Watu siku hizi Tanzania wanakufa wakiwa na sura za kung'aa, mashavu yamejaa, miili iliyonona, umri pungufu ya miaka 50; Hii sio trend ya kawaida

Dawa za ARV zitaangamiza wengi, unaona mdada ni mrembo au mkaka na ana afya nzuri kumbe kaunganishwa kwenye gridi ya umeme. Ukigusa umeenda na maji
Hilo sio kweli, tatizo kubwa ni magonjwa yasiyoambukiza ndio yanaotuua vibaya kutokana na life style na vyakula ambayo ni adui wa miili yetu
ZAmani watu tulikuwa tunatembea kila siku, ila siki hizi kila mtu ana gari , kama hana atatumia boda na daladala huyo maana yake ni anajaza sumu mwilini ,hicho chakula unachokula kinageuka sukari na kuweka sumu na mafuta mwilini
Utakufa kwa sukari, cancer, figo au pressure hilo tatizo ni kubwa kuliko unavyodhania ,utadondoka na kufa huku ukiwa na afya yako
 
ARV ni kama methali....
Uzuri wa mkakasi ndani kipande Cha mti! 🥴
Enzi hizo kuna wimbo fulani niliwahi kuusikia, “Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti”

Walikuwa wakiaminishwa na kupatiwa tahadhari kuwa urembo wa mwanamke unaweza usiakisi yaliyomo ndani.

🎶🎶
Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti,
Matiti ya kuchongoka,
Kiuno cha mdundiko,
Waliopaka wanja, na rangi kwenye kucha,
Hao tuwaepuke, wamejaa UKIMWI.
 
Kweli aisee mwezi wa 12 tulizika mtoto wa mjomba mdada(35yrs) yaani huyu alidondoka tu akafariki hapohapo, mwezi huohuo tena kabla ya x-mass kuna janja (22yrs) mgomba wa jirani yeye alivyolala ndio hakuamka tena asubuhi anaamshwa kimya hadi tukavunja mlango kumbe tayari wa juzi.

Yaani sasahivi kidogo wazee ndio tunawauguza ila range ya (20-40yrs) wanakufa ghafla sana.
 
Inaogopesha aisee
 
Si kweli. Kwani wote wanaokufa wanang'ara sura kama unavyosema? Nenda vijijini uone wanaokufa katika umri huo mwanangu.
 
Sote njia yetu Moja ila kiukweli ukimwi ni tisho ambalo linachukuliwa poa. Aisee watu wameathirika bana sio mchezo🤔
 
Sahihi, waswahili wanafikiri mashavu kunona sana na kitambi ni afya nzuri wakati ni kinyume chake.
 
Pombe Kali na ma chorestrlo
Kiufupi ni pressure na sukari
 
Fiksi hii
 
Pombe Kali energy...sukari na wanga inanenepesha sana na kuua watu sana plus spirts za pombe...unakunywa heness unajifanya unazo kumbe imetengenezwa hapo mabibo...bado Kuna majoboz mabrand kibao usalama upo wapi plus mafegi kilanaina ....
 
📌DALII KIMOKO! NI MWENDO WA KIMYAKIMYA.

📌MBAAZI HIZO LAZIMA UNONO.

📌UNAKULA MBAAZI ALAFU BADO UNABWIA MAPOMBE, HUPUMZISHI MWILI,HULI MLO KAMILI,HUACHI NGONO ZEMBE LAZIMA USEPE MAPEMA!!!

📌HAKUNA MAAJABU TAKWIMU ZINAONYESHA GITAA LA DALI KIMOKO LIKO🔥🔥🔥

📌AJALI ZA BARABARANI ZIMEONGEZEKA. HILI NALO LINAFUKUZIANA NA DALI KIMOKO!

📌LIFESTYLE ( PRESSURE NA KISUKARI) HII INASHIKA NAMBA TATU.

#TII SHERIA BILA SHURUTI!!!
 
Ukiangalia mtaani kwako tu utaona wazee sio wengi basi vijana tujue ya kwamba wengi wetu tunakufa hpa katika ujana

Wazee kwa vijana tufanye yale yampendezayo Muumba na tuwe mbali na makatazo yake

Kifo hakina umri wala saa
Huenda wapo members wengi humu jukwaani washafarikk ila hakuna wa kuthibitisha hilo kama hamjuani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…