Watu 11 wamepoteza maisha ndani ya Kiwanda cha Mtibwa Sugar, Morogoro

Watu 11 wamepoteza maisha ndani ya Kiwanda cha Mtibwa Sugar, Morogoro

Wameitangaza hii UTV kwenye Morning Trumpet.

Kiwanda kilikuwa kimeandaa na kutengeneza umeme wao pitia mitambo yao ya kufua umeme huo inawezekana kutumia maboiler ya huko kiwandani.

Usiku wa leo ndio walikuwa wanawasha rasmi huo umeme wao, inaonekana umeme umekuja ukiwa mkali na kusababisha control room ilipuke na kuungua kulikopelelea vifo vya hao watu 11. Kwenye control room hiyo kulikuwa na watu 13. 11 wamekufa hapo hapo na 2 ambao mmoja ni mtanzania na mwingine ni raia wa kigeni walikeruhiwa na sasa wapo Hospitali.
 
Kuna taarifa nimezipata kutoka kwa mtu wangu wa karibu anadai Watu 11 wamefariki Dunia ndani ya Kiwanda cha Mtibwa Sugar kilichopo Morogoro kutokana na hitilafu za kiufundi.

Wenye taarifa kamili tujuzeni

==== ===

Watu 11 wakiwemo raia watatu wa kigeni wamefariki dunia na wawili wamejeruhiwa kwa ajali iliyotokea katika kiwanda cha uzalishaji wa sukari cha Mtibwa baada ya kutokea kwa hitilafu ya mtambo wa mvuke wa kuzalisha umeme.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama amesema tukio hilo limetokea majira ya saa saba na nusu usiku wa kuamkia leo Mei 23,2024.

Kamanda Mkama amesema raia wa kigeni waliofariki ni kutoka nchini Kenya, India na Brazili

Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Mtibwa Sugar na majeruhi wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Bwagala.

Waliokufa ni wataalamu wa umeme na mitambo ambao walikuwa kwenye chumba cha kudhibiti mitambo hiyo.

Chanzo: AZAM TV
Chanzo sio Azam TV ni UTV kipindi cha Morning Trumpet kwani hakuna channel iitwayo Azam TV 😀😃😄😁
 
Kwaiyo wameiva kwa mvuke poleni wataalam ajali kazini, kwanini wasiwe na yale manguo spescheli
 
Aisee,niliwahi kufanya kazi hapo mwaka 2009 napajua vizuri nilitumia sana lile basi lao la kiwanda kwenda Madizini na kurudi kiwandani.Pole kwa ndugu zao.
 
Wameitangaza hii UTV kwenye Morning Trumpet.

Kiwanda kilikuwa kimeandaa na kutengeneza umeme wao pitia mitambo yao ya kufua umeme huo inawezekana kutumia maboiler ya huko kiwandani.

Usiku wa leo ndio walikuwa wanawasha rasmi huo umeme wao, inaonekana umeme umekuja ukiwa mkali na kusababisha control room ilipuke na kuungua kulikopelelea vifo vya hao watu 11. Kwenye control room hiyo kulikuwa na watu 13. 11 wamekufa hapo hapo na 2 ambao mmoja ni mtanzania na mwingine ni raia wa kigeni walikeruhiwa na sasa wapo Hospitali.
Duh R.I.P engineers wamekufa kwenye harakat.
 
Kwa vyombo vyetu hiyo sio habari kubwa. Hata hutaisikia kivile Africa ni Africa.
 
Back
Top Bottom