Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Halafu naye anasema ana PhD ya Uchumi kama Mwendazake aliyekuwa anadai ana PhD ya Chemistry.

Kwa kweli utoaji PhD wa UDSM unatia mashaka makubwa sana ukiangalia hawa watunikiwa wawili Magufuli na Mwigulu
Unaandika utopolo Dkt Mwigulu amekaa muda gan paleee???this is utter nonsense unayoongea
 
Wasalaam wanajamii forum!

Kwanza kabisa naomba nitoe masikitiko yangu makubwa sana kuhusu upigwaji holela wa pesa za umma kienyeji kiasi hiki. Huu ni sawa na uuaji kabisa usiovumilika hata kidogo. Ninampa pole sana Mama yangu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Nitashangaa sana kuona Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba mpaka muda huu yupo kazini wakati wizara yake imechafuka kiasi hiki. Yaani mpaka Waziri mkuu anagundua uchafu huu waziri ulikua umelala wapi? Haiwezekani waziri upo pesa za walipa kodi zinaliwa kiasi hicho na wewe upo huenda unajua au hujui kabisa kinachoendelea, maana yake wewe hujui upo ofisini unafanya nini, yaani upo sawa na wabunge wasiokua na vyeo.

Toka awali tulisema kabisa kua Dkt Mwigulu si mtendaji ni mwanasiasa wa kelele za majukwaani, huwezi kupewa wizara nyeti kama hii Madudu yote yanatokea mikononi mwako mchana kweupe wewe upo usingizi wa pono. Kama mwananchi mwenye haki ya kutoa maoni na kuhoji, nakuomba ujiuzulu mapema tu kulinda heshima yako, walishe watu wenye weledi wafanye kazi zao.

Chande chonde Mhe Rais tumbua huyu mtu au hamisha mpeleke mazingira kule, tuletee waziri smart atakayeweza kufuatilia yote yansyotendeka ndani ya wizara. Tuna vijana watendaji na waaminifu wasioweza kutafuna pesa ya mtu wape kazi Mama achana na Mwanasiasa huyu atakupotezea malengo yako. Ningeomba ikiwezekana kabisa Mteuea hata Prof Assad CAG Mstaafu mpe ubunge wa kuteuliwa katika nafasi 2 za Rais zilizobakua kisha mpe kazi ya kusimamia Wizara hii. Ikishindikana Mhamishie Waziri Ummy Mwalimu kwenye wizara yako, huyu ni kiboko ya mafisadi.

Mwigulu anawaza Urais 2021 angebakia kua mbunge wa kawaida tu ili afanye maandalizi yake vizuri, kazi za serikali hataweza. Mama usipoteze muda katika hili fanyika kazi kwa haraka, taifa linahitaji pesa sana kwa sasa halafu zinachezewa.

Nimemaliza, sina chuki binafsi na ndugu Mwigulu Nchemba na ni rafiki yangu wa karibu lakini Maslahi ya taifa ndio kubwa kuliko ukaribu wangu na Waziri.
Khaaaa....🤣🤣

Maneno yanakutoka tu.....

Ingekuwa kuachia NGAZI ni jambo rahisi kihivyo basi hakuna KIONGOZI NA BOSI yeyote angesalia UONGOZINI kila "rafu" zinapochezwa CHINI YAKE....kwani ni NYINGI....ziko hadi katika MAKUSANYO YA NYUMBA ZA IBADA......

#KaziIendelee
 
Kuna nini,? fungukeni, kama kuna upigaji sehemu tujuzeni tupige kelele wote mpaka kieleweke acheni mafumbo na kuzunguka aitasaidia.
Umeuliza nami kabla sijauliza, mara paap, ndi-ndi! msg ya Whatsapp imeingia na hotuba ya majaliwa; P.M.
Sikiliza hiyo:
View attachment 1800330
 
Halafu naye anasema ana PhD ya Uchumi kama Mwendazake aliyekuwa anadai ana PhD ya Chemistry.

Kwa kweli utoaji PhD wa UDSM unatia mashaka makubwa sana ukiangalia hawa watunikiwa wawili Magufuli na Mwigulu
Nini kimetokea
 
Waziri Mkuu ameshalishughulikia kwa kuona TATIZO LILIKO...

PM hakusita kuiagiza TAKUKURU ifanyie kazi jambo hilo....

Leo kumtuhumu WAZIRI ambaye hata ROBO MWAKA hana ni KUMUONEA TU .....

NI KUMUONEA TU....

NI SIASA KOKO TU ....

#KaziIendelee
 
Hivi, ni mfumo upi wa kuhakikisha pesa ya umma haicheziwi??

Mbona Kila utawala unachemka??
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Fedha. Amefanya hivyo ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya Fedha za Umma.

Ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, ACP Salum Hamdun kufanya uchunguzi. Tuhuma mojawapo inayokabili ni malipo ya Milioni 251 yaliyofanyika Machi 31, 2021 yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi na waliohusika.

======

Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi mkaguzi mkuu, mkaguzi msaidizi na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazowakabili.

Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu iliyotolewa leo Mei 28, 2021 inaeleza kuwa katika kikao kazi na waziri wa fedha na mipango, katibu mkuu, manaibu katibu wakuu na watendaji waandamizi wa wizara hiyo mkoani Dodoma jana, Majaliwa amemuagiza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika si za kweli wahusika warejeshwe kazini.

Majaliwa amezitaja tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31, 2021 kupitia vocha 30 ya Sh251 milioni yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi maalum ni nini na nani aliifanya.

Amebainisha kuwa siku hiyo hiyo pia zililipwa Sh198.8 milioni kwa madai kuwa ni posho ya honoraria.

Mtendaji mkuu huyo wa Serikali amesema Aprili 8, 2021 watumishi 27 wa wizara hiyo walilipwa Sh44.5 milioni za posho ya kazi maalum ya wiki nne na Aprili 13, 2021 zililipwa Sh155.2 milioni kwa watumishi 68 ikiwa ni posho ya kazi maalum ya wiki tatu.

Pia Aprili 30, 2021 zililipwa Sh43.9 milioni kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira na siku hiyohiyo zililipwa Sh14.4 milioni kwa ajili ya siku ya wanawake.

Inaeleza kuwa fedha nyingine Sh43 milioni zililipwa siku hiyo na kufanya jumla ya malipo yaliyolipwa siku hiyo kuwa Sh101.8.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Meimosi, 2021 zililipwa Sh184.1 milioni na mchana wa siku hiyo zikalipwa Sh264 milioni zikiwa ni malipo ya kazi maalum.

"Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho,” amesema Majaliwa.

Inabainisha kuwa Mei 3, 2021 zililipwa Sh146.5 milioni kwa watumishi 125 zikiwa ni malipo ya kuandaa mpango kazi wa manunuzi kazi ambayo ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku na siku hiyohiyo zililipwa Sh171.2 milioni kwa ajili ya kuandaa nyaraka za Bunge.

Taarifa hiyo imemnukuu Majaliwa akisema Sh155 milioni zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi.

"Yaani hii kazi ya ukaguzi inalipwa kwenye maeneo manne, huu ni utaratibu wa wapi? Mnazidi kutupunguzia imani, na sijaongelea eneo la kuhamisha mafungu na utaratibu kuhamisha fedha kisha mnakwenda kuzichukua huko mlikozihamishia,” amesisitiza Majaliwa.

Amewataka watendaji wa wizara hiyo kujenga uaminifu kwa wanaokusanya mapato kwa kufanya kazi kwa uaminifu na kuwatahadharisha kuwa watakaoendekea kucheza na fedha za umma hatua kali zitachukuliwa dhidi yao huku akiwapongeza wafanyakazi wenye weledi.

Chanzo: Mwananchi
Kama waziri mkuu Kassim Majaliwa alikuwa hajui huu utaratibu basi inabidi ajitafakari sana. Huu ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa watumishi wa serikali kulipana posho kwa kazi nyingi za ofisini kama kuandika taarifa za mwezi na mwaka, kuandika hotuba za bajeti, kuandika taarifa mbalimbali za utendaji kazi zao nk.

Hakuna kazi serikali inayofanywa bila posho na hii imesababisha ugumu kwa viongozi katika kuwasimamia watumishi walio chini yao kama hakuna fedha. Bila posho kazi itafanyika kwa mbinde sana au huyo boss atoe ahadi ya posho pindi fedha itakapopatikana, na ahadi yenyewe iambatane na kuandikwa kwa vocha.

Kwa hiyo hii hatua anayotaka kuichukua waziri mkuu haitafanikiwa kwani posho hizi zilikwisha halalishwa wizara zote na watumishi wanajua kuwa ni haki yao. Vinginevyo asubiri mgomo baridi na ufanisi hafifu kutoka kwa watumishi.
 
Nimesikiliza huko unaweza kumpiga mtu ngumi, watu wanaiba hatari kwa kweli hakuna uchunguzi halafu unafukuzwa kazi hapana unafilisiwa rudisha pesa zote na interest juu halafu mahakamani unahukumiwa hii ndio funzo, halafu nauliza kweli nani ana sign hizi voucher ni rahisi hivi pesa kuibiwa namna hii? maswali mengi kuliko majibu.
Wala nafikiri msihangaike sana, kama matumizi ya pesa yamesemwa kuwa yalikuwa ni ya'shughuli na kazi maalumu'..... kazi iendelee.
 
Wasalaam wanajamii forum!

Kwanza kabisa naomba nitoe masikitiko yangu makubwa sana kuhusu upigwaji holela wa pesa za umma kienyeji kiasi hiki. Huu ni sawa na uuaji kabisa usiovumilika hata kidogo. Ninampa pole sana Mama yangu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Nitashangaa sana kuona Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba mpaka muda huu yupo kazini wakati wizara yake imechafuka kiasi hiki. Yaani mpaka Waziri mkuu anagundua uchafu huu waziri ulikua umelala wapi? Haiwezekani waziri upo pesa za walipa kodi zinaliwa kiasi hicho na wewe upo huenda unajua au hujui kabisa kinachoendelea, maana yake wewe hujui upo ofisini unafanya nini, yaani upo sawa na wabunge wasiokua na vyeo.

Toka awali tulisema kabisa kua Dkt Mwigulu si mtendaji ni mwanasiasa wa kelele za majukwaani, huwezi kupewa wizara nyeti kama hii Madudu yote yanatokea mikononi mwako mchana kweupe wewe upo usingizi wa pono. Kama mwananchi mwenye haki ya kutoa maoni na kuhoji, nakuomba ujiuzulu mapema tu kulinda heshima yako, walishe watu wenye weledi wafanye kazi zao.

Chande chonde Mhe Rais tumbua huyu mtu au hamisha mpeleke mazingira kule, tuletee waziri smart atakayeweza kufuatilia yote yansyotendeka ndani ya wizara. Tuna vijana watendaji na waaminifu wasioweza kutafuna pesa ya mtu wape kazi Mama achana na Mwanasiasa huyu atakupotezea malengo yako. Ningeomba ikiwezekana kabisa Mteuea hata Prof Assad CAG Mstaafu mpe ubunge wa kuteuliwa katika nafasi 2 za Rais zilizobakua kisha mpe kazi ya kusimamia Wizara hii. Ikishindikana Mhamishie Waziri Ummy Mwalimu kwenye wizara yako, huyu ni kiboko ya mafisadi.

Mwigulu anawaza Urais 2021 angebakia kua mbunge wa kawaida tu ili afanye maandalizi yake vizuri, kazi za serikali hataweza. Mama usipoteze muda katika hili fanyika kazi kwa haraka, taifa linahitaji pesa sana kwa sasa halafu zinachezewa.

Nimemaliza, sina chuki binafsi na ndugu Mwigulu Nchemba na ni rafiki yangu wa karibu lakini Maslahi ya taifa ndio kubwa kuliko ukaribu wangu na Waziri.
Ndugu yangu Mwigulu alitokea kuwatungia watu kesi ya aibu ya "UGAIDI". Mahakama Kuu Kanda ya Tabora ikamtimua kwa kumwambia atafute shitaka lingine, kwani hapakuwa na Ugaidi Tanzania. Huyu si mtu mwema hata kidogo
 
Sasa naanza kuelewa kwa nn wale jamaa walitaka kupora urais wa mama. Ni kweli kwamba mwanamke hawezi kuwa rais bora hapa Tanzania? Bado naamini imawezekana. Mama, Mh. Suluhu Rais wangu, mwenye jinsia ya kike. Fanya jambo juu ya waziri huyu mzembe ili wasioamini utendaji wa mwanamke wakuelewe vizuri.
Msimkorofishe rais acheni afanye kazi
Mnataka kesho na kesho kutwa mambo kama hayo yafanywe chinichini hapa waziri mkuu ale fungu na yeye mambo yaishie hukohuko we utajulia wapi?

ikiwa Madudu yanaanikwa mnakimbilia kumlaumu rais kwa lipi sasa
Waziri mkuu ni mteule wa rais mbona hamumsifu rais kwa kufanya kazi nzuri ya kumteua waziri mkuu ambaye ni mtendaji mzuri aliyeona hii changamoto na kuifanyia kazi?
Mwigulu mwenye wizara yake ni mteule wa rais pia kafanya Madudu yameanikwa sasa ni kazi ya rais kuangalia afanye nini juu ya huyu mtu ili mambo yaende sawa na hii ndiyo kujenga nchi
Kama wewe ndiyo rais utafanya nini ili kuweka mambo sawa Magufuli alizuia watu kusema leo watu wanasema ndiyo tunajua haya yote cha muhimu mama afanye maamuzi yasiyo na kigugumizi jela zipo
 
Vijana wa Leo ni waoga Sana, nakubaliana na wewe Kwa mambo yanayoendelea Kwenye wizara ya fedha kwamba, hayakubaliki na mhusika awajibike, Lakini stakubaliana na wewe kumpigia Debe msaafu kurudi tena kazini, wstaafu tuwapongeze Kwa kazi nzuri waliyoifanyia nchi hii Ila sio kurudi ofisini tena, vijana tutafanya kazi gani??
Hii maana yake kuna watu wana akili ambazo wengine hawana. Wana uwezo wa kiutumishi ambao hauna mfano kwa wengine.
Hii ni dhana tu ambayo ukweli ni tofauti. Wapo watu wengi na wenye uwezo, lakini kwa sababu hawajapewa nafasi ndiyo maana bila kujua wanapigiwa debe walewale.

Huwezi kujua uimara na udhaifu wa mtu kabla hajapewa nafasi kujaribu.
 
Wasalaam wanajamii forum!

Kwanza kabisa naomba nitoe masikitiko yangu makubwa sana kuhusu upigwaji holela wa pesa za umma kienyeji kiasi hiki. Huu ni sawa na uuaji kabisa usiovumilika hata kidogo. Ninampa pole sana Mama yangu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Nitashangaa sana kuona Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba mpaka muda huu yupo kazini wakati wizara yake imechafuka kiasi hiki. Yaani mpaka Waziri mkuu anagundua uchafu huu waziri ulikua umelala wapi? Haiwezekani waziri upo pesa za walipa kodi zinaliwa kiasi hicho na wewe upo huenda unajua au hujui kabisa kinachoendelea, maana yake wewe hujui upo ofisini unafanya nini, yaani upo sawa na wabunge wasiokua na vyeo.

Toka awali tulisema kabisa kua Dkt Mwigulu si mtendaji ni mwanasiasa wa kelele za majukwaani, huwezi kupewa wizara nyeti kama hii Madudu yote yanatokea mikononi mwako mchana kweupe wewe upo usingizi wa pono. Kama mwananchi mwenye haki ya kutoa maoni na kuhoji, nakuomba ujiuzulu mapema tu kulinda heshima yako, walishe watu wenye weledi wafanye kazi zao.

Chande chonde Mhe Rais tumbua huyu mtu au hamisha mpeleke mazingira kule, tuletee waziri smart atakayeweza kufuatilia yote yansyotendeka ndani ya wizara. Tuna vijana watendaji na waaminifu wasioweza kutafuna pesa ya mtu wape kazi Mama achana na Mwanasiasa huyu atakupotezea malengo yako. Ningeomba ikiwezekana kabisa Mteuea hata Prof Assad CAG Mstaafu mpe ubunge wa kuteuliwa katika nafasi 2 za Rais zilizobakua kisha mpe kazi ya kusimamia Wizara hii. Ikishindikana Mhamishie Waziri Ummy Mwalimu kwenye wizara yako, huyu ni kiboko ya mafisadi.

Mwigulu anawaza Urais 2021 angebakia kua mbunge wa kawaida tu ili afanye maandalizi yake vizuri, kazi za serikali hataweza. Mama usipoteze muda katika hili fanyika kazi kwa haraka, taifa linahitaji pesa sana kwa sasa halafu zinachezewa.

Nimemaliza, sina chuki binafsi na ndugu Mwigulu Nchemba na ni rafiki yangu wa karibu lakini Maslahi ya taifa ndio kubwa kuliko ukaribu wangu na Waziri.
Licha ya kuwa naye atakuwa kwenye nafas ya kujieleza ili tujue ni vipi amekuwa nyuma ya tukio,lakini naunga nawe mtoa post. Mh.Waziri hili limekuchafua vibaya....Kiungwana achia ngazi pengine tutakuelewa!!!
 
Kuna muda itabidi tuingie barabarani kudai haki kwa lazima.
Nchi unaambiwa hatuna hela ya kuongeza mishshara lakini kila kona mbwa wanapiga dili.
Kwa taarifa ya Wazir Mkuu leo unawaza kwanini tusingefanya kama Kibwetele tu, yaani unamuambia Wazir Mkuu na hao waandishi tokeni nje halafu piga kibiriti tutakutana jehanamu.
 
Wasalaam wanajamii forum!

Kwanza kabisa naomba nitoe masikitiko yangu makubwa sana kuhusu upigwaji holela wa pesa za umma kienyeji kiasi hiki. Huu ni sawa na uuaji kabisa usiovumilika hata kidogo. Ninampa pole sana Mama yangu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Nitashangaa sana kuona Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba mpaka muda huu yupo kazini wakati wizara yake imechafuka kiasi hiki. Yaani mpaka Waziri mkuu anagundua uchafu huu waziri ulikua umelala wapi? Haiwezekani waziri upo pesa za walipa kodi zinaliwa kiasi hicho na wewe upo huenda unajua au hujui kabisa kinachoendelea, maana yake wewe hujui upo ofisini unafanya nini, yaani upo sawa na wabunge wasiokua na vyeo.

Toka awali tulisema kabisa kua Dkt Mwigulu si mtendaji ni mwanasiasa wa kelele za majukwaani, huwezi kupewa wizara nyeti kama hii Madudu yote yanatokea mikononi mwako mchana kweupe wewe upo usingizi wa pono. Kama mwananchi mwenye haki ya kutoa maoni na kuhoji, nakuomba ujiuzulu mapema tu kulinda heshima yako, walishe watu wenye weledi wafanye kazi zao.

Chande chonde Mhe Rais tumbua huyu mtu au hamisha mpeleke mazingira kule, tuletee waziri smart atakayeweza kufuatilia yote yansyotendeka ndani ya wizara. Tuna vijana watendaji na waaminifu wasioweza kutafuna pesa ya mtu wape kazi Mama achana na Mwanasiasa huyu atakupotezea malengo yako. Ningeomba ikiwezekana kabisa Mteuea hata Prof Assad CAG Mstaafu mpe ubunge wa kuteuliwa katika nafasi 2 za Rais zilizobakua kisha mpe kazi ya kusimamia Wizara hii. Ikishindikana Mhamishie Waziri Ummy Mwalimu kwenye wizara yako, huyu ni kiboko ya mafisadi.

Mwigulu anawaza Urais 2021 angebakia kua mbunge wa kawaida tu ili afanye maandalizi yake vizuri, kazi za serikali hataweza. Mama usipoteze muda katika hili fanyika kazi kwa haraka, taifa linahitaji pesa sana kwa sasa halafu zinachezewa.

Nimemaliza, sina chuki binafsi na ndugu Mwigulu Nchemba na ni rafiki yangu wa karibu lakini Maslahi ya taifa ndio kubwa kuliko ukaribu wangu na Waziri.
kwani Mwigulu ndio kawatuma waibe Fedha za umma, inaonekana hao ndio tabia yao hiyo ya kupiga fedha za walipa kodi.
 
Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba mpaka muda huu yupo kazini wakati wizara yake imechafuka kiasi hiki. Yaani mpaka Waziri mkuu anagundua uchafu huu waziri ulikua umelala wapi?

Majina yanayowatukuza ndiyo chanzo cha uzembe na majivuno kazini na kuacha mambo ya msingi, nakumbuka aliwahi kusema ana the highest GPA na yuko smart upstairs kumbe hamna kitu
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Fedha. Amefanya hivyo ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya Fedha za Umma.

Ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, ACP Salum Hamdun kufanya uchunguzi. Tuhuma mojawapo inayokabili ni malipo ya Milioni 251 yaliyofanyika Machi 31, 2021 yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi na waliohusika.

======

Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi mkaguzi mkuu, mkaguzi msaidizi na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazowakabili.

Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu iliyotolewa leo Mei 28, 2021 inaeleza kuwa katika kikao kazi na waziri wa fedha na mipango, katibu mkuu, manaibu katibu wakuu na watendaji waandamizi wa wizara hiyo mkoani Dodoma jana, Majaliwa amemuagiza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika si za kweli wahusika warejeshwe kazini.

Majaliwa amezitaja tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31, 2021 kupitia vocha 30 ya Sh251 milioni yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi maalum ni nini na nani aliifanya.

Amebainisha kuwa siku hiyo hiyo pia zililipwa Sh198.8 milioni kwa madai kuwa ni posho ya honoraria.

Mtendaji mkuu huyo wa Serikali amesema Aprili 8, 2021 watumishi 27 wa wizara hiyo walilipwa Sh44.5 milioni za posho ya kazi maalum ya wiki nne na Aprili 13, 2021 zililipwa Sh155.2 milioni kwa watumishi 68 ikiwa ni posho ya kazi maalum ya wiki tatu.

Pia Aprili 30, 2021 zililipwa Sh43.9 milioni kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira na siku hiyohiyo zililipwa Sh14.4 milioni kwa ajili ya siku ya wanawake.

Inaeleza kuwa fedha nyingine Sh43 milioni zililipwa siku hiyo na kufanya jumla ya malipo yaliyolipwa siku hiyo kuwa Sh101.8.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Meimosi, 2021 zililipwa Sh184.1 milioni na mchana wa siku hiyo zikalipwa Sh264 milioni zikiwa ni malipo ya kazi maalum.

"Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho,” amesema Majaliwa.

Inabainisha kuwa Mei 3, 2021 zililipwa Sh146.5 milioni kwa watumishi 125 zikiwa ni malipo ya kuandaa mpango kazi wa manunuzi kazi ambayo ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku na siku hiyohiyo zililipwa Sh171.2 milioni kwa ajili ya kuandaa nyaraka za Bunge.

Taarifa hiyo imemnukuu Majaliwa akisema Sh155 milioni zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi.

"Yaani hii kazi ya ukaguzi inalipwa kwenye maeneo manne, huu ni utaratibu wa wapi? Mnazidi kutupunguzia imani, na sijaongelea eneo la kuhamisha mafungu na utaratibu kuhamisha fedha kisha mnakwenda kuzichukua huko mlikozihamishia,” amesisitiza Majaliwa.

Amewataka watendaji wa wizara hiyo kujenga uaminifu kwa wanaokusanya mapato kwa kufanya kazi kwa uaminifu na kuwatahadharisha kuwa watakaoendekea kucheza na fedha za umma hatua kali zitachukuliwa dhidi yao huku akiwapongeza wafanyakazi wenye weledi.

Chanzo: Mwananchi
Wachunguzi nao watajilipa mamilioni kama posho ya kazi maalum. Bado dipipi, hakimu na wajanja wengine.
 
Back
Top Bottom