Watu siku hizi Tanzania wanakufa wakiwa na sura za kung'aa, mashavu yamejaa, miili iliyonona, umri pungufu ya miaka 50; Hii sio trend ya kawaida

Mikopo Consultant

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2024
Posts
529
Reaction score
1,150
Zamani kidogo kama miaka 15 nyuma ukisikia msiba mara nyingi unakuta ni mtu pamoja na kuwa mzee wa walau zaidi ya miaka 65 ila utakuta hata ukimuangalia utaambiwa kabisa bwana huyu alikuwa mgonjwa wa ugonjwa ABCDE na hata ukimuangalia marehemu unakuta kweli kachokaa, yaani magonjwa yamempiga kweli kweli.

Sasa aisee hii miaka ya karibuni, tena karibuni zaidi, kumekuwa na trend ya vifo vingi vya watu tena wengi wao ni pungufu ya miaka 50, na ukiwaangalia unaweza kuona mtu kapost status wiki iliyopita whatsapp, meaning hakuwa kwenye hali ya ugonjwa wa kumweka kitandani. Maana yake ni vifo vya ghafla bin vuu.

Kingine pia, wanaokufa yaani hata kwa watu waliokutana nao na hata picha zao yaani hawaonekani kuwa na shida, miili imenona, mashavu yapo na nyuso zenye tabasamu.

Najua humu ni great thinkers kwamba mna uwezo wa kuangalia mambo beyond awareness.

Hii inaweza kuwa ina maana kwamba rika la kati ya miaka 30 mpaka 55 hapa Tanzania kuna wagonjwa wengi ambao ndani ya miaka 5 kutoka sasa tunaweza kuwapoteza kwa ghafula zaidi ya asilimia 30? Kama ikitokea, si itakuwa na athari kwenye labor force na economic growth? Na je family sustainability ya Tanzania itakuwa kwenye hali gani ikiwa umri wa wababa na wamama wa familia wanaangamia kwa wingi?

Aisee watu wanakufa kwa speed ya mwanga, wakitabasamu usoni, je huu ni mwanzo wa mwenendo mpya wa watu kufariki?
 
Sasa wewe ulitaka watu wafe na sura kama zimekula ndimu au quinine?
 
Mimi naona mchawi wa vifo vingi vya watu wenye miaka pungufu ya 50 ni ajali za barabarani, wanaokufa kwa magonjwa ni wachache.
51 na kuendelea ndio wengi wana case za magonjwa.
Ajali miaka ya sasa ni hatari kuliko magonjwa.
 
Hakuna mchawi zaidi ya life style. kuna mwili ulionona si dalili ya afya njema bali ni afya mbovu na muda wowote unaweza kupoteza maisha..Mwaka 2019 nilikuwa na mwili ulionona kila mtu alikiwa ananiambia nina afya njema na maisha mazuri lakini siku moja nikawa sijisiki vizuri kufika hospital dk akanimbia nina hitaji matibabu haraka coz sukari na pressure vilikuwa juu sana na ngachelewa ndio ile inakupiga heart attack..nikaanza dawa na mazoezi mengi within 2 weeks nkapona kila kitu ..now ni miaka mitano imepita nko na mwili mzuri na sina hyo magonjwa na life style yangu ni mazoezi na kungalia sana ulaji
 
Tuliambiwa Kifo ni kifo tu
Bora tupunguze mawazo
1000018341.gif
 
Zamani kidogo kama miaka 15 nyuma ukisikia msiba mara nyingi unakuta ni mtu pamoja na kuwa mzee wa walau zaidi ya miaka 65 ila utakuta hata ukimuangalia utaambiwa kabisa bwana huyu alikuwa mgonjwa wa ugonjwa ABCDE na hata ukimuangalia marehemu unakuta kweli kachokaa, yaani magonjwa yamempiga kweli kweli.

Sasa aisee hii miaka ya karibuni, tena karibuni zaidi, kumekuwa na trend ya vifo vingi vya watu tena wengi wao ni pungufu ya miaka 50, na ukiwaangalia unaweza kuona mtu kapost status wiki iliyopita whatsapp, meaning hakuwa kwenye hali ya ugonjwa wa kumweka kitandani. Maana yake ni vifo vya ghafla bin vuu.

Kingine pia, wanaokufa yaani hata kwa watu waliokutana nao na hata picha zao yaani hawaonekani kuwa na shida, miili imenona, mashavu yapo na nyuso zenye tabasamu.

Najua humu ni great thinkers kwamba mna uwezo wa kuangalia mambo beyond awareness.

Hii inaweza kuwa ina maana kwamba rika la kati ya miaka 30 mpaka 55 hapa Tanzania kuna wagonjwa wengi ambao ndani ya miaka 5 kutoka sasa tunaweza kuwapoteza kwa ghafula zaidi ya asilimia 30? Kama ikitokea, si itakuwa na athari kwenye labor force na economic growth? Na je family sustainability ya Tanzania itakuwa kwenye hali gani ikiwa umri wa wababa na wamama wa familia wanaangamia kwa wingi?

Aisee watu wanakufa kwa speed ya mwanga, wakitabasamu usoni, je huu ni mwanzo wa mwenendo mpya wa watu kufariki?
Sio kweli
 
Oya vijana ukimwi upo, Kuna siku nili kuwa hospital ila Kuli kuwa na ka semina.

Vijana tukawa tuna ambiwa tupime ukimwi, kwakuwa najuana na dokta fulani aka nikomalie nipime.

wakati wa majibu, aisee pisi zaidi ya 3 zili toka zina Lia. Mmoja ali zimia kudadadeki.
 
Back
Top Bottom