Nafikiri kuna kitu wengi wetu hatukizangatii; ila huko mbeleni kinatucost sana. Pamoja na yote ni muhimu kuobserve emotional stability +emotional intelligence ya mwenzi wako. Hakuna mtu aliye emotionally stable atakayefanya jitihada za kuumiza wengine kwa sababu tu yeye ameumia.
There is no separation that doesn't hurt; uwe umemuacha mtu au ameachwa. What matters ni jinsi ambavyo tunadeal na maumivu yetu.
Sasa ukiachana na mtu ambaye ni unstable emotionally; anachokuwa anafanya ni kuwa anatafuta mtu wa kumuhamishia machungu yake. Na kwa case hiyo wewe mzazi mwenza ndiyo unakuwa 1st victim au hata mtoto wenu au mtu yeyote ambaye ataona anaweza kuwa victim wake.(Wapo wazazi ambao wanatengana halafu unakuta mzazi mmoja anahamishia uchungu wake kwa mtoto wakr; mtoto atachukiwa hadi ajute kuzaliwa). Anachotaka kuona ni kwamba unaumia zaidi; na njia rahisi ya kukuumiza ni kupitia kwa mtoto wenu.
Under normal circumstances; hakuna mzazi mwenye akili timamu atakayejisikia amani kumuona mtoto wake ananyong'onyea na kuishi kwenye upweke, questioning his/her worth kwa sababu mama yake amemwambia baba yake hamjali, hampendi, amemtelekeza; ilhali baba anajitahidi kwelikweli kupambana kuwa kwenye maisha ya mtoto wake. Nothing breaks a parent's heart like seeing your kid down. Humsaidii mtoto wako unapomjaza sumu kuhusu mzazi wake mwingine. Ndiyo maana wapo wazazi ambao wanaweza kumdanganya mtoto kuwa hiki kitu kakutumia baba yako; kumbe baba hana hata habari huko aliko. Mzazi mwenye akili timamu atahakikisha analinda hisia za mtoto wake at any cost. Mtoto kukua huku akiwa anajua kuwa mzazi wake mmoja hamtaki/amemtelekeza is so traumatic.....Humjengi mtoto kwa kumwambia mapungufu au kumpandikiza chuki juu ya mzazi wake mwingine; unamuumiza mtu vibaya mnoo
Huyo mzazi mwenzako amebeba uchungu wake wa kutosha juu yako. Yote anayofanya ni kuhakikisha tu kuwa anakuumiza na kufanya watu wengine wakuone huna maana. Sasa usikubali amtumie mtoto wako kukuumiza; na wala usikubali kumtelekeza mwanao kisa ujinga wa mama yake. Wanaume kataeni mambo ya "huyo mtoto akikua atanitafuta mwenyewe". It's high time you fight tooth and nail kwa ajili ya watoto wenu. Usimuache mtoto akue akiwa na ombwe nafsini mwake kwamba baba alinikataa. Itafaa nini mtoto wako aje akutafute akishakuwa ameharibikiwa kisaikolojia au kitabia beyond repair; kisa your absence?
Huyo baby momma wako mpeleke ustawi wa jamii; deal naye kisheria period. Huko mtapewa maelekezo jinsi ya kumlea mtoto jointly. Na mtoto akishaaanza kupata ufahamu (kama bado ni mdogo sana) utaanza kufanya naye mambo kwa pamoja ili kucreate memories na kubond naye. Aone baba akimnunulia nguo, akimlipia ada na mengineyo. In the meantime, keep records of each and everything. Kuna wanawake usipodeal nao ruthlessly; ni mtoto wenu ndiyo atakuwa affected zaidi mwisho wa siku.