi aonekane ni kijana maana ndiyo akili yake imeishia hapo kwa vidosho, watu wanapakua mabilioni akina Lugola, Makonda, Sabaya, Mnyeti n.k lakini ndiyo kwanza anacheka nao.
Na mie pia, naona ka simuelewagi.Huu ni upuuzi tu, unless mwandishi kakosea. Sina hakika kama ni kazi ya Mkaguzi Mkuu kufanya kazi ya Pre-Audit. My understanding pre-audit inafanyika kabla malipo hayajafanyika.
Hii ni kazi ya Mweka Hazina/ Accountant. Lingekuwa ni tukio la mwaka uliopita ambao tayari Mkaguzi ameufanyia kazi, basi ningemuelewa Majaliwa.
Napataga shida kumuelewa huyu bwana.
Yaani mahela yote hayo yamechotwa!!! Msiwe mnatuambia maana nahisi kuzimia ukizingatia kijimshahara kangu ka mwezi May kameshakataWaziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Fedha. Amefanya hivyo ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya Fedha za Umma.
Ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, ACP Salum Hamdun kufanya uchunguzi. Tuhuma mojawapo inayokabili ni malipo ya Milioni 251 yaliyofanyika Machi 31, 2021 yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi na waliohusika.
======
Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi mkaguzi mkuu, mkaguzi msaidizi na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazowakabili.
Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu iliyotolewa leo Mei 28, 2021 inaeleza kuwa katika kikao kazi na waziri wa fedha na mipango, katibu mkuu, manaibu katibu wakuu na watendaji waandamizi wa wizara hiyo mkoani Dodoma jana, Majaliwa amemuagiza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika si za kweli wahusika warejeshwe kazini.
Majaliwa amezitaja tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31, 2021 kupitia vocha 30 ya Sh251 milioni yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi maalum ni nini na nani aliifanya.
Amebainisha kuwa siku hiyo hiyo pia zililipwa Sh198.8 milioni kwa madai kuwa ni posho ya honoraria.
Mtendaji mkuu huyo wa Serikali amesema Aprili 8, 2021 watumishi 27 wa wizara hiyo walilipwa Sh44.5 milioni za posho ya kazi maalum ya wiki nne na Aprili 13, 2021 zililipwa Sh155.2 milioni kwa watumishi 68 ikiwa ni posho ya kazi maalum ya wiki tatu.
Pia Aprili 30, 2021 zililipwa Sh43.9 milioni kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira na siku hiyohiyo zililipwa Sh14.4 milioni kwa ajili ya siku ya wanawake.
Inaeleza kuwa fedha nyingine Sh43 milioni zililipwa siku hiyo na kufanya jumla ya malipo yaliyolipwa siku hiyo kuwa Sh101.8.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa Meimosi, 2021 zililipwa Sh184.1 milioni na mchana wa siku hiyo zikalipwa Sh264 milioni zikiwa ni malipo ya kazi maalum.
"Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho,” amesema Majaliwa.
Inabainisha kuwa Mei 3, 2021 zililipwa Sh146.5 milioni kwa watumishi 125 zikiwa ni malipo ya kuandaa mpango kazi wa manunuzi kazi ambayo ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku na siku hiyohiyo zililipwa Sh171.2 milioni kwa ajili ya kuandaa nyaraka za Bunge.
Taarifa hiyo imemnukuu Majaliwa akisema Sh155 milioni zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi.
"Yaani hii kazi ya ukaguzi inalipwa kwenye maeneo manne, huu ni utaratibu wa wapi? Mnazidi kutupunguzia imani, na sijaongelea eneo la kuhamisha mafungu na utaratibu kuhamisha fedha kisha mnakwenda kuzichukua huko mlikozihamishia,” amesisitiza Majaliwa.
Amewataka watendaji wa wizara hiyo kujenga uaminifu kwa wanaokusanya mapato kwa kufanya kazi kwa uaminifu na kuwatahadharisha kuwa watakaoendekea kucheza na fedha za umma hatua kali zitachukuliwa dhidi yao huku akiwapongeza wafanyakazi wenye weledi.
Chanzo: Mwananchi
Tanzania Ni TajiriTanzania Ni Tajiri
! Yaani siku 14 baada ya JPM kututoka?
Takukuru walirudisha mpira kwa CAG!Pengine hakuna ushahidi. Mwisho wake atapewa kazi nyingine.
Said Lugumimnaonea dagaa.
Na tukubaliane pesa yote inayopigwa huko Serekalini,na pesa zote za biashara haramu zote zitumike hapahapa Nchini ili zije kiurahisi mtaani! Hakuna Mtu kuzipeleka pesa zetu Ughaibuni!!Tanzania yetu inarudi; pesa zitakuwa nyingi sana mitaani tena na kila mtu atafurahi.
Kuna office zingine ukiwa mfanyakazi,posho siyo tatizo,mradi ujuwe jinsi ya kujenga hoja ya kuzichomoa tu!!Kwa hiyo hapo wizara ya fedha ni mwendo wa kulipana posho tu daily, watumishi kwenye wizara nyingine kama elimu mtumishi anaweza kutoboa mwaka bila kuiona posho, kumbe mafungu ya kulipana posho yamebakizwa wizara ya fedha....ama kweli.
Lini?Takukuru walirudisha mpira kwa CAG!
Jiwe alimpiga roba kali, kila kitu alikuwa anataka aonekane yeye, Waziri Mkuu alikuwa hana meno kabisa, alikuwa kila akitaka kugusa mahali anakutana na watu pendwa wa Jiwe, inabidi arudi nyuma. Now Mama kamwachia uwanja ajimwage atakavyo, wakati yeye anadili zaidi na mambo makubwa makubwa. Jiwe bwana, hadi madarasa na vyoo alikuwa anataka azindue yeye, alikuwa anafuatilia hadi nani kamtongoza nani kwenye ofisi mbalimbali, very stupid presidentVery smart prime minister.
Ila kuwa Makini mzee maana imani ya Watanzania imeelekezwa zaidi kwako sasa,Japo Kundi la mafisadi,watumishi wazembe na wezi wa mali za umma bado linakuona wewe ni kikwazo kwao
Hii kesi Majaliwa anaangukia puaHuyu naye anatafuta kumfuata mwendazake, Ndugai anachezea pesa za umma kwa wabunge fake na kutwa yupo naye lakini yupo kimya.
Babati, ofisi ya bunge haiwezi kuingiliwa na Majaliwa ndg yanguHuyu naye anatafuta kumfuata mwendazake, Ndugai anachezea pesa za umma kwa wabunge fake na kutwa yupo naye lakini yupo kimya.
Huna habari bwashee?Lini?
Baeleze ukweli mama!Niliwahi kuleta uzi hapa kwamba wapigaji tumerudi mjini tokea tarehe 18 march 2021 uzi ukafutwa.
JPM alikua kiboko.. yeye ndio alikua sheria.
Ila kwa kutumia sheria zetu hizi huwezi epuka upigaji.
Kwani Approval zipoje huko serikalini, fedha inatokaje bila signature ya katibu mkuu wa wizara husika au waziri?
Mwigulu atwambie kama kweli hakua na taarifa.. au na yeye yumo kwenye mamho haya.
Tanzania Ni TajiriHuna habari bwashee?
Takukuru walimchunguza Kakoko kwa 98% wakarudisha mpira kwa CAG amalizie hiyo 2%
Hivi JPM alikutenda nini? Kila siku ni kumpalamikia kama msimbeJiwe alimpiga roba kali, kila kitu alikuwa anataka aonekane yeye, Waziri Mkuu alikuwa hana meno kabisa, alikuwa kila akitaka kugusa mahali anakutana na watu pendwa wa Jiwe, inabidi arudi nyuma. Now Mama kamwachia uwanja ajimwage atakavyo, wakati yeye anadili zaidi na mambo makubwa makubwa. Jiwe bwana, hadi madarasa na vyoo alikuwa anataka azindue yeye, alikuwa anafuatilia hadi nani kamtongoza nani kwenye ofisi mbalimbali, very stupid president
Mkaguzi Mkuu wa Wizara ya Fedha ni dagaa? Yeye ndiye atajua vya kujibu maana sheria zote za matumizi ya fedha za serikali anazijua.mnaonea dagaa.