Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Wageni wakinunuliwa soda na maandazi, ukajipitisha pitisha mama atakukata jicho moja( non verbal communication) lazima utaondoka tu haraka! Ukijifanya jeuri au una temporary blindness eti hujaona hilo jicho mama atakuagiza kitu kwa jirani ili uondoke hapo mbele ya wageni, ole wako ujifanye kuwahi, mama atakufinya kifinyo cha tumbo na ole wako utoe sauti ya kilio....yaani unavibrate tu!
Siku hizi wanangu tunajibizana mbele ya wageni!
 
hicho kizazi chenu unachokisifia ndio kimelifikisha taifa hapa lilipo...
na fimbo zote mlizochapwa lakini mikataba mnayosign hadi aibu kwa vizazi 100 vijavyo..
nyie wazee ningekua na uwezo ningebadiri katiba mshtakiwe woote kwa ujinga mliofanya na sifa za kijinga mnazotafuta sasa hivi
Kweli mkuu. Hao ilikuwa ni kuwafunga tu hakuna namna.
 
zaman mwalim.au baba wa mwenzenu akiwa anapita wakat mnacheza mpira mnasimamisha mnamuamkia na kama ana mzigo mnampokea mnaukimbiza hadi home kwake akivuka uwanja tu kabumbu linaendelea siku hizi ukipita katikati ya uwanja unaweza ukapigwa mtama au mpira wa kichwa na matusi juu
Sasa huu ndio ukoloni. We unakatiza eneo ambalo ni kiwanja watoto wanacheza mpira unategemea nini kama sio kupigwa na mpira?
 
Si kweli, hii ilikuwa iko kila mahali siyo kwa mkoa mmoja. Leo hii mgeni yuko sitting room mtoto anaenda mpokonya simu na kuruka ruka kwenye makochi

Ilisaidia sana kuweka adabu na utii kwenye jamii. Ilikuwa rahisi kumpisha hata mkubwa wako sit kny gari lakini siku hizi yote hayo ni ndoto.

Aiseee.
 
Ukila ukikomba mboga unachapwa,
na ukila ukibakisha nyama ili uile mwisho pia unachapwa
 
siku izi fimbo hazipatikani mti imezuiliwa kukatwa, fagio zina bei ghali in short material yamekua adimu
 
Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu unaweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo:
1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa hukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa.
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaanguka, utachapwa.
27. Ukitembea na mtu mzima, akajikwaa ukamcheka, utachapwa.
28. Ukijamba mbele ya wakubwa, utachapwa.
29. Mtu mzima akijamba, ukamwangalia, utachapwa.
30. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila kupewa, utachapwa.
31. Ukinawa kabla ya wakubwa, utachapwa.
32. Ukimaliza kula ukanyanyuka kabla ya wakubwa, utachapwa.
33. Umechelewa kurudi dukani, utachapwa....
Haya yalikuwa malezi au kuoneana?Kumbuka yako
Umesahau moja tu kwenda kucheza ambapo ulitakiwa ulale Nayo utachapwa
 
Wageni wakinunuliwa soda na maandazi, ukajipitisha pitisha mama atakukata jicho moja( non verbal communication) lazima utaondoka tu haraka! Ukijifanya jeuri au una temporary blindness eti hujaona hilo jicho mama atakuagiza kitu kwa jirani ili uondoke hapo mbele ya wageni, ole wako ujifanye kuwahi, mama atakufinya kifinyo cha tumbo na ole wako utoe sauti ya kilio....yaani unavibrate tu!
Siku hizi wanangu tunajibizana mbele ya wageni!
Unajisifia Kuharibu watoto
 
Nakumbuka kuna siku asubuhi tulikuwa na Mamam tunaenda kumsalimia Mjomba, njiani Mama akanunua vitumbua vya kutosha kwa ajili ya brekfast, ili tukifika homekwetu tunapiga chai. Bahati mbaya baada ya salamu za hapa na pale, pale kwa Mjomba, tukavisahau vile vitumbua pale kwa Mjomba, wakati tunaondoka Mjomba akatusindikiza.

Mbele mbele mi si nikakumbuka kuwa tumeshau vitumbua! Nikamwambia Mama. Mama akasema basi tutanunua vingine huko mbele. Mimi kwa kupenda vitumbua nikaanzisha mtiti nikimuambia mama turudi tukachukue vitumbua vyetu, Mama akanibembeleza kuwa tutanunua vingine mbele. Baada ya umbali kidogo Mjomba si akatuaga anarudi! Mungu wangu. Nilijuta. Yaani ile Mjomba kupotea tu, nilichezea kichapo hicho, yaani Bi Mkubwa hakuchagua pa kupiga! Mkono Mmoja kanidhibiti nisiporochoke, mkoni mmoja ananishughulikia! Nilijuta! Nilikoma kiherehere tangu siku hiyo!
 
copied somewhere

WATOTO WA SIKU HIZI HAWAJUI KABISA ENZI ZETU UNAWEZA KUCHAPWA KWA SABABU ZIFUATAZO:
1. Unalia sababu umechapwa, utachapwa tena
2. Umechapwa hukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa.
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaanguka, utachapwa.
27. Ukitembea na mtu mzima, akajikwaa ukamcheka, utachapwa.
28. Ukijamba mbele ya wakubwa, utachapwa.
29. Mtu mzima akijamba, ukamwangalia, utachapwa.
30. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila kupewa, utachapwa.
31. Ukinawa kabla ya wakubwa, utachapwa.
32. Ukimaliza kula ukanyanyuka kabla ya wakubwa, utachapwa.
33. Umechelewa kurudi dukani, utachapwa.N.K

Na mengine uyajuayo
Ndio maana watoto wa zamani tunaheshima hata nikipokea meseji napiga magoti
 
Mkuu hao wa kuhoji mambo umekutana nao wapi? Hivi vichwa vilivyojaa viroba vitahoji nini? Wao wanawaza pool table, bet, mlegezo na viroba tu!!
Hawa hawa wanywa viroba na wa cheza pool ukiwauliza matatizo ya nchi watakupa majibu mujarabu lakini leo wenye phd zao wasomi wa enzi hizo akili zao wamewauzia wanasiasa
 
Usipowatetea mafisadi na waharifu wa makosa mbalimbali wakati wewe ni mwanachama wa cdm utapigwa tu
 
Back
Top Bottom