Watoto wako walibadilisha vipi maisha Yako...!

Watoto wako walibadilisha vipi maisha Yako...!

ERoni
Ushimen
Grahams
binti kiziwi
Kalpana
Liverpool VPN 😄mje mtupe experience zenu baada ya kupata watoto
Daah mimi sijui hata nisemeje..ila wamenifanya niwe organised..yani nadhani unanielewa kuanzia chakula...utunzaji wa hela...n.k
Halafu kingine kikubwa wamenifanya niwe na moyo wa ufatiliaji wa vitu vingi sana..zamani nilikua siwazi ila siku hizi kabla sijafanya kitu najiuliza kwanza outcome yake nk..
 
Nilipata kazi nikiwa kwenye 26 yenye mshahara wa kuanzia comma mbili, matumizi yangu yalikuwa rafu, nguo na viatu nanyooka dukani hata kiatu kiwe laki na nusu nabeba, mwaka naweza kubadili simu 5, kubadili magari, n.k. kiufupi sikuwa na dira.

Siku ya siku najuzwa umekuwa baba ila nilisita kuamini, ni baada ya mtoto kuzaliwa akiwa copy tumefanana pua hadi komwe ndipo nikajua sasa nimekuwa rasmi father.

Ni kama akili ilipigwa facrory reset, ni ile hali ya kujiona sasa umekuwa kichwa cha familia, nilianza kuwaza future, nilipunguza sana matumizi simu moja miaka miwili, kununua nguo nilijibana sana, chakula kuna muda narudi kula nyumbani, nilipunguza kwenda viwanja, n.k.

Kitu kinachofanya mwanaume abadilike zaidi baada ya kupata mtoto inategemea pia na uhusiano na mwanamke, kama hakuna mahusiano mazuri mwanaume anaweza asibadilike na hata kuongeza safari za bar, kushinda, nje, kuoa mwanamke mwengine, n.k, wengine watapeleka mtoto kwa bibi au kusubiri miaka ya kisheria ya kumchukua mtoto
 
mtoto wa kwanza nilijiona still mama's little princess, yan bado najiona mtoto hii ilichagizwa na kushikwa na uchungu kwa siku saba nakuja kujifungua mtoto sina kazi naye kabisa, ukweli sikuona mabadiliko hapo bado niko kwetu nakula uzazi ile kurud kwangu unaamka asubuh mtoto anakusubiri baba ake naye ilibidi nipambane nijione dah mbona kama mambo yamenibadilikia haraka sana nilitaman kurud kwetu sema nikajiambia sasa hii sndo faida ya kuolewa narudi kufanya nn tena nikakaza kizaazaa nikabeba mimbaingine fasta huku huyu first born ananyonya kilichonistua ni kutapika kwake napima imo ile siku nililia sana niliona kabisa ya kwanza niliponea tundu la sindano this time around nakwenda kufa, nikaanza kufikiria kuhusu yeye ataishije roho inaniuma naona ninemkatili mno kumwambia mama naona aibu ikabidi tuambizane na baba ake kwanza nikamuachishe dogo nyumban tuangalie hili jipya jingine ndio namwelezea mama, akasema muachishe nikaachisha mimba haikunisumbua hata kidogo baba yao Mungu ampe maisha marefu mtoto wa mama mkwe alikua benet yan akirud jion ananisaidia nilipoachia anahakikisha sikosi mahitaji muhimu, mpaka nikajifungua sasa huyu wa pili madaktar walikua wanaambizana mapigo ya moyo ya mtoto hayasikiki na nina odema plus plus nikawanajisemea rohon kama nakufa siwez zuia mwanangu tu ninayemuacha sina namna nikajifungua toto langu la kilo nne pt saba kawaida kabisa hakunisumbua kabisa lakini huyu ndio alinifanya nione hell nooo mimi n mtu mzima sasa, natakiwa kubehave kama mama, na ndipo nilibadili rasmi mtindo mzima wa maisha yangu, yani nilianza kiyachukulia maisha kwa ukaribu zaidi, nalea sasa vipacha vyangu vya nje maisha yanakwenda
 
Natamani muendelezo jamn mbna nzuri hiv 😍
 
Nilipata kazi nikiwa kwenye 26 yenye mshahara wa kuanzia comma mbili, matumizi yangu yalikuwa rafu, nguo na viatu nanyooka dukani hata kiatu kiwe laki na nusu nabeba, mwaka naweza kubadili simu 5, kubadili magari, n.k. kiufupi sikuwa na dira.

Siku ya siku najuzwa umekuwa baba ila nilisita kuamini, ni baada ya mtoto kuzaliwa akiwa copy tumefanana pua hadi komwe ndipo nikajua sasa nimekuwa rasmi father.

Ni kama akili ilipigwa facrory reset, ni ile hali ya kujiona sasa umekuwa kichwa cha familia, nilianza kuwaza future, nilipunguza sana matumizi simu moja miaka miwili, kununua nguo nilijibana sana, chakula kuna muda narudi kula nyumbani, nilipunguza kwenda viwanja, n.k.

Kitu kinachofanya mwanaume abadilike zaidi baada ya kupata mtoto inategemea pia na uhusiano na mwanamke, kama hakuna mahusiano mazuri mwanaume anaweza asibadilike na hata kuongeza safari za bar, kushinda, nje, kutafuta mchepuko au mke wa pili, n.k,
Exactly wanawake pia wanachangia lkn nafikir ujionwa mtoto hushtua wazazi wote wawil
 
Mwanangu wa pili, alinifanya niwaheshimu zaidi wanawake, akiwa kichanga hakumtaka mama ake, dada wa kazi wala mtu mwingine zaidi yangu.

Kanipigisha sana mikesha, hadi nikajua kua wanawake wanajukum gumu sana la ulezi hivo wanahitaji heshima ya pekee.
 
Mtoto wangu wa kwanza nampata baada ya wiki 2 kumaliza mtihani wa form 6, nilitia ujauzito wakati nipo A level, ukweli usiopingika mimba ile ilinifanya nikaharibu form 6, palikuwa hapasomeki, shule hapaendeki, mpaka mwl. Wangu wa fizikia ananitafuta baada ya kuona nimekuwa mtoro sana, alinipenda sababu form 5 nilikuwa napasua sana physics, alikuwa ananitegemea, ila baada ya ile mimba shule ikaanza kulegalega(hapo katikati kuna mengi)

Mtoto akazaliwa, matokeo yakatoka nina 4, siwezi kwenda chuo, bimkubwa akaniweka chini, akielewa yaliyotokea, habari za mimba alikuja kuzipata mimba tayari ina miezi kama 7-8 hivi(too late, hili suala la kuficha ukweli ndio liliniponza na shule)
Bimkubwa akataka niende chuo(diploma) akanikabidhi na ada kabisa, baada ya kufikiri kwa kina nikaghairi kwenda chuo, nikarudi kwa bimkubwa nikamueleza uhalisia tayari nina mtoto ninapaswa kusimama kama baba, hivyo siwezi kwenda chuo, hii pesa ya ada naifanyia biashara kisha nikikaa sawa nitajisomesha, hiyo sababu ya kwanza ambayo nilimueleza, ya pili ilikuwa moyoni, haina nguvu kama ya kwanza lakini pia nilikuwa najisikia kauvivu kuanza diploma, wakati wenzangu wapo degree, lakini kibaya zaidi wale ambao nilimaliza nao la 7 wako mwaka wa pili, sababu mie form 1 nilisoma mara 2, ya kwanza nilimpiga mwalimu, wakanitimua shule, nikaenda kuanza upya, hivyo wale wenzangu wanakuwa mwaka wa 2 nami ndio kwanza diploma.

Bimkubwa akakubali kishingo upande, nikaanza biashara, home kulikuwa na tv hizi, nikapata Playstation 2, lakini pia kuna banda nilinunua kipindi nipo A level kwa ajili ya kufungua saluni(A level nilikuwa nasoma huku napiga mishe mishe hasa za udalali wa simu na deals nyingine halali) kibanda kile nikaghairi, nikamkodisha muuza chips, nikawa nakunja elfu 6 yangu daily, na zile ps2, nikawa navuta sh 10 mpaka 20, kinachoingia naangalia mtoto na kingime nahifadhi, nikanunua pikipiki ya kwanza, ya pili, nikarudi chuo hapa yakaanza maseke, pikipiki ya pili ikaibiwa ikiwa haina hata mwezi m1, Playstation wakaja askari kuzibeba, nikaenda kuwaletea noma na ujeuri wangu, nikazipata nikauza.. Nikanunua pikipiki used kama 2 hivi na ile ya zamani zikawa 3, madereva kwa kuwa nipo chuo, hela hawapeleki, service hawafanyi, nikazikuta zimechoka kinoma, nikaja nikayauza kwa hasara.

Kuhusu ulezi mwanangu nilimchukua akiwa na miaka mi3-4 hivi nikaishi nae, akaja akaanza la kwanza, mpaka la 3 ndio mimi nikaoa mwanamke mwingine, sikumuoa mzazi mwenzangu, sababu niliona ana akili za kushikiwa toka mwanzo niligundua mama yake mzazi ni mpenda hela hivyo mie alikuwa hanikubali, niliamua kumuoa sababu tu kwao alikuwa akinyanyasika kisa kazalia home, niliamua nimpe heshima, aheshimike.
Ila alijitela nahisi maneno ya mama yake yalimuingia, wakati nataka kwenda kumalizia mahari, akaanza ooh, sijui tutafute maisha kwanza, kimeenda kimerudi, kumbuka hapo nilishatanguliza kama laki 7 hivi katika mahari ya milioni 2, nikampa kauli moja unataka ndoa ni sasa, hutaki basi sahau kuolewa na mimi, nikamuuliza "TUTAFUTE MAISHA KWANZA, TULIYAPOTEZEA WAPI" 😂

hapo nikafunga file lake mpaka nilipokuja kuoa mke wangu huyu wa sasa.
Nimelea mwanangu kwa mapenzi mpaka anafika la 3, mama yake anakuja kumchukua ampeleke shule, kenge yule toka kamchukua mtoto, hajataka kumleta kwangu likizo yoyote ile, kila nikimtaka mtoto ni sababu tu, mpaka hivi sasa kaingi darasa la 6, na inaonesha anamjaza sumu mtoto kuhusu mimi baba yake, alishambadili ma dini, akaulizwa kwanini umefanya hivyo eti baba yake alinikataa 😂 na katika watoto wangu woote, huyu ndio alinikaa kumoyo kutokana na stori yake ndefu, ila huyu mwanamke anafanya kila kitu kiwe kichungu kwangu.
Nilipofikia nimeweka mikono juu, mtoto akipokea sumu za mama yake sawa, akiwa mdadisi akasimuliwa na watu wema kwao juu ya mazuri na upendo wangu kwake na akaijua thamni ya mdingi wake sawa pia.

Khabari ni ndefu sana, ila kwa leo inatosha.
 
Back
Top Bottom