Wateule wa Rais mbona hamumsaidii kujibu hoja za Mkataba wa Bandari!

Umedanganywa na ukadanganyika.

Umeusoma mkataba?
Yes, na kurudia kuusoma tena 2×, jumla mara 3.
Siamini kabisa ndugu zetu wanaweza kutuuza kwa waarabu bila hata huruma. Huko tunakoenda lazima tutoane ngeu tu, na kesi za uhaini juu!
 
Hii dhana ya "kusaidia" , "kutetea" inazidi kuota mizizi katika utendaji wa kiserikali. Watu wafanye majukumu yao.

Maana hata mtu akiteuliwa utasikia "naenda kimsaidia rais!". Huendi kumsaidia rais, unaenda kutekeleza majukumu yako ya kichama au kiserikali kuendana na job description yako. Sio "msaada"

Na fedha zinapotumwa kwa miradi mbali mbali ya maendeleo sio "msaada" unaotolewa na rais unaohitaji shukrani. Bali ni serikali inatekeleza majukumu yake ya kikatiba....
 
Yes, na kurudia kuusoma tena 2×, jumla mara 3.
Siamini kabisa ndugu zetu wanaweza kutuuza kwa waarabu bila hata huruma. Huko tunakoenda lazima tutoane ngeu tu, na kesi za uhaini juu!
Mkataba liousoma ni wa ni IGA? Au?
 
Kwenye hii mikataba ya bandari unataka tujibu nini sasa au unataka wana ccm tucheze ngoma tusioijua?
 
Wazo lako unalitoa wakati huu,mnaanza kumkataa mama kipindi hiki!
 
Mkataba ni wa Samia na Makame hao wengine wanaogopa kupoteza nafasi zao, ila wangekuwa wazalendo wangebwaga manyanga ili kieleweke
 
Yaani unataka waingilie makubaliano ya mtu na wajomba zake?

Uwe unafikiri sawasawa.

Kama DP world Kweli Ina manufaa, kwann asiwapeleke Zanzibar?

Hilo ni lake, alinywe mwenyewe.
Mkuu umeua,wasimwingilie Mama kwani Mjomba nae ni Mama![emoji1787][emoji1787]
 
Wengi walikuwa ni wanufaika (crooks)

Good✔Jibu ni hili 👆

Wanufaika wakubwa wa bandari ni hao viongozi wakubwa wastaafu na waliopo madarakani.

wapo viongozi wengi wana share kwa wafanyabiashara wakubwa na wapo wanaofanya biashara wanao import & export kupitia bandari,sasa mirija ya upigaji iaenda kufyekelewa mbali.
 
Kwenye hii mikataba ya bandari unataka tujibu nini sasa au unataka wana ccm tucheze ngoma tusioijua?

mwanzo mlipiga mapambio mama anafungua nchi,vipi kwa sasa mmekua Sukuma gang mnamkwamisha Rais,au mmegundua kuna pumba na mchele mnaamua kumkataa mama?
 
Suala la bandari limeisha na watu wako busy kwenye utekelezaji tu.
Sasa hayo ya sijui nani asaidie kujibu sioni kama yatasaidia kubadili chochote!
Na hili litapita tu....
 
Yaani unataka waingilie makubaliano ya mtu na wajomba zake?

Uwe unafikiri sawasawa.

Kama DP world Kweli Ina manufaa, kwann asiwapeleke Zanzibar?

Hilo ni lake, alinywe mwenyewe.
La bandari lishaisha hilo
 
Suala la bandari limeisha na watu wako busy kwenye utekelezaji tu.
Sasa hayo ya sijui nani asaidie kujibu sioni kama yatasaidia kubadili chochote!
Na hili litapita tu....
kweli kabisa hili lishapita,kama ingekua ni uongo press ya Dr.Slaa kwa ninavyowajua CCM na serikali yake wasingeacha kumjibu,ila kwasababu ni kweli wameuchuna kimyaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…