Ukitaka kujua udhaifu wa elimu na ufahamu mdogo wa watz kwenye ishu mbali mbali, soma baadhi ya michango iliyoletwa hapa, kubwa eti SHERIA IFUATWE..lakini ukimuuliza maana ya hiyo sheria kuwekwa hajui!! anachojua sheria ifuatwe..majibu km haya yapo pia kwenye nyingi ya idara za serikali.."ndio utaratibu" ukimuuliza utaratibu uliwekwa ili iweje??? hajui..kwa hapa eti makontena kuletwa kwa jina la Makonda ndio sheria imekiukwa!! ujinga wa mwisho kabisa! cha kujiuliza, JE..ni kweli kuna mpango wa kusaidia elimu mkoa wa dar unaosimamiwa na Makonda?? je ofisi nyingi za walimu kwa shule za serikali mkoa wa Dar zina samani zinazotakiwa?? na nani hununua samani hizi za walimu zinapochakaa au kuharibika? mwenye akili aliyeelimika hata kwa elimu ya form iv tu asingepoteza muda kwenda kutoa povu bandarini..jibu liko wazi kabisa!
Kila kiongozi akiamua kuingiza mzigo bandarini kwa jina lake na kwa hoja hiyo hiyo ya msaada itakuwaje?
Ndomana nasema hii sheria ifutwe ili kila mtu akajiingizie kontena kwa njia yake akatoe msaada kwa jamii, ILIMRADI TU WAAMBIE NI MSAADA, NA JINA LIWE LAKO, HAPO NI MTELEZO, kila MTz alete kontena lake, kwenye manifesto aandike KWA MSAADA TU, sheria ina uonevu kwa WASAMARIA WEMAKila kiongozi akiamua kuingiza mzigo bandarini kwa jina lake na kwa hoja hiyo hiyo ya msaada itakuwaje?
Kwan Bashite wakati anaagiza hakujua kama yeye hana Exemption tax?? Hakujua kama bidhaa anayoagiza haina exemption tax?? Kwa nini asingetumia taasisi yenye exemption tax kuomba walete huo mzigo? Kama alikua na nia njema kweli???Hii sheria hii ndo tatizo, japo ipo wazi sana na ipo wazi kweli, yaani ipo wazi sana. Mh Mpango anajua anachofanya na Mh Makonda ni mzalendo, so hata wa kutetewa sijui ni nani. Mi mwenyewe napenda mzigo utoke ila pia ulipiwe kodi maana sheria inasema hivyo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Unaongeleaje swala la kodi, je tupindishe kidogo sheria mzigo uendeMakonda mdharau uwezavyo lakini perfomance yake itakufumba mdomo tu!!! Yule ni talented, amepakwa mafuta kusaidia watu! Ukipingana naye utakwenda na maji!!! Labda kama ametumia hii fursa kupitisha vitu vyake binafsi na uwe na ushahidi usiovujisha maji, lakini kama ni mali ya ofisi za waalimu kwa asilimia 100, ukimpinga unakwenda na maji!!! NI suala la muda tu, naona kuna mtu anajiloga mwenyewe hapa!!! kesho na keshokutwa asitafute mchawi!!!!!! Binafsi nilikuwa simpedi Makonda LAKINI NIMELAZIMIKA KUMKUBALI KWA PERFORMANCE YAKE!!! nI MBUNIFU MNO HAIJAPATA KUTOKEA!!! HONGERA SANA KWA RAIS MAGUFULI kutupatia kiongozi ambaye ukuu wa mkoa ni kiatu kidogo sana kwake!! Saizi ya mguu wake inadai ofisi kubwa kama ya Waziri wa TAMISEMI ili effect yake ienee Tanzania nzima. Bila shaka mkuu analiona hilo pia!!!
Tatizo unaangalia upande mmoja mkuu, akiruhusiwa kupita sheria itaruhusu mtu hata mimi kuleta msaada, na napenda kweli kutoa misaada, tatizo hii KODI, akipita makonda hata mimi ntaweza kupitisha yangu, we hupendi kuleta MISAADA [emoji848]Kwan Bashite wakati anaagiza hakujua kama yeye hana Exemption tax?? Hakujua kama bidhaa anayoagiza haina exemption tax?? Kwa nini asingetumia taasisi yenye exemption tax kuomba walete huo mzigo? Kama alikua na nia njema kweli???
Aliona kwamba hatapa political mileage??? Huu mzigo una makando kando sana!! Mpango anajua anachokifanya,no way out alipe tu,na aache kutoa matamko ya vitisho kwa watakao nunua hizo bidhaa!!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama inawezekana tusamehe pale alipokosea na tuthamini lengo lake kwani lengo lake ni zuri.Mkuu nasikia kosa la Makonda ni kuyaingiza hayo makontena kwa jina lake,kumbe alipaswa kuyaingiza kwa jina la taasisi ya Elimu.
Sent using Jamii Forums mobile app