Wateule wa Rais mbona hamumsaidii kujibu hoja za Mkataba wa Bandari!

Wateule wa Rais mbona hamumsaidii kujibu hoja za Mkataba wa Bandari!

KIKWETE pamoja na udhaifu wa Sirikali yake alitoka kufafanua mambo yaliyoleta taharuki ktk JAMII,

Magufuli pia alijaribu Kutoa ufafanuzi,

Mkapa ndo usiseme, Kila mwisho wa Mwezi alihutubia Taifa,

Suala la Bandari pamoja na kelele na sintofahamu iliyopo, kwanini Sa100 amekaa kimya?

Atoke kufafanua, maana kwenye Mnara Ule Dubei tuliona picha yake alipokwenda huko.

Ni BUSARA kunyamaza, lakini katika Issue ya bandari, atoke aitishe PRESS ahojiwe tumsikie.
Naona umekwepa swali umerukia kina Mkapa na Kikwete na wengine, rudia:

Huyo nwengine aliyesaini mikataba 19 mimi simfahamu wala hiyo mikataba mingine siifaham. Inahusu nini?

Unayo, uiweke hapa tuijadili?
 
Hilo ni dili la Rais Samia na Mbarawa, ndiyo wamesaini makaratasi; wamelikoroga, walinywe.
Hao wengine mnataka kuwafanya wanyamwezi tu kwa kuwabebesha mizigo mizito isiyokuwa yao.
Kwa "dili" unamaanisha nini? Umeusoma mkataba waliousaini? Au unahororoja tu bila mpango?
 
Naona umekwepa swali umerukia kina Mkapa na Kikwete na wengine, rudia:

Huyo nwengine aliyesaini mikataba 19 mimi simfahamu wala hiyo mikataba mingine siifaham. Inahusu nini?

Unayo, uiweke hapa tuijadili?
Mimi Sina, kama unaweza kuvujisha kama huu wa Bandari tumegee bi Faiza Fox.

Atoke kufafanua, Nchi inahitaji kujua nini kilitokea.
 
Hoja ya nani waijibu? Sijaona hoja ambayo haijajibiwa na Mbarawa.
Mbarawa katoa majibu na sio majawabu. Kwa ufupi hakuna mwananchi anaelewa mnaongea nini. Nyie majizi mnaofaidika na huo wizi, ndio mnaelewa mnaongea nini.
 
Mkataba ni siri ausome vipi? Tunachojua wazanzibari mmeamua kuuza mali ya wajinga wa Tanganyika.
Mkataba umejadiliws bungeni na upo hata hapa JF siri gani mkataba wa mashirikiano ya nchi kwa nchi?
 
Mkataba umejadiliws bungeni na upo hata hapa JF siri gani mkataba wa mashirikiano ya nchi kwa nchi?
Ule sio mkataba bali ni makubaliano ya ushirikiano. Mikataba nchi hii ni siri.
 
Mbarawa katoa majibu na sio majawabu. Kwa ufupi hakuna mwananchi anaelewa mnaongea nini. Nyie majizi mnaofaidika na huo wizi, ndio mnaelewa mnaongea nini.
Kashtski basi polisi. Au hujuwi kuwa "majizi" yanashtakiwa polisi?

Tunafahamu kwanini roho zinawauma.

Mtakufa navyo vijiba vya roho.
 
Naona huna ulijuwalo.

Kuna Tanzania bila Zanzibar?

Hivi Tanganyika iko wapi?
Ukitaka kujua Tanganyika ipo, toka huku Tanganyika nenda Zanzibar kagombee uongozi, ukikubaliwa uje utoe mrejesho hapa jf.
 
Kashtski basi polisi. Au hujuwi kuwa "majizi" yanashtakiwa polisi?

Tunafahamu kwanini roho zinawauma.

Mtakufa navyo vijiba vya roho.
Nikashitaki Polisi ipi, hii hii inayolinda majizi?
 
Back
Top Bottom