Watu 'Powerful' 12 ni akina nani hadi waachiwe kuharibu Bonde la Ihefu?

Watu 'Powerful' 12 ni akina nani hadi waachiwe kuharibu Bonde la Ihefu?

Picha-na.-1-1-1024x661.jpg


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (aliyesimama), akizungumza na baadhi ya wakulima na wafugaji wanaofanya shughuli zao kwenye Ranchi ya Usangu iliyopo Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya, pamoja na baadhi ya wawekezaji waliopatiwa vitalu katika ranchi hiyo wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel na kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune.
Picha-na.-3AAA-1024x576.jpg


Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) Bw. Masele Mipawa akitoa taarifa ya madeni ya wawekezaji waliopatiwa vitalu kwenye ranchi za taifa zilizopo maeneo mbalimbali nchini wakati wa kikao cha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki na baadhi ya wakulima na wafugaji wanaofanya shughuli zao kwenye Ranchi ya Usangu iliyopo Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya, pamoja na baadhi ya wawekezaji waliopatiwa vitalu katika ranchi hiyo. Bw. Mipawa amesema NARCO inawadai wawekezaji zaidi ya Shilingi Bilioni Sita
 
Shithole country! Nchi hii ina mtu anayeitwa rais, lakini kuna watu wana nchi ndani ya nchi. Ni marais ndani ya nchi. Naye Rais wa nchi anaamini wanastahili kufanya hayo! Mbaya zaidi wana tabia ya urafiki ndani ya uongozi.
 
12 January 2021

Changamoto zilizopo kwenye Ranchi ya Usangu


1671457262247.png

…………………………………………………………………………………

Na. Edward Kondela

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki ametoa siku kumi kwa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kubaini na kuwanyang’anya maeneo, wawekezaji waliopatiwa vitalu katika ranchi za taifa ambao wamebadili matumizi ya ardhi kinyume na makubaliano ya mikataba yao.



Waziri Ndaki amebainisha hayo jana (12.01.2021) wakati alipotembelea Ranchi ya Usangu wakulima ambao wanaweza kulima malisho ya mifugo ili kuondokana na migogoro ya wakulima kupata maeneo kwa ajili ya kilimo ili kujikwamua kiuchumi.



Amesema ni muda muafaka kwa wizara kuangalia namna wananchi wanavyoweza kutumia maeneo hayo kwa ajili ya tija kwa taifa badala ya kusubiri wawekezaji ambao baadhi yao wamekuwa wakienda kinyume na makubaliano ya mikataba na kuwafanya wananchi wanaoishi karibu na ranchi za taifa kukosa maeneo kwa ajili ya kufanya shughuli zao za kiuchumi.



Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema atahakikisha anasimamia maelekeo yote yaliyotolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki likiwemo la wawekezaji kulipa madeni ya vitalu walivyokodishwa ili Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) inayomiliki maeneo hayo iweze kujiendesha kibiashara kama moja ya malengo ya kampuni hiyo kupitia maeneo yake.



Katika mkutano huo Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki na baadhi ya wakulima, wafugaji na wawekezaji wanaofanya shughuli zao kwenye Ranchi ya Usangu iliyopo Wilaya ya Mbarali, Bibi Uliya Mahenge amemuomba Waziri Ndaki kuwapatia wakulima maeneo kwenye ranchi za taifa ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo huku wakilipa kodi ya serikali ya maeneo hayo watakayokidishwa kama ambavyo wafugaji wanavyopatiwa vitalu kwa ajili ya kufugia mifugo kwenye ranchi hizo.



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amemaliza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Mbeya ambapo katika ziara hiyo alikuwa na lengo la kufahamu changamoto zilizopo kwenye Ranchi ya Usangu ambayo ni moja ya ranchi zinazomilikiwa na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) ambayo ipo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
 
Back
Top Bottom