Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Wasalaam wanajamiiForums!

Kwanza kabisa naomba nitoe masikitiko yangu makubwa sana kuhusu upigwaji holela wa pesa za umma kienyeji kiasi hiki. Huu ni sawa na uuaji kabisa usiovumilika hata kidogo. Ninampa pole sana Mama yangu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Nitashangaa sana kuona Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba mpaka muda huu yupo kazini wakati wizara yake imechafuka kiasi hiki. Yaani mpaka Waziri mkuu anagundua uchafu huu waziri ulikua umelala wapi? Haiwezekani waziri upo pesa za walipa kodi zinaliwa kiasi hicho na wewe upo huenda unajua au hujui kabisa kinachoendelea, maana yake wewe hujui upo ofisini unafanya nini, yaani upo sawa na wabunge wasiokua na vyeo.

Toka awali tulisema kabisa kua Dkt Mwigulu si mtendaji ni mwanasiasa wa kelele za majukwaani, huwezi kupewa wizara nyeti kama hii Madudu yote yanatokea mikononi mwako mchana kweupe wewe upo usingizi wa pono. Kama mwananchi mwenye haki ya kutoa maoni na kuhoji, nakuomba ujiuzulu mapema tu kulinda heshima yako, walishe watu wenye weledi wafanye kazi zao.

Chande chonde Mhe Rais tumbua huyu mtu au hamisha mpeleke mazingira kule, tuletee waziri smart atakayeweza kufuatilia yote yansyotendeka ndani ya wizara. Tuna vijana watendaji na waaminifu wasioweza kutafuna pesa ya mtu wape kazi Mama achana na Mwanasiasa huyu atakupotezea malengo yako. Ningeomba ikiwezekana kabisa Mteuea hata Prof Assad CAG Mstaafu mpe ubunge wa kuteuliwa katika nafasi 2 za Rais zilizobakua kisha mpe kazi ya kusimamia Wizara hii. Ikishindikana Mhamishie Waziri Ummy Mwalimu kwenye wizara yako, huyu ni kiboko ya mafisadi.

Mwigulu anawaza Urais 2021 angebakia kua mbunge wa kawaida tu ili afanye maandalizi yake vizuri, kazi za serikali hataweza. Mama usipoteze muda katika hili fanyika kazi kwa haraka, taifa linahitaji pesa sana kwa sasa halafu zinachezewa.

Nimemaliza, sina chuki binafsi na ndugu Mwigulu Nchemba na ni rafiki yangu wa karibu lakini Maslahi ya taifa ndio kubwa kuliko ukaribu wangu na Waziri.

Zaidi, soma: Wizi Mkubwa wafanyika Wizara ya Fedha na Mipango, Waziri Mkuu Majaliwa asimamisha wakaguzi kupisha Uchunguzi
 
Sasa wawili tu. Hapi hatuhitaji uchunguzi ni kuanzia KM na watendaji wote sasa wangekuwa Isanga prison!
 
Huyu kama Rais hatamtumbua basi tutegemee utendaji mbovu zaidi. Hapa waziri ni mzembe kupita kiasi
 
Kipi kilichofanywa na Ummy hadi useme ni kiboko ya mafisadi?
 
Hikubariki na haitakubarika watumishi wa umma ambao wanalipwa mishahara wajilipe posho milioni 400 siku moja!

Huu ni wizi wa mchana kweupe!

Mama yetu mpendwa anza na hawa nyani vinginevyo tutavuna mabua. Usiwahurumie hata kidogo. Kwa kuwa wao hawana huduma na kodi zetu,tengua viuno wote,including waziri wao kama hatachukua jukumu la kujiuzulu mwenyewe.
 
Mama asicheke na mbwa yoyote, wananchi tupo na yeye. CP Salum Hamduni na yeye asituangushe tupo na yeye pia, azae na hao kina Ole Sabaaya na matapeli wenzake.
 
Hikubariki na haitakubarika watumishi wa umma ambao wanalipwa mishahara wajilipe posho milioni 400 siku moja!

Huu ni wizi wa mchana kweupe!

Mama yetu mpendwa anza na hawa nyani vinginevyo tutavuna mabua. Usiwahurumie hata kidogo. Kwa kuwa wao hawana huduma na kodi zetu,tengua viuno wote,including waziri wao kama hatachukua jukumu la kujiuzulu mwenyewe.
 
Kina nani hao mbona huwataji?
 
Anza na wabunge kwanza wana mishahara minono 12M per moon lakini bado wanalipwa 340000 kwa siku
 
Nimesikiliza huko unaweza kumpiga mtu ngumi, watu wanaiba hatari kwa kweli hakuna uchunguzi halafu unafukuzwa kazi hapana unafilisiwa rudisha pesa zote na interest juu halafu mahakamani unahukumiwa hii ndio funzo, halafu nauliza kweli nani ana sign hizi voucher ni rahisi hivi pesa kuibiwa namna hii? maswali mengi kuliko majibu.
 
Uzi wako haujakamilika, weka habari iliyotosheleza nyama na ugali.
Tuambie ni kina nani wamejilipa milioni 400?
Lini wamejilipa kiasi hicho?
Kwanini wamejilipa kiasi hicho?
Je, sheria inasemaje kuhusu watumishi kujilipa posho?
Na utuambie source ya habari yako ni ipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…