Watoto hawana faida, hasa kwa masikini. Kuzaa watoto ni mateso ya kujitakia tu

Najuta kuzaliwa na wazazi masikini na mbaya wakaaga mpambano mapema, although wamenifanya niwe strong na nihustle sana mpaka kuwa na uhakika wa kuweza kujilisha, kulisha watoto wangu na kusaidia baadhi ya nnaoweza kuwasaidia. Hii ilinifanya nizae watoto wawili tu maana ndio Nina uwezo nao wa kuwahudumia. Masikini usiye na uhakika wa kipato tafadhali sana tumia condom, hawa watu maisha yamewapiga hata hiyo child support Kuna wengine wanaitamani. Maamuzi unayo mwanaume hawa wenzetu uvae condom usivae wala hawajari.
 
Hata mimi ninakubaliana na ukisemacho hasa kwa kuwachukulia wazazi wako kama mfano.
Ninachofahamu ni kuwa wanajutia sana kwa kosa la kukubali mimba iliyopelekea uwepo wako ikatungwa.
 
Amua kufariki mkuu ili na wewe usije kushuhudia mafanikio ya wanao.
 
Ili binadamu waendelee kuwepo duniani ni LAZIMA wazaliane

Unaposema hakuna UMUHIMU wowote wa kuzaa watoto maana yake ni kwamba hakuna umuhimu wowote wa binadamu kuendelea kuwepo duniani

Binadamu waliokuwepo hai miaka 200 nyuma wote wamekufa, wasinge zaliana maana yake hata wewe usingekuwepo
Ili watu waendelee kuwepo miaka 200 mbele baada ya kuwa sisi wote ambao tupo hai tukifa ni LAZIMA sisi tuliopo tuzaliane
 
Mkuu wazee wako wametimiza wajibu wao wa kukuleta duniani na kukulea kwa uwezo wao, na wewe timiza wajibu wako kutoboa
 
Mkuu wazee wako wametimiza wajibu wao wa kukuleta duniani na kukulea kwa uwezo wao, na wewe timiza wajibu wako kutoboa
Mkuu kama wewe ni mkristo na unaamini katika maandiko, moja ya mstari katiba biblia unasema, Mithali 13:22 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki. Mwisho wa kunukuu.

Agizo la kwanza la Mungu kwa wanadamu alipowaumba na kuwaweka katika uso wa nchi ni wazae na kuijaza dunia, lakini pia Mungu huyo huyo anataka uwaachie wajukuu zako urithi, yani uwape watoto wako mali na hadi wajukuu uwaachie urithi. Sasa mzazi asipotimiza wajibu wake ndio mambo yanakuwa hivyo. Tunaacha kujitafuta toka tuko watoto sababu wazee wetu wengine walikula bata sana hadi wanaondoka wanaacha laana na madeni.
 
Zaeni muongezeke muijaze dunia.
 
Baba na mama ako wasingezaa watoto wengi wewe ungekuwepo maana wewe ni mtoto wa 5 wangeishia 2 au 1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…