Kweli mkuu. Hao ilikuwa ni kuwafunga tu hakuna namna.hicho kizazi chenu unachokisifia ndio kimelifikisha taifa hapa lilipo...
na fimbo zote mlizochapwa lakini mikataba mnayosign hadi aibu kwa vizazi 100 vijavyo..
nyie wazee ningekua na uwezo ningebadiri katiba mshtakiwe woote kwa ujinga mliofanya na sifa za kijinga mnazotafuta sasa hivi
Sasa huu ndio ukoloni. We unakatiza eneo ambalo ni kiwanja watoto wanacheza mpira unategemea nini kama sio kupigwa na mpira?zaman mwalim.au baba wa mwenzenu akiwa anapita wakat mnacheza mpira mnasimamisha mnamuamkia na kama ana mzigo mnampokea mnaukimbiza hadi home kwake akivuka uwanja tu kabumbu linaendelea siku hizi ukipita katikati ya uwanja unaweza ukapigwa mtama au mpira wa kichwa na matusi juu
Si kweli, hii ilikuwa iko kila mahali siyo kwa mkoa mmoja. Leo hii mgeni yuko sitting room mtoto anaenda mpokonya simu na kuruka ruka kwenye makochi
Ilisaidia sana kuweka adabu na utii kwenye jamii. Ilikuwa rahisi kumpisha hata mkubwa wako sit kny gari lakini siku hizi yote hayo ni ndoto.
Ilikuwa unatakiwa useme "mimi hapa "ila kuna ushuzi ule wa telex huwa hautoi sauti ila harufu yake balaa.Vp tabia za wakubwa kuchafua hewa na kutusingizia watoto?
Ulikiendeleza kipaji chako cha mbio au ilikuwa unakuwa na mbio ukiona bakora?Nimecheka sana,
Me nilikua bingwa wa kukimbia vichapo, nilikua muoga sana wa fimbo.
Umesahau moja tu kwenda kucheza ambapo ulitakiwa ulale Nayo utachapwaWatoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu unaweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo:
1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa hukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa.
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaanguka, utachapwa.
27. Ukitembea na mtu mzima, akajikwaa ukamcheka, utachapwa.
28. Ukijamba mbele ya wakubwa, utachapwa.
29. Mtu mzima akijamba, ukamwangalia, utachapwa.
30. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila kupewa, utachapwa.
31. Ukinawa kabla ya wakubwa, utachapwa.
32. Ukimaliza kula ukanyanyuka kabla ya wakubwa, utachapwa.
33. Umechelewa kurudi dukani, utachapwa....
Haya yalikuwa malezi au kuoneana?Kumbuka yako
Unajisifia Kuharibu watotoWageni wakinunuliwa soda na maandazi, ukajipitisha pitisha mama atakukata jicho moja( non verbal communication) lazima utaondoka tu haraka! Ukijifanya jeuri au una temporary blindness eti hujaona hilo jicho mama atakuagiza kitu kwa jirani ili uondoke hapo mbele ya wageni, ole wako ujifanye kuwahi, mama atakufinya kifinyo cha tumbo na ole wako utoe sauti ya kilio....yaani unavibrate tu!
Siku hizi wanangu tunajibizana mbele ya wageni!
Hawa hawa wanywa viroba na wa cheza pool ukiwauliza matatizo ya nchi watakupa majibu mujarabu lakini leo wenye phd zao wasomi wa enzi hizo akili zao wamewauzia wanasiasaMkuu hao wa kuhoji mambo umekutana nao wapi? Hivi vichwa vilivyojaa viroba vitahoji nini? Wao wanawaza pool table, bet, mlegezo na viroba tu!!
Maana hakuna namnaUkiwa wa bashite darasani Utachapwa!!
(In mizengo pinda's voice)