Watoto na wajuku zako watanunua viwanja vya kujenga wapi?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1,842
Reaction score
6,087
Umeshajiuliza waliowahi kupata viwanja kariakoo Sasa Wanaishi kama wafalme, mnaziona zile slums ambazo zipo Buguruni, Manzese zote ni hela ndefu jaribu kumuamisha mtu uone bei utakayo pewa.

Jiji la Dar es Salaam kama vile limeshajaa tu, Ukiwa na kipato kidogo jiandae kujenga kibaha kwa Mathias, au Kigamboni mbali mbali siijui hata panaitwaje, Kuna rafiki yangu machinga kajenga zake Mkuranga Lakini anafanya shughuli zake Dar, wengine Kariakoo but wanakaa Bagamoyo huko, kupata eneo mjini imekuwa shughuli sio kidogo but Ukiwa na pesa unaweza kujenga popote tu na kumuamisha mtu yoyote.

Ukienda Mwanza napo Kama unafanya kazi town na huna hela unabangaiza bangaiza kupata kiwanja labda uende sehemu wanapaita ilalila au kahama ndani ndani kabisa, nyanshishi au usagara huko, Nyasaka, buhongwa kayenze ambayo mara ya kwanza nilipoingia Mwanza yalikua ni mapori Lakini sasahivi kiwanja kidogo nimeambiwa Million 20 nikatoka nduki.

Kizazi kijacho nadhani wataanza kujenga misungwi huko, wenye pesa wawekeze kwenye real estate, nadhani ni biashara ambayo inakua thamani Kila siku, Kuna maeneo watu wanauza kama mashamba huko ndio pakununua kwa ajili ya baadae.
 
Watu wa Dar mnadhani Tanzania ni Dar tu. Ndio maana nchi haiendelei. Hata viongozi wetu wanadhani Tanzania ni Dar pekee.

Tanzania ni nchi kubwa sana. Na bado maeneo mengi ni pori kabisa. Ishu ni kubanana Dar. Ndio maana jpm aliona watu waende Dodoma.

Tafuta watu wa mafuso au wachimba visima wakupe taarifa. Nchi hii ni kubwa na ni tupu. Watu kubanana Dar ndio chanzo cha matatizo
 
Mwanza bado ni Pori
mjini kabisa kuna viwanja vya milioni 8 hapa hapa igoma. Umeme maji barabara vipo .. kwenda Town ni dk 20 tu
nipigie 0744033555
Mkuu million 8 ni pesa kweli, na anaeweza ku-afford kununua huyo anao uwezo, vipi kuhusu sisi Walala hoi, hapa mjini tutapata wapi kiwanja Cha million 3?
 
Wengi watakapokuja shtuka ardhi ni mhimu,maeneo ya mashamba ambayo sasa ni laki mbili pwani huko,muda huo itakuwa ni milion kadhaa.
Hakika asilimia 100%...wenye pesa na wenye uwezo wa kuchungulia fursa wameshanunua hekari za kutosha, wamesajili na kuanza vipimo (kuvikata).
 
Watu wa Dar mnadhani Tanzania ni Dar tu. Ndio maana nchi haiendelei. Hata viongozi wetu wanadhani Tanzania ni Dar pekee.

Tanzania ni nchi kubwa sana. Na bado maeneo mengi ni pori kabisa. Ishu ni kubanana Dar. Ndio maana jpm aliona watu waende Dodoma.

Tafuta watu wa mafuso au wachimba visima wakupe taarifa. Nchi hii ni kubwa na ni tupu. Watu kubanana Dar ndio chanzo cha matatizo
Sasa ndugu watu wanafata huduma na fursa ilipo? Tanzania ni kubwa sana na ukisafiri sehemu kuubwa ni wazi, Lakini huko unaweza kuishi? Kama bidhaa tu hakuna.
 
Ukiwa una papara Dar unaweza kuiona imejaa, lakini hadi kesho kuna viwanja vingi tu vya bei nafuu... Tatizo lenu mkipata hela kidogo mna wehuka mnapata kiherehere na ushamba wa pesa, kiwanja cha million 5-10 unaambiwa million 20. Kama hadi leo hii Tabata, Kinyerezi, Kimara, Tegeta, Boko, Mbezi n.k kuna viwanja vingi tu vizuri mnasemaje kumejaa???
Ukiwa una papara ya kununua kiwanja hata Katavi au Tabora kumejaa hakuna viwanja...
 
Madalali pia wanachangia kufanya viwanja viwe ghali. Mbezi hipi naweza pata kiwanja Cha million 3 mkuu, kama sio chanika Mwisho.
 
Sasa ndugu watu wanafata huduma na fursa ilipo? Tanzania ni kubwa sana na ukisafiri sehemu kuubwa ni wazi, Lakini huko unaweza kuishi? Kama bidhaa tu hakuna.
Katika masuala ya ardhi kuna kosa walifanya viongozi miaka hiyo ya 60 na 70. Ni kukosa master plan ya masuala ya ardhi. Mambo yakaenda ovyoovyo tu mwishoni miji ikakua ovyoovyo bila kupangiliwa. Halafu watu wakajaa kwenye miji bila mipango ndio maana unaona hiyo hali watu wamejaa Dar na wengine mwanza mpaka juu kule kwenye mawe 😂😂😂.

Hii dhana za kila kitu Dar imesababisha nchi isiendelee. Inatakiwa nchi ikue kwa kupanuka sio kubanana sehemu moja. Hizi huduma ni changamoto ya ufisadi na 10% ila nakwambia ukweli nchi bado ni kubwa na ni Tupu.

Halafu Dar ni bandari tu inaifanya iwe kama mlango wa kuingiza vitu. Kiufupi bila serikali kuwekeza katika ofisi zote kuwa Dar miaka ya 60 na 70 Dar ingekuwa kama Lindi 😂😂😂

Halafu madalali pia wanaongeza cha juu bila sababu. Una kuta kiwanja kidogo tu huko ndanindani dalali anasema milioni 90 😂😂
 
Umeongea ukweli wa asilimia 100, na Ili joto lote la dar Lakini watu wanakimbilia kinyama na kubanana, kigezo sio bandari maana hata bandari ikijengwa bagamoyo haitoweza kufika hata robo ya dar.
 
Umeshajiuliza waliowahi kupata viwanja kariakoo Sasa Wanaishi kama wafalme, mnaziona zile slums ambazo zipo buguruni,manzese zote ni hela ndefu jaribu kumuamisha mtu uone bei utakayo pewa.

Jiji la dar es salaam kama vile limeshajaa tu, Ukiwa na kipato kidogo jiandae kujenga kibaha kwa Mathias, au kigamboni mbali mbali siijui hata panaitwaje, Kuna rafiki yangu machinga kajenga zake Mkuranga Lakini anafanya shughuli zake dar, wengine kariakoo but wanakaa bagamoyo huko, kupata eneo mjini imekua shughuli sio kidogo but Ukiwa na pesa unaweza kujenga popote tu na kumuamisha mtu yoyote.

Ukienda Mwanza napo Kama unafanya kazi town na huna hela unabangaiza bangaiza kupata kiwanja labda uende sehemu wanapaita ilalila au kahama ndani ndani kabisa, nyanshishi au usagara huko, Nyasaka, buhongwa kayenze ambayo mara ya kwanza nilipoingia Mwanza yalikua ni mapori Lakini sasahivi kiwanja kidogo nimeambiwa Million 20 nikatoka nduki.

Kizazi kijacho nadhani wataanza kujenga misungwi huko, wenye pesa wawekeze kwenye real estate, nadhani ni biashara ambayo inakua thamani Kila siku, Kuna maeneo watu wanauza kama mashamba huko ndio pakununua kwa ajili ya baadae.
Uko sahihi mkuu
 
Umeongea ukweli wa asilimia 100, na Ili joto lote la dar Lakini watu wanakimbilia kinyama na kubanana, kigezo sio bandari maana hata bandari ikijengwa bagamoyo haitoweza kufika hata robo ya dar.
Katika masuala ya miji kuna ishu ya fursa za kipato. Sasa kwa kibongobongo kuna vipato aina mbili kuu.
1. Kipato toka serikalini.
2. Kipato toka sekta binafsi.

Sasa toka miaka ya 60 na 70 serikali ilikuwa Dar na watu wengi walikaa Dar na kupata kazi Dar. Na watu walinunua ardhi Dar kipindi hicho toka miaka ya 60. Pia palikuwa na miji mingine yenye nguvu kama Morogoro na Tanga. Sasa ishu ni kuwa viwanda vilifilisika. Watu wakabakia kusikilizia fursa za Dar kutokana na watu kuwa wengi Dar.
Sekta binafsi ya Tanzania bado ni ndogo sana. Na inategemea serikali hasa kupata tenda na pia kuuza kwa soko la ndani. Kama sekta binafsi ikianza kuexport bidha nje ya nchi kwenye soko la afrika mashariki, sadc, africa, china, ulaya, marekani, asia ndio itakuwa na nguvu.

Sasa kaa ukijua ya kwamba pesa haishindwi kitu. Kama mji ukiwa na bandari na kukawa na fursa za kiuchumi na viwanja vikauzwa kwa bei nafuu. Hiyo Dar inaweza kubakia patupu.

Mfano: kuna maghorofa mengi yalijengwa dar na pakawa na maofisi ndani yake. Ila serikali ilipohamia Dodoma yale maghorofa mengi ni tupu na hakuna anayepanga humo ndani. Hiyo ni kumaanisha fursa ndio kila kitu

Bado Tanzania ni kubwa na Tupu
 
Shukrani sana umeongea sahii na nimepata elimu pia.
 
Back
Top Bottom