Watu wa kanda ya ziwa hawana uelewa wa kuwepo kwa makabila mengine nchini

Watu wa kanda ya ziwa hawana uelewa wa kuwepo kwa makabila mengine nchini

Niko kanda ya ziwa,

Nimeshangazwa na kitu kimoja

Watu huku hawajui kama kuna makabila mengine ukiacha yale yanayopotikana kanda yao

Ukisema wewe ni mgogo utaulizwa wagogo kwao ni wapi?makabila makubwa kama wasambaa,wahehe,wangoni,walugulu hawajulikani huku.

Watu hawajuihata Tanga iko wapi kijiografia.

Hapa naongelea watu wazima na wengine wamesoma mpaka vyuo vya kati.sio watoto au layman

Tembea uone

Nadhani ukubwa wa kabila la wasukuma unachangia maana utoke Geita uende Mwanza,Katavi,Shinyanga,Tabora,Simiyu watu wanaongea lugha moja tu,
Yani kumuuliza mtu mmja Dar ni wap ashindwe kukujibu ndo useme watu wa kanda ya ziwa hawajui fulani na fulani wanatokea wapi watu wengine jamani
 
Karagwe huko ni kwa kina Nshomile, sio usukumani
Kwa hiyo we ukisikia janda ya ziwa unajua ni kwa wasukuma tu,kuna waangaza,wasubi,washubi,wakilongo,wanyambo,wazinza,wakara,wakerewe,wazanaki ,wasumbwa,wakireme, nk makabila zaidi ya 30
 
Kwa mfumo mzuri wa demokrasia Wasukuma ndio waongoze Tz. Wengi wape!
 
Wewe ndio sio muelewa. Kila mkoa hapa Tanzania huwezi kukosa watu ambao hawajui makabila au maeneo ya sehemu nyingine ya Tanzania. Hii inatokana na hao watu kutosoma na pia kukosa kusafiri safiri.
Sahihi
 
Niko kanda ya ziwa,

Nimeshangazwa na kitu kimoja

Watu huku hawajui kama kuna makabila mengine ukiacha yale yanayopotikana kanda yao

Ukisema wewe ni mgogo utaulizwa wagogo kwao ni wapi?makabila makubwa kama wasambaa,wahehe,wangoni,walugulu hawajulikani huku.

Watu hawajuihata Tanga iko wapi kijiografia.

Hapa naongelea watu wazima na wengine wamesoma mpaka vyuo vya kati.sio watoto au layman

Tembea uone

Nadhani ukubwa wa kabila la wasukuma unachangia maana utoke Geita uende Mwanza,Katavi,Shinyanga,Tabora,Simiyu watu wanaongea lugha moja tu,
Hata wewe ukiambiwa kuwa kuna kabila la WAKWAYA, WAARUSHA, WASWAHILI, WAMACHINGA, n.k. unaweza ukashangaa.

Tanzania ina utajiri mkubwa sana wa makabila, zaidi ya 120.

Inawezekana hata Wazanaki na Wakwere yasingejulikana kama yasingetoa viongozi wa Kitaifa.
 
Nikwel mie nimezaa huko magu yan niwambia mi nimwenyeji watanga nanimzigua wametoka patupu wao wanajua nchi niusukuma tu hawajui kuhusu makabila mengine ila shida nikua sukumaland nikubwa unakuta mtu katoka magu kaenda katoro nimbal ila bado nikisukuma tu
 
Back
Top Bottom