Watoto wa shule sekondari siku hizi hawapendi kuchomekea! Nani alaumiwe kati ya Wizara, Wazazi au Walimu?

Kunamengi mazito ya kukomaa nayo ktk elimu yetu Africa ukiachana na kuchomekea, Elim yetu inamsaada mdogo sana kwa wanafunzi uko mbelen
Kwahiyo wavae vimini haina neno?
 
Nidhamu. Inategemea unaongelea nidhamu ya nn hasa... watu wengi wana overuse neno nidhamu. Utakua surprised kujua namna watu wa hizo shule kubwa jinsi walivo watovu wa nidhamu. Sema wao wanakua na nidhamu ya uwoga tu. Mm nawajua wengi tu waliosomea izo shule maana nilisoma nao chuo; hua hawana nidhamu sawa tu na wale wanaosoma shule za kata. Ndio wengine wana nidhamu ila wengine hawana vilevile tu kama wa shule za kata...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini hata mtaani kunahitaji nidham, hawa hawa ndo wakwe wenu baadae watawaolea watoto wenu
Watoto na vijana hawawezi kuvaa nje na kile kinchoendelea na jamii,
Utamaduni siku hizi si mali ya jamii moja, wale wenye ushawishi na vioo vya jamii ndiko ambako vijana huiga.

Mwanafunzi anataka aonekane Kama Diamond Platinum, kwa sababu anavutiwa nae, akivaa jeje a.k.a bwanga staili, nao wanavaa.

Tamthilia, muziki, wachezaji mpira na washereheshaji mbalimbali kwa ujumla ndio wanaoangaliwa.

Vijana wanajifunza kwa kuona sio kwa kuambiwa peke ake. Kwa viongozi hao nao Wana maadili?! Tunasikia ‘mipigo’ kila Kona, kwao hii tabia bado wanashindwa kuikomesha.

Hata hivyo utamaduni ni dhana nyumbufu sio funge. Kama ambavyo waliosoma miaka ya mwanzoni walikuwa wakipiga 'mlege' kuonesha ‘unyamwezi-wa-kimambele’, ndivyo ilivyo kwa Sasa pia.
 
Nidhamu katika muktadha gani? Mafanikio katika muktadha gani? Sare ina mchango gani katika kubadili ‘cognitive’ ya mwanafunzi?

‘Affection’ au? 'Affection' ya mwanafunzi inathiriwa na visabanje k.v maisha ya jamii. Na jamii imekuwa pana kuna jamii kama jamii na Kuna jamii TEHAMA.

Tv, tamthilia, mitandao, shule, wazazi wote hawa wanasanidisha data katika akili ya mtoto. Katika hali kama hii unatarajia mtoto aweje!?

Ni jambo la kawaida mama mtu kumnyoa kiduku mtoto wake ili afanane kama Sammata.
Shule inapingana na mambo menegi yanayoendelea katika jamii katika uga wa 'cognitive' na 'affection'.

Elimu inapaswa kubadili mkabala, iache kuibadili na kuprogram watu inavyotaka waishi katika jamii; elimu inatakiwa kuchechemua uwezo na utunduizi na kuongeza utashi wa mtoto wa kujitawala katka mazingira ya dunia hii yenye taarifa chungu nzima na zinafikika kwa urahisi isivyokawaida.

Kizazi cha jana kinaona kama vijana ni ‘waasi wa tabia’ ni kwa sababu tajwa hapo juu: wapiga miluzi kwa jamii tunayoishi ni wengi. Zamani mtoto alijifunza kutoka nyumbani, kanisani, msikitini na shuleni.

Siku hizi vijana wanajifunza kutoka : kwenye tv, tamthilia, mitandao, shule, wazazi, jamii, wasanii, kanisani, msikitini n.k walimu wamekuwa wengi na kila Mwalimu na mtalaa wake!
 
Lakini hata mtaani kunahitaji nidham, hawa hawa ndo wakwe wenu baadae watawaolea watoto wenu
Mkuu, haya mambo ya kutochomekea yalikuwepo toka zamani, I mean, tangu ninamaliza kidato cha sita mwaka 2007 sema kwa siku hizi watu wamekuwa wengi hivyo hata wasiochomekea wameongezeka.

Kwa mtazamo wa harakaharaka, kuchomekea kunahusishwa sana na white-collar jobs kama uhasibu na kazi zingine za kukaa kwenye ofisi za viti vya kuzunguka na AC, ilhali kazi kama kuimba muziki au kucheza soka na sanaa zingine hazihitaji wachomekeaji.
 
Nimekupata lakin kama wanafunz wakiwa katika mazingira ya shule wakiwa wamechomekea ila wakitoka ndo wanachomoa naona sio tatzo sana au sio vibaya
Asilimia kubwa ya wazazi ambao hawana muamko wa elimu pia hawana muda na good manners za watoto wao.
 
Kwamba msanii ni kioo cha jamii au siyo
 
Kwani hilo swala la kuchomekeaa linamsaidia nini mwanafunzi kitaaluma?
Badala ya kuingiza mambo ya msingi ya kuinuaa uboraa wa elimu inayotolewaa na hayo mashulee mna pambania very minor issue ambayo haina impact yoyote kwa discplined kid.
 
Kuna siku nilipita dukani nka kuta watu wamekaa kwa njee. Si wakapita wanafunzi wa shule ya kata walikua wana toka shule maongezi yalkua kama ifuatavyo,


Malaika; hizi shule uki waangalia tu unajua hawa awa toboi necta

Shetani ; hili liko wazi sijui kwa nini wana endelea kusoma hili hali wanajua darasa zima wata faulu wa 5

Malaika ; kwani waalimu wa shule za kata ni tofaut na wale wa private ?

Shetani: private watu wame lipia pesa zao waalimu awa wezi kuleta mzaa kama uku kata

Malaika : akacheka
 
Duh
 
Tukiwa MASS pale Mbeya rafiki angu alikua hapendi kuchomekea
 
Mfumo wenyewe wa Elimu ni Utumwa tupu, haina haja.

Kama vipi pigeni marufuku kuchomekea shuleni, nao watachomekea.
 
Ila kweli aisee..Mimi huku nawaona hawafanani na mwanafunzi..Mimi sijasoma zaman sana lakini angalau tulikuwa tunavaa decently, sketi ndefu, shati unachomekea unavaa na Tai. Kiatu cheusi na socks. We used to look smart!
Lakini siku hizi hata socks hawavai, hasa watoto wa kiume, sijui kimetokea nini.

Ila tusiwalaumu wao tuanze na wazazi maana wakati mtoto anatoka kwao wazazi wanatakiwa wahakikishe yuko sawa na shule pia walimu wanatakiwa waangalie uvaaji wa mwanafunzi wao maana huwezi kuwa mwalimu wa shule ambayo mwanafunzi wamevaa kihuni kihuni na ukawa comfortable. Wazazi na walimu wawe wa kwanza kulaumiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…