Watoto ni gharama si baraka. Kabla hujafikiria kuzaa watoto tambua hili mapema

Mara nyingi vijana waliopata malezi bora ya wazazi na jamii hawashindwi kumudu gharama za kawaida za maisha. Fuatilia utathibitisha.

Kijana akilelewa hovyo na akafanikiwa kuwa na uchumi mzuri, hata akizaa analeta mtoto wa hovyo. Fuatilia utathibitisha.

Meta mada usitumie nguvu nyingi kupambana na matokeo, tafuta chsnzo.
 
Generations lazima ziwepo otherwise wasingezaliwa watu kabla ya Uhuru wa TZ Kwa sasa kusingekua na watu,muhimu ni kuzaa utakaowaweza wasimamia
 
Kimsingi kila mtu apige vizuri hesabu zake kabla ya kuzaa. Kuna wangese wanamuuliza mleta mada kama wazazi wake walikuwa na kianzio wakati wanamzaa yeye... hao ni wapumbavu kwa sababu hata wazazi wetu hawatapenda waone wajukuu zao wanaishi kwa dhiki kama wao walivyotulea sisi. Wazazi wetu wangependa kuona haturudii makosa yao. Sema MASKINI WENGI NI WAJINGA NA WAPUMBAVU WASIOTAKA KUSIKIA USHAURI HATA KAMA UNA FAIDA KWAO. Wengi wetu tuna ndugu kwenye ukoo wasioweza kulipa hata bill ya laki 5 hospitalini.
 
Njia ambayo Adam alikuja ilimpasa kuwepo malighafi hizo Mkuu! Adam na Hawa hawakuingia dunia through reproductive organ! Ila kuanzia Kaini na Abel pamoja na Seth huko mbele ndo walianza kupita njia hizi
Kaini na Abel wamerithi mali kutoka kwa wazazi wao. Wakati saivi wanaume kibao wanakufa wanaacha madeni na watoto wao wanaenda kuishi mtaani.

Hii generation haiwezi kuziishi falsafa za vizazi vilivyopita kwasababu za kimazingira. Zamani swala la kuoa ni la wazazi wako wewe kwanzia kutafuta mke hadi gharama za ndoa

Zamani mke ndiye atahakikisha mji wake hauna njaa kwa kulima kwa bidii, zamani unakatiwa eneo ujenge uishi na familia yako.
 
Mkuu! Unadhani kila mtu anaishi kwenye hizi fikra za kukataa kuzaa!? Tembea uone interior ndani ndani huko uond watu wanavyotumia mbegu na mayai yao kushusha watoto.
Nakubalian na hoja kuwa dunia imebadilika ila haina maana kwamba watu wasizae kisa tu maisha yana ugumu wake.
 
Kuna wale wazazi wana uwezo, wana kila kitu. Wanazaa wtt wawili au watatu. Wanaprovide vizuri tu kwa kila kitu chao.
Lkn wanashindwa kwenye malezi yenye maadili mema. Mtu ana mtt mmoja au wawili tu lkn wanakuwa wahuni, mashoga, wasagaji, wala unga n.k
Hawa mie ndio huwa nalia nao. Maana na wao sijui tuseme pia wasizae!?
 
Huna akili
 
Sizungumzii kukataa kuzaa, nazungumzia kujipanga kabla ya kuzaa.

Nisikuchoshe, lengo kuu la kuzaa na huna uwezo wa kuwatunza ni lipi?

Uwaone tu ufurahie,
Au wakutese kwa wingi wao kwa kuwatafutia mahitaji,
Au utapata sifa unao watoto wengi,
Au kuwatesa kwa kutowapa mahitaji muhimu,
Au utakuwa umewasaidia kuwaleta duniani,
Au kuongeza watoto wa mtaani,
Au? Au? Au?
 
Sio familia zote wako hivyo ila kulea mtoto kwenye poverty kwangu mimi ni uongo
 
Huko Ujerumani, Italia, n.k wanawabembeleza watu wazaliane kwa kuwalopa, cnhi omejaa vikngwe baada ya watu kuwa na akili kama za mleta mada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…