Watu ambao Wanatengeneza maudhui (Content) ndio wanaopewa ajira sana zama hizi, fursa za pesa Tanzania zipo kwenye Content creations

Watu ambao Wanatengeneza maudhui (Content) ndio wanaopewa ajira sana zama hizi, fursa za pesa Tanzania zipo kwenye Content creations

Elezea content zake vizuri, kama sio kwamba wenye biashara ndo wanawekaza kwake ili aendelee ku-promote biashara zao, huyu haiko independent anamilikiwa na kampuni fulani ku promote brand yao.

Yupo independent kama mwijaku.

Mwijaku ameajiriwa na clouds fm ila haimzuii kufanya matangazo ya kampuni zingine

Huyu binti pia ameajiriwa na Tilisho ila haimzuii kufanya matangazo na kampuni zingine

Nenda katazame page yake. Yeye anafanya kazi za matangazo na kampuni nyingi. Yeye matangazo ya ma bus tu ndio anakataa kampuni zingine sababu ni wapinzani wa Tilisho. Ila kama sio bus anakubali anapiga hela yako

Ni balozi wa hisense Tanzania.
Anatangaza hotels za watu
Anatangaza madawa ya watu
Yaani kila dili ya pesa haachi anakufanyia tangazo
 
Ndo shida kubwa ya dada zetu watanzania ukifika kwake anakua obsessed na kutongonzwa kwanza, anijahidi asiwe cheap kwako, wskati wewe ni mteja unahitaji huduma tu.
Tatizo na sisi wanaume wa kitanzania tamaa mno, tukipokelewa vizuri na tabasamu hapo hapo tunasimamisha, tunaomba namba, kimasihara inatawala kichwani. Hii nchi ni ngono tu yaani.
 
Huu ni ukweli mchungu, zama zimebadilika

Vijana mnaomaliza chuo mjifunze kutengeneza content zitakazotrend hasa za kuelimisha, kufundisha, kuburudisha na kuchekesha watu..

huko ndipo kuna fursa za dili nyingi zama hizi
muhimu content 🐒

unaweza kua na elimu au huna but what matters most ni content 🐒
 
Tatizo na sisi wanaume wa kitanzania tamaa mno, tukipokelewa vizuri na tabasamu hapo hapo tunasimamisha, tunaomba namba, kimasihara inatawala kichwani. Hii nchi ni ngono tu yaani.
Kuomba number sio kosa, kosa ni kunikubalia maombi yangu ya hovyo na kuharibu kazi yako.
 
Kuomba number sio kosa, kosa ni kunikubalia maombi yangu ya hovyo na kuharibu kazi yako.
Mkuu, kila anayekuja akimuomba namba ili amtongoze unategemea atakuwa sawa? Imagine kila mwanamke anayekuja ofisini kwako anajilegeza, anakukonyeza, utaweza kufanya kazi? Ndo maana na wao ukifika tu wanajua atatongozwa sababu weshajizoelea aina ya wanaume waliopo. Nchi akili za watu wake ni ngono tu.
 
Wanaweza wasifurahie lakini yeye maisha yanamnyookea anaishi anavyotaka yeye.

Simpendi huyu jamaa lkn ndo hivyo naona akifanikiwa kwa upuuzi wake
Tatizo jamii ya watanzania haijui kuchuja takataka na dhahabu, tanzania mtu yoyote anaweza akawe cereblity bila kufanya mambo ya maana unakumbuka Dr shuka sikumvuki jina vizuri alipata umarufu kwa ujinga tu, nk, Elimu yetu imeshindwa kutegeneza jamii ya watu intellectual.
 
Mwijaku sio mpuuzi. Bali Mwijaku amechagua niche ya upuuzi uchawa ili awe unique kwenye kutengeneza content zake. Kuna kitu kinaitwa Niche kwenye content creations.

Mwijaku ana degree ya maigizo kutoka creative arts udsm

Kabla hujaanza kutengeneza content zako kwanza Lazima ujue unapita njia gani ili upenye sokoni ukubalike.

Ndio maana kuna foodlover yeye amechagua niche ya mapishi. Yeye anapiga hela za matangazo ya wauza vyombo tu na spices

Kuna kina Steve mweusi yeye amechagua niche ya comedy

Kuna kina Lilian yeye amechagua niche ya ukungwi. Kufundisha mapenzi.

Lazima uwe na niche
Kama ni graduate kweli tena ana first class degree Bcom, ni mpuuzi mkubwa hiyo dispised Unemployement, hiyo kazi inaweza kufanywa na wakina Nyerere ambao hawana shule, ni sawa sawa kumuona medical sajioni anaendesha daladala na na inamlipa kama 8m kwa mwezi then umsifie kwamba ana akili na anapiga pesa.
 
Huyu binti content zake za ukonda wa bus Tilisho zimempa dili nyingi za ubalozi na matangazo. Na instagram ana followers milioni

Hapo tu ana miaka 24 ameshanunua gari yake. Na hata chuo kikuu hajafika

Kuna watu kibao wanafanya kazi miaka kibao serikalini na private sector ila hawawezi kununua hata IST. Maana wanategemea source moja tu ya income

View attachment 2950665
Huyu dem kafanikiea like BOOM.
Sidhani kama alitegemea au labda alikua na mipango ya afanyacho.
 
Watanzania hadi tutakapoacha kula UGALI ndiyo tutakuwa na akili
Itakuwa Ugali unatumbaza ety.MD anamalza chuo aruhusiwi kufungua duka la dawa ila masai ajaenda hata shule anapewa kibali na wizara cha kuuza dawa..
 
Angeweka ya ngono😄tungejazana lundu we siunaona baby wa Taifa ni udsm alumn ila ni kungwi.
Ndo ivo mkuu, contents za maana hupati watu, ila zile za kijinga utalamba mamilioni.

Na hii ndio sababu watu wanatapeliwa kijinga, mtu anataka kazi ila kufatilia platform za kazi hataki yeye anafatilia udaku.
Hataki zile kazi za kwenda kufanya interview, yeye anataka kamserereko.

Sasa wajanja wanakuja kukupigia humohumo kwenye kamserereko ukatakako.
 
Back
Top Bottom