Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Kwakweli ndiyo maana watu wamepoteza imani na serikali, wamepoteza morali ya kazi wamepoteza hata nia ya kuendelea kulipa kodi kumbe kuna genge la watu wanajinufaisha na fedha za umma
 
Kodi inakusanywa kutoka kwa WALALAHOI halafu hela inalambwa tu......

Vyema UCHUNGUZI uje na majibu kuwa si kweli na waendelee na majukumu yao!!

#KaziInaendelea
 
Mkuu usemacho ni kweli ila hapo chini kumeongezwa neno "na baadhi ya watendaji ....".
 
Wazee wetu WASTAAFU Wanateseka kusogeza Mafao yao Wengine Wanajilipa Pesa
 
Hayo ndiyo matokeo ya kumhamisha katibu mkuu wa fedha, Bw. Dotto, aliyekuwa ameidhibiti vizuri wizara hiyo. Katibu mkuu wa sasa ndiye anatakiwa kutumbuliwa. Hizo pesa hazingeweza kuwa zinachotwa ovyo ovyo bila idhini yake.
 
Matumizi yale yalikuwa ya nini? Online payment yes...nani aliruhu na kwanini?
 
Kwakweli ndiyo maana watu wamepoteza imani na serikali, wamepoteza morali ya kazi wamepoteza hata nia ya kuendelea kulipa kodi kumbe kuna genge la watu wanajinufaisha na fedha za umma
Watetezi wao wapo hapa JF, angalia uzi unavyochangiwa....ama kweli JPM uliondolea wakati taifa bado linakuhitaji Sana, nasikia makusanyo huko TRA ni kichefuchefu....
Dawa hospital mtaniambia kufika julai hali itakuwaje.
SSH apewe mikumi!
 
Kwa kweli haijakaa sawa. Accounting Officer aka Afisa Masululi (mwenye vote) ni katibu mkuu wa wizara hiyo ambaye pia anaitwa Mlipaji Mkuu. Pesa ye yote haiwezi kulipwa bila idhini ya Afisa masululi. Mkaguzi mkuu wa ndani si mlipaji na wala hawezi kumzuia afisa masululi kufanya malipo. Kazi yake ni kushauri tu na ushauri wake si lazima ufuatwe.

Hivyo wakuwajibishwa na ubadhirifu huo ni katibu mkuu pamoja na mhasibu mkuu wake. Mkaguzi mkuu wa ndani yeye ni shahidi wa ubadhirifu huo. Of course mwenye mamlaka ya kumwajibisha katibu mkuu si waziri mkuu bali ni rais wa JMT. Waziri mkuu saizi yake ni Mhasibu mkuu - huyu ndiye angaliondoka naye na kumuachia rais kushughulika na katibu mkuu wake. Hao watendaji wengine wadogo wadogo ni kuwaonea tu maana wao wanatekeleza kilichoidhinishwa na hao mabosi wao ie katibu mkuu na mhasibu mkuu.

Ni vizuri sasa Mama akapunguza muda wa kukaa DSM akifanya diplomasia na kukaa zaidi Dom akifanya uendeshaji (executive duties) wa serikali.
 
Kosa la jinai lina mwisho?
 
Hivi JPM alikutenda nini? Kila siku ni kumpalamikia kama msimbe
Utawala wake wa hovyo umenisababishia majanga mengi sana, mojawapo kuondoka Tz bila hata ya kupenda, hali iliyosababisha mambo yangu mengi kusimama huko nyumbani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…