Nimepitia komenti za wadau hapa,nimekuja kujua kumbe
Jamaa na familia yake (Malechela) wamemtoa dem huku bongo na kumpeleka US,wakamtafutia kazi na hata hii michakato ya uraia kwake ilikuwa rahisi sababu ya jina la Malechela.
Still bado akazinguana na baba watoto, kipindi ambacho mwenzake anaungaunga na kutaka hata kule kidogo alichokuwa nacho wagawane (unaweza ukakuta anachokipata yy ni kikubwa kuliko cha mwenzio).
Sawa mnamlaumu jamaa kwa maisha yake ya starehe huku bongo, ila hamjui may be jamaa alikuwa anapitia maumivu ya kihisia ya tokanayo na familia yake. Hiyo haitoshi ugomvi wa familia unamshirikisha tahira wa taifa Mange Kimambi ,anaweka wazi mambo ya familia public,akizani anamkomoa mmewe kumbe kuna siku zile meseji zitawaumiza wao na hasa watoto.
Jamaa kweli si malaika ana mabaya yake ila mwanamke aliyezaa nae inawezekana ikawa sababu ya maisha aliyo yaishi sasa. Kwa mbele hasa US wanawaume wanapitia maumivu mengi ya kihisia sababu ya kunyanyaswa na wanawake (mara zote wanaume hawaongei), hasa inapofikia kipindi cha talaka maana hapa kuna kugawana mbali na hasa zaidi mkewe kutumia watoto kama fimbo ya kumchapia mmewe.