Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Na K. U. M. A zingine zinampiga mkwala Majaliwa eti asifatilie sana maana atatafuta kumfuata JPM,

Hizi ndo zilimchukia magu maana hakuruhusu haya yaendelee.
 
Waziri Mkuu ameshalishughulikia kwa kuona TATIZO LILIKO...

PM hakusita kuiagiza TAKUKURU ifanyie kazi jambo hilo....

Leo kumtuhumu WAZIRI ambaye hata ROBO MWAKA hana ni KUMUONEA TU .....

NI KUMUONEA TU....

NI SIASA KOKO TU ....

#KaziIendelee
Kweli hii issue inafanyika Mwigulu yupo Sheria kwa maana Waziri na Katibu Mkuu kabla ya uteuzi wa mawaziri na makatibu wa mkuu ndio wanaweza kutoa maelezo ya kina tauche siasa za chuki
Kwa maelezo ya Waziri Mkuu haya matukio yametokea machi na aprili sasa kipindi hicho nani alikuwa Waziri fedha na Katibu Mkuu
 
Kweli hii issue inafanyika Mwigulu yupo Sheria kwa maana Waziri na Katibu Mkuu kabla ya uteuzi wa mawaziri na makatibu wa mkuu ndio wanaweza kutoa maelezo ya kina tauche siasa za chuki
Kwa maelezo ya Waziri Mkuu haya matukio yametokea machi na aprili sasa kipindi hicho nani alikuwa Waziri fedha na Katibu Mkuu
👍
 
Uchunguzi ufanyike kama kuna kazi walifanya walistahili malipo hiyo ni haki yao, mh.Waziri mkuu ni vyema uchunguzi ufanyike kwanza ndo uma utamgaziwe matokeo other Wise watu watachafuliwa bila sababu za msingi
 
kufuatia ukwapuaji wa fedha za umma ulio ibuliwa na Mhe. Waziri Mkuu, Je kweli hazina yetu iko salama? maana inaonekana huo mchezo ni wa muda mrefu!!

Hazina ni sehu nyeti sana kwa taifa kama ilivyo BOT, tuangalie na tuzingatie uadilifu wa watumishi ktk kitengo hicho.
 
Khaaaa....🤣🤣

Maneno yanakutoka tu.....

Ingekuwa kuachia NGAZI ni jambo rahisi kihivyo basi hakuna KIONGOZI NA BOSI yeyote angesalia UONGOZINI kila "rafu" zinapochezwa CHINI YAKE....kwani ni NYINGI....ziko hadi katika MAKUSANYO YA NYUMBA ZA IBADA......

#KaziIendelee
Mkuu kwenye nyumba za IBADA nako siku hizi kunatisha.
 
JPM alikua kiboko.. yeye ndio alikua sheria.
Ndio maana alikuwa anajichotea anapotaka, anavyotaka na mkawa mnashangilia na kutetea mpaka makoo yanawauma. Rejea 1.5 tril, 2.4 tril na utitiri wa mabulungutu ya kununulia mvuto.
Sasa Masalia waliozoezwa hivyo waliisha nogewa wanataka kuendelea. Wajameni, Katiba mpya ndio dawa.
 
Wasalaam wanajamii forum!

Kwanza kabisa naomba nitoe masikitiko yangu makubwa sana kuhusu upigwaji holela wa pesa za umma kienyeji kiasi hiki. Huu ni sawa na uuaji kabisa usiovumilika hata kidogo. Ninampa pole sana Mama yangu Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Nitashangaa sana kuona Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba mpaka muda huu yupo kazini wakati wizara yake imechafuka kiasi hiki. Yaani mpaka Waziri mkuu anagundua uchafu huu waziri ulikua umelala wapi? Haiwezekani waziri upo pesa za walipa kodi zinaliwa kiasi hicho na wewe upo huenda unajua au hujui kabisa kinachoendelea, maana yake wewe hujui upo ofisini unafanya nini, yaani upo sawa na wabunge wasiokua na vyeo.

Toka awali tulisema kabisa kua Dkt Mwigulu si mtendaji ni mwanasiasa wa kelele za majukwaani, huwezi kupewa wizara nyeti kama hii Madudu yote yanatokea mikononi mwako mchana kweupe wewe upo usingizi wa pono. Kama mwananchi mwenye haki ya kutoa maoni na kuhoji, nakuomba ujiuzulu mapema tu kulinda heshima yako, walishe watu wenye weledi wafanye kazi zao.

Chande chonde Mhe Rais tumbua huyu mtu au hamisha mpeleke mazingira kule, tuletee waziri smart atakayeweza kufuatilia yote yansyotendeka ndani ya wizara. Tuna vijana watendaji na waaminifu wasioweza kutafuna pesa ya mtu wape kazi Mama achana na Mwanasiasa huyu atakupotezea malengo yako. Ningeomba ikiwezekana kabisa Mteuea hata Prof Assad CAG Mstaafu mpe ubunge wa kuteuliwa katika nafasi 2 za Rais zilizobakua kisha mpe kazi ya kusimamia Wizara hii. Ikishindikana Mhamishie Waziri Ummy Mwalimu kwenye wizara yako, huyu ni kiboko ya mafisadi.

Mwigulu anawaza Urais 2021 angebakia kua mbunge wa kawaida tu ili afanye maandalizi yake vizuri, kazi za serikali hataweza. Mama usipoteze muda katika hili fanyika kazi kwa haraka, taifa linahitaji pesa sana kwa sasa halafu zinachezewa.

Nimemaliza, sina chuki binafsi na ndugu Mwigulu Nchemba na ni rafiki yangu wa karibu lakini Maslahi ya taifa ndio kubwa kuliko ukaribu wangu na Waziri.
Hapo kwa Mwigulu rais alichemka. Ni mwizi mzoefu anaenda kuongeza mabasi yake ya esther
 
WAZIRI ANAGANYA NINI? HAPO JE HAFAHAMU HILI? MWIGULI BROTHER PLS "RESIGN SOFLY" AND NO WAY OUT PLEASE PLEASE PLEASE.
**Mnamuumizi kichwa RAIS WETU.
POLE SANA MAMA.
Very smart prime minister.

Ila kuwa Makini mzee maana imani ya Watanzania imeelekezwa zaidi kwako sasa,Japo Kundi la mafisadi,watumishi wazembe na wezi wa mali za umma bado linakuona wewe ni kikwazo kwao
WAZIRI ANAFANYA NINI? HAPO JE HAFAHAMU HILI? MWIGULI BROTHER PLS "RESIGN SOFLY" AND NO WAY OUT PLEASE PLEASE PLEASE.
**Mnamuumizi kichwa RAIS WETU.
POLE SANA MAMA.
 
Binafsi hotuba nimeisikiliza

Inaonesha upigaji ulianza baada ya kifo Cha mwendazake

Maana yake Ni kabla hata ya Mh Mwigulu kuteuliwa kuwa waziri

Kwa hili kwa mhukumu Mwigulu sioni Kama Ni sahihi

Yapo mengi ya kujiuliza:
Mf: Waziri mkuu amepataje taarifa n.k

Lakini kwa hatua alizochukua pm Ni sahihi

Uchunguzi kwanza alafu mengine yatafuata kwa utaratibu
 
Zile bilions walizosema ndio hizo ? Dr Mwigulu alikuwa bado hajapewa Waziri pale alikywavana act tu...wakati Mpango anaumwa
 
Hii Wizara kama wameweza kufanya hayo basi wafanyakazi wote wa hii wizara wanatakiwa kuondolewa kabisa serikalini. Dawa ni kuisafisha hiyo wizara. Bila hivyo hakuna kitakachorekebika bila hatua stahiki.
 
Back
Top Bottom