Watoto wangu wote hufariki baada ya kuzaliwa au mimba kuharibika


Solution nn ukiwa ivo
 
Yawezekana wewe sio mleaji Mungu nae anaepusha viumbe hivyo visije kupata tabu duniani,kingine watoto ni Rizki kama Rizki nyingine kama Muumba kakupangia usiipate basi hata ufanyaje hautapata muhimu shikamana na imani yako Oa muombe Mungu akupe hitajio lako la Watoto acha uzinifu.
 
😀 😀 😀daah na wew na huyo mwanamke hamjielewii wote... yani mtu ana mtoto wa miezi 4 unamwagia ndani tu na maskini ndo tuna huu upuuzi una vitoto vingi kuvibebanisha tu
 
😃😃😃🙌msalimie mtaalam
 

Pole kwa unayopitia. Ni vyema kufika hospitali na kufanya ufatiliaji kwa mambo haya:

1: Grupu la magonjwa yanaitwa TORCH.
TORCH ni kifupi cha magonjwa ya: Toxoplasma gondii, Others/wadudu wengine wahusikao( Syphilis, Pavovirus, Listeria na H. Zoster), Rubella, Cytomegalovirus (CMV), na Herpes simplex virus (HSV).

Magonjwa haya huambukizwa kwa mtoto wakati wa ujauzito kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na wakati mwingine baada ya kuzaliwa. Kama una mojawapo ya haya, unaweza kuwa chanzo cha maambukizi kwa wenzio.

Madhira ya magonjwa haya ni:
1: Ujauzito/mtoto kutokukua vizuri
2: Mimba kuharibika
3: Kuzaa watoto waliofariki
4: Kuzaa watoto ambao hufariki baadaye.

2: Rhesus factor/incompatibility
Hii pia inaweza kuhusika, kwani ina madhira kama TORCH. Litabaki hapo kwa sababu hatujui aina ya magrupu ya damu na rhesus factor zao zote. Ni vyema pia ukilifanyia kazi kabla ya maamuzi yako ya mwisho kwenye kupata mwenza wa maisha.

3: Coincidence:
Suala la mapacha, linaweza likawa ni sababu ya uchanga/prematurity na huduma waliyopata baada ya kuzaliwa kulingana na changamoto zinazowakuta.

 
Pole na poleni nyote wenye kadhia kama hii, kwa namna tofauti.

CHUNGUZA ILI KUJUA CHANZO.
Chukua hatua mbili.
1. Kisayansi. Nenda hospitali kamuone daktari.
2. Kiiman.
Uchunguze ukoo wenu kwa kuwaangalia ndugu upande wa baba na upande wa mama, ikibidi washirikishe maana wazazi hua ni ngumu kuwaeleza watoto wao mambo kama haya mpaka yatokee. Chunguza unaweza kuta ni tatizo la ukoo.
Je, umewahi kumkatili binti wa watu kihisia? Chunguza.
Je, umewahi changia binti kutoa mimba yako? Chunguza.
Hutakosa pakutokea. Binafsi hapo kwenye imani wekeza nguvu zaidi.
Kila kheri MUNGU akusaidie.
 
Pole sana ndugu mungu atakujalia siku moja …… ushauri wangu nenda kapimwe mimi nazani kuna possibility kubwa huko na ugonjwa unaita sickle cell anemia. Again pole sana
 
Huyo Rafki yako Ana Laana!! Amempa mimba Mschana asiempenda akamforce atoe mimba ila Dada WA watu alikataa akaishia kufariki siku ya Kujifungua! Hajajifunza wala Hajakoma eti sshv anaendelea Kumwagia Ndani kila anaekutana nae eti liwalo na Liwe, huyo atakuja kuishia kupata UKIMWI. Mwambie akaombe Msamaha kwenye Kaburi LA huyo Binti na Kichanga chake😏
 
usisahau na kufanya dawa za kitaalam pengine majini wanakula watoto wako
 
mkuu hii kitu inaumiza sana ni vile inawakuta watu wchache hawawezi kuelewa,ila namini yote ni mipango ya Mungu wakati sahihi ukifika nitapata watoto wengi zaidi hata ya niliowapoteza
Imani ndio Cha muhimu, jipe Moyo mkuu
 
Katika maelezo yako yote hamna sehemu uliyosema umeoa, Mimi naona utafute mwenza sahihi uoe Kwa pamoja mtashinda Hilo unalopitia.
Si ajabu Kuna agano lilifanywa na mababu zako kuwa usizae Nje ya ndoa.
Mambo ni mengi other things are more spiritual than we can imagine.
 
Kwani lazima mzae,ulimwengu ushakuwa mgumu huu.
 
Ingia kwenye Maombi kaka lia na Mungu sana . Piga Dua kwa Imani kubwa kaka . Pole sana kaka Naomba Mungu akusaidie hio hali iishe na amini inawezekana kupata watoto kaka kwa Mungu hakuna lisilowezekana kaka
 
Sahii kabisa,
Kuna Vitu haviko sawa kwenye past yake
 
Acha zina wewe,owa kwanza then uje huku tukushauri vitu vya kukusaidia...
 
Andaa sadaka nzuri na ukamtolee Mungu anayetupa uhai.
Pia ni vizuri upate mke na ufunge ndoa kwa mujibu wa imani yenu.
Sio kunyandua kila aliye mbele yako.
Sadaka inavunja agano na laana.
Pole sana aisee.
 
dah[emoji22],,huwezi amini mkuu nina hicho kinyama sehemu ya haja kubwa na kimenitokea miezi kadhaa iliyopita
Pole kama kuna wazee kwenu waeleze hili watakusaidia kuna dawa zake inategemea na koo na kabila hivyo waone wazee wako washirikishe hili tatizo sio maarufu sana ila lina athari kubwa na bbn linatibika kumbuka sio bawasiri ni tatizo tofauti ila hufanana na bawasiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…