Watu 'Powerful' 12 ni akina nani hadi waachiwe kuharibu Bonde la Ihefu?

Watu 'Powerful' 12 ni akina nani hadi waachiwe kuharibu Bonde la Ihefu?

Ni taarifa inayoonesha kwamba hatutaendelea. Tuna kundi la watu wa hovyo, lakini wanaitwa ni powerful!
Kwa maoni yako endelea;


Je hamkuwahi kuambiwa kuna watu wakiguswa nchi itatetemeka?
 
Hakuwa na lolote yule jamaa , mdogo wa Rostam Aziz alipodakwa na Makontena ya meno ya tembo pamoja na mibunduki kadhaa ya kivita , Jiwe alikubali Rushwa ya Channel 10 ili yaishe.

Umesahau hili ?
Kwaiyo Rostam angelifungwa wewe ungenifaika nini? Sinibora alivyohongwa Chanel 10, Sasahivi inalingizia taifa mapato, juzi kuna Mchina amekamatwa ameua tembo zaidi ya 500 amehukumiwa kifungo cha miezi 6 au kulipa faini ya laki tano.
 

Acha zako hizo, waliotorosha Makinikia si walitajwa na kamati mbona hakuna aliyekamatwa? Waliobeba pesa za Tegeta Escrow nani alikamatwa? Kesi ya Tanzanite one Kuna fisadi Gani wa CCM alikamatwa?

CCM wanalindana miaka yote kama isingekua hivyo Ile ripoti ya Bashiru ingesomwa hadharani na JPM mbona aliufyata??
Nyinyi ndio mlianza kupiga kelele kuwa Magufuli alikuwa anachuki na matajiri,hadi akina Lugemalira na Set walipokamatwa na kutiwa ndani kelele zilikuwa nyingi kuwa walionewa,nenda kaulize Samia watu Mia nne aliowachia baada ya kifo cha Magufuli ni akina nani kama,Sio hao akina Kitila waliokuwa wakiiba fedha za Serikali kupitia ofisi zao za mfukoni.
 
Ashukuriwe Rais Samia kwa kurejesha Uhuru wa maoni mpaka watu wanafunguka bila hofu..
Uhuru wa maoni ulikuwa enzi za Kikwete ila Kikwete akaishia kuwa rais dhaifu, uhuru wa maoni umerudi tena sasa sijui Samia naye atakuwa rais dhaifu pia au atakuwa anachukua maamuzi magumu pale anapotakiwa kufanya hivyo ili asiwe dhaifu?
 
Hili lilimshinda vipi? Kwa Nini Hawa hakuwagusa?

Yule mtu wenu alikuwa Ni mjinga tuu aliyefanya visasi na sio Mambo ya Msingi Kama haya..

Mbinga ya Masai ilikuwa inaharibiwa na mifugo anashangaa tuu.
Hilo neno "mjinga" mbona unalirudia sana mkuu?
 
JPM ndiye aliamua Nchambi alipe hiyo faini ndogo?!
Whatever the case hoja hapa ni kwamba untouchables walikuwepo hata kipindi Cha JPM. Huyo Mwanyika si JPM alisema kasababisha Tumeibiwa Makinikia ya matrillion ila faini less than 1 Billion!!

So CCM ni wale wale tu JPM wasn't anything special otherwise wezi wote wa Escrow na EGMA wangekua jela.
 
Nyinyi ndio mlianza kupiga kelele kuwa Magufuli alikuwa anachuki na matajiri,hadi akina Lugemalira na Set walipokamatwa na kutiwa ndani kelele zilikuwa nyingi kuwa walionewa,nenda kaulize Samia watu Mia nne aliowachia baada ya kifo cha Magufuli ni akina nani kama,Sio hao akina Kitila waliokuwa wakiiba fedha za Serikali kupitia ofisi zao za mfukoni.
Sasa JPM alimfunga nani Kila mtu pesa ilikua inaongea? Nchambi na Mwanyika walikua na kesi za mabilion ila wakalipa fine chini ya 1% walioiba!! utadhani madhara yaliyoletwa na ufisadi yanakua solved kwa pesa pekee.

Huyo Mwanyika kutoka kuitwa msaliti Hadi kupewa ubunge na JPM Tena alimfanyia kampeni kabisa.

Untouchables walikuwepo miaka yote hata JPM aliwajua ila aliwalinda tusidanganyane hapa kwamba alishughulikia mafisadi kama alikua na jeuri hiyo angewashughulikia wezi wa mali za CCM.
 
Ni mawazo ya hovyo na potofu kufikiria usalama ndio muarobaini wa kila kitu.
Nimemsikiliza ndugu yangu Balile! Kwa aliyosema ni mambo mazito yanayofanya kama Taifa tujiulize mamlaka zetu hasa za usalama wanamuogopa nani kwenye ulinzi wa rasilimali zetu?

Balile binafsi nimekupa heshima ya pekee kwa hili.
 
Back
Top Bottom