JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,114
- 3,541
Naam, wana bodi !
Niende moja kwa moja kwenye mada. Nayo inahusu watu dhaifu. Watu dhaifu ni watu hatari sana. Wakiwa wanasiasa wanakuwa hatari zaidi. Ni waoga wa mabadiliko. Waangalie wale wote waliobeba agenda ya mitano tena. Karibu wote ni dhaifu kisiasa na kijamii. Wanaposema mitano tena wanasukumwa na ubinafsi na kuogopa kuwa akija kiongozi mwingine watabaki na ulaji wao kweli?
Ukimtazama yule Mbunge wa Makambako utagundua haya ninayosema. Kwanza yule hata darasa la Saba hajafika, anawaza kwamba hivi akija kiongozi mwingine atakubali kumwacha aendelee kugombea ubunge na elimu yake duni ilihali ndani ya chama kuna wasomi wazuri tu? Kwa hiyo dawa ni kujifanya anampenda Rais na kutaka aendelee milele. Ni udhaifu wake ndio uliomfikisha hapo.
Mwigulu Nchemba ni msomi dhaifu. Ni kiongozi dhaifu hata kuliko watu ambao hawajasoma. Amefikia hatua anauliza watu wanadai KATIBA, KATIBA ya nini wakati Magufuli anatosha? Unajua kwanini? Amejua mapungufu ya mtukufu bosi wake kwa hiyo yupo tayari kuweka pembeni elimu yake yote ilimradi anapata mkate wa kila siku na kulinda maslahi yake kisiasa. Ni mtu dhaifu siyo mtu wa principles.
Kuna yule sijui Kessy, Mbunge Wa zamani wa Nkasi. Wajumbe walimchinjia baharini baada ya kuona amebeba agenda mfu. Nkamia naye wajumbe waliona dawa inayomfaa ni kumchinjia baharini. Ametulia !
Ninachotaka kusema ni kwamba watu dhaifu popote pale ni hatari. Wanakuwa hatari zaidi wanapokuwa wanasiasa. Mara nyingi hawana aibu. Ni wajinga wa milele. Kwao wao ustawi wa Nchi siyo kitu cha maana kuliko mafanikio yao binafsi. Hawabebi agenda za Nchi. Hawaangalii ajira kwa vijana, Utawala bora, Taswira ya Nchi Duniani n.k.
Kuna mjinga moja bila aibu aliutangazia ulimwengu kuwa ati watanzania sisi tunatamani kuona Chato ina kuwa kama Singapore!!! Kweli? Watu dhaifu wakimzunguka Rais ni hatari sana. Watu dhaifu nadra sana kutumia akili, mara nyingi huenenda na alama za nyakati au huangalia upepo unavuma kuelekea wapi. Hao ni watu dhaifu.