21 November 2022
MFEREJI ULIOJENGWA UKUTA MKUBWA KUZUIA MAJI KUINGIA MTO RUAHA MKUU WAANZA KUBOMOLEWA -
Ni utekelezaji wa maagizo 10 ya Makamu wa Rais kuhakikisha mabanio yote haramu ya maji yanabomolewa - Inakadiriwa umegharimu zaidi ya Milioni 400.
- Kazi zaidi inahitajika kufanyika kubomoa kingo nyingine Siku chache baada ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kuzielekeza Mamlaka zinazosimamia mto Ruaha Mkuu kuhakikisha vizuizi vyote vinaondolewa Ili kuuruhusu mto huo kutiririsha maji kama kawada.
Moja kati ya kizuizi kikuu Cha mto Ruaha kupata maji kimeanza kuondolewa Hapa ni Kata ya Imalio Usongwe katika mfereji wa nguvu kazi Mwanavala unaopeleka maji katika mashamba ya mnazi katika eneo la Warumba yanayotakiwa kuingia katika Mto Ruaha Mkuu na kuelekea hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Bwawa la Mtera, Kidatu, Bwawa la Nyerere na hatimaye Bahari ya Hindi.
Zoezi la kubomoa mabanio haya yasiyorasmi yanayotumika kuchepusha kinyume na sheria kutoka katika Mto Mfereji huu unakadiriwa kuwa umejengwa kwa zaidi ya Milion 400 miaka kadhaa nyuma.
Jitihada za kuuokoa mto Ruaha Mkuu kuufanya uwe unatiririsha maji mwaka mzima Zinaendelea na Mto Ruaha kuacha kukauka mwaka mzima INAWEZEKANA.
Ukiokoa mtiririko wa Maji mto Ruaha Mkuu maana yake umeoko na kuilinda Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Maana yake pia umalihakikishia Taifa Upatikanaji wa umeme katika Bwawa la Mtera, Kidatu na Nyerere linaloelekea kukamilika.
Source : JAMVI online TV