secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 23,984
- 51,055
Wakuu, hawa watoto wetu sometimes wanajua sana kutuaibisha/ kutuangusha.
Jumatatu iliyopita nilishiriki mahafali ya darasa la Saba ya binti yangu. Mambo yalikwenda tu vizuri mwanzoni, lakini baadaye hali ya hewa ilichafuka kidogo.
Hali ulianza kubadilika pale watoto walipoanza kuonesha vipaji vyao, wa kucheza alicheza, wa kuchora alichora basi ikawa shwari tu!
Aisee! Ukafika muda ambapo mwanafunzi mwenye kipaji Cha kuimba akaitwa, basi akatokea kijana wangu wa darasa la tano, akinyakua kioaza sauti kwa mbwembwe akaanza kuuimba wimbo wa NEY WA MITEGO "PALE KATI PATAMU" kuanzia mwanzo hadi mwisho 😯😯😯
Mzee mwenzenu, kutokana na kutotegemea hili, macho yalinitoka mithili ya Zongibinyo na kujiuliza, iweje mtoto ambaye kutwa akiwa nyumbani hupendelea kuimba tenzi za rohoni aporomoshe bongo flava isiyo na maadili.
Lile tukio lilishusha sana heshima yangu hasa ukizingatia kuwa Mimi ni mzee wa kanisa hapa Kijijini.
Hawa watoto hawa! 😹😹