Mwiba1
JF-Expert Member
- Jun 6, 2016
- 1,122
- 2,445
Angalizo kwenye biblia watoto kuwatii wazazi, lakini pia wazazi wasiwachokoze watoto wao. Sasa mzazi Alotelekeza familia miaka kibao yupo bongo anabadilisha malaya kila siku anasubiri yupo kitandani ndio anawatafuta watoto. Unajua trauma kiasi gani watoto hao wamepitia kulelewa na mama pekee nchi yenyewe marekani ? Je mama huyo alikuwa anafanya kazi ngapi ili kuwasomesha watoto hao peke yake bila msaada. Alafu leo hii anakuja kirahisi tu kuomba msamaha. Alafu eti anakimbilia kulaani, hapo alielaaniwa ni baba kutelekeza familia yake, sio watoto kumtukana kwanza kwa malezi ya USA mtoto kumtukana mzazi ni kawaida na sio kumtusi tu hata kumfunga, nakama hizo laana zingekuwa zinafanya kazi basi vichaa ulaya wangekuwa wengi. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo kama wewe ni baba unayejiheshimu basi watoto wako watakuheshimu na kama haujiheshimu watoto wako sio kukutukana tu watakupiga ngumi kabisa na utawalaani sana.Unaweza kutoa uthibitisho kuwa hakuna laana ya baba ila ya mama TU?