Watu wa Musoma tukumbushane stori za Musoma kuanzia 2000-2010

Watu wa Musoma tukumbushane stori za Musoma kuanzia 2000-2010

Tarime mhh!! Hapana
Mbona Tarime kuna amani na pako poa tu, angalia hiyo bili iliandikwa na muhudumu kwa mteja hapo Tarime (kwa hisani ya FB).
Uyo inaoneka alileta ujuaji musoma wakamfanya kitu mbaya
Tatizo la watu wa Musoma ugomvi wao hauishi. Hata ukifanikiwa kumpiga sio mwisho wa vita, lazima atalipa kisasi kwa namna yoyote haswa wakurya wa Tarime na Serengeti. Unaeza kusahau kuwa ugomvi umeisha ukapigwa ambush ya hatari.
 

Attachments

  • 1605983157556.png
    1605983157556.png
    54.4 KB · Views: 9
Dah umenikumbusha musoma tech pale baruti kuna jamaa alikua anaonyesha movie kwenye kibanda umiza,jpili na jmosi zilikua zile xxx tukawa tunaita kikao ili kuweka tafsida,yani kuna mshikaji ilikua ikifika kumi na mbil jioni keshawahi kwenye kikao,daah noma sana enzi hizo
Brai
 
Mgasa, Kinche, Bonny Weed, Ally Bega, Duchu, Maromaro (R.I.P). List ni ndefu sana kwa wanangu wa Jamaica Mockers.

Mbio za vijiti unakutana na akina Jigga, Jira, Chui, Mapacha (jamaica pia walikua na mapacha).

Huku West Lawama unakutana na wakongwe akina Majani.

Yale maisha yamefanya tukawa tough sana. Kusurvive katikati ya gangs kama zile inahitaji roho ngumu. Bahati nzuri nilikua muhuni mpenda shule, hiyo ndio ponapona yangu. Othrerwise ningekua either jela au kaburini.
Uwakumbuke pia kina Kejile na musaKankani, na Mnyama Kwinki!
 
Washamba tu hakuna hata sehemu moja yenye wajanja hyo wilaya mitaa yote kamnyonge,mwisenge,Nyamatare,nyasho,Biafra,iringo,mkendo, pote sijaona wajanja vijana wa hapo musoma wengi wao ni watoto wa mama jitu linalelewa home miaka nenda rudi,hamjitumi kutafta Mali vijana wajanja na wenye hela musoma wanaikimbia akina magori zembwera washasepa hapo mji unaongoza Kwa wivu majungu na ushirikina.

Ukienda maofisini kule Manispaa wamelundikana wakwaya na wajita wamebadili ofisi za umma kuwa Mali zao binafsi.

Haya makabila ndiyo yenye vijana wengi wakorofi hapo mjini ,naijua musoma vizur Sana enzi za westlawama ,Jamaica mocas ,wanaume nenge enzi Hizo kulikuwa na majamaa vichwa Sana kwenye hayo makundi wengine sasa hivi ni marehemu wengine ni walemavu walikutana na mkono wa wananchi wakanyooshwa.

Enzi Hizo shule ya Day secondary hapo musoma ilikuwa moja Tu Musoma Day now inaitwa morembe ya serikali nadhani afu na mwemben ya private ikaanza zingne kama mara sec na musoma tec zilikuwa bodi pamoja na songe sec ikiwa mchanganyiko kabla ya kufanywa girls na kubinafsishwa serikalini baada ya fujo kubwa iliyosababishwa na disco Kati ya songe sec na musoma teck na kupelekea kifo cha mwanafunz mmoja na majeruhi wa kutosha.

Anyway wasalimie Sana Musoma mji wa wanafiki wivu na majungu matajiri wa hapo musoma ni wawili Tu miaka nenda rudi Mthayo mmbunge na Shemeji yake Zembwera ndo wanamiliki biashara kubwa hapo town .

Anakuja mtu anasema musoma inakuwa Kwa kasi shem on you motherfuk....
Inawezekana wewe ndo unaleta majungu na hujakaa mji huo vya kutosha. Tunaoifahamu Musoma tangu miaka ya 1980 tunakuona unapika majungu mkuu. Changamoto ya mji kutetereka ni baada ya biashara ya minofu ya samaki kupeleka Ulaya ilipodorora na viwanda vichache vilivyokuwepo kufa na kuzikwa kabisa. Tuliojihusisha kidogo na biashara ya samaki tunaikumbuka sana Musoma na watu wake si wavivu kama unavyotaka tuamini.
 
Huyu mzee Barongo ni marehemu,alikuwa muhaya lakini pia alikuwa ndiye afisa utamaduni wa wilaya.
Akipiga pank lake kichwani, mtu nadhifu, amenyoosha suruali yake kisawasawa na urefu na uhandsome ule dah Musoma ilikuwa inatisha.

Wapi kina nyakitopela?...Mapinduzi Muhere na wanyama wengine? Hahahahaaa home sweet home
 
Sehemu bora kabisa musoma kuwahi kutokea ilikuwa diocese ya musoma( kituo cha matumaini ya vijana).

Kilikuwa kituo bora cha michezo na masomo, vyote vilitolewa bure kabisa kilikuwa kisima cha maarifa, kituo hiki cha kanisa romani cathoric baada tu ya kufungwa ndipo yalipoanza kuibuka makundi ya uharifu na wahuni

Pale ilikuwepo michezo ya aina zote unayoifahamu wewe, maktaba na madarasa ya kufundishia fani mbalimbali ikiwemo uchoraji n.k

Vijana na watu wote walikuwa wanakutana pale kushiriki michezo na masomo hivyo hapakuwa na makundi ya kihuni, zilikuwepo timu za mipira na michezo mingine pamoja na wasomi.

Sijaona kikiongelewa humu mkumbuke na mazuri, msikumbushane matukio ya wahuni tu.
Mkuu umeongea jambo la maana sana!

Pale ndipo wengi tumejifunza Basketball, Vollball na michezo mingi tu achilia mbali maktaba pale.

Hii ndio wengine imetupandisha ndege kwa mara ya kwanza na kutupa maisha tuliyonayo leo!

Musoma!....Dah
 
kati ya musoma na mara wapi kuna wajaluo wengi
Mara ni mkoa na musoma mjini ni wilaya ambayo ndiko yaliko makao makuu ya mkoa wa Mara. Wajaluo wengi wako sehemu kubwa ya wilaya ya Rorya, ingawa pia kuna waruri, wasimbiti, wasuba n.k
 
Musoma n wilaya, Mara ni mkoa.
Mkoa wa Mara kuna wilaya ya Butiama,Musoma, Tarime, Rorya, Mgumu na Bunda

Musoma wanapatikana wajita na wakwaya ( awa ukweli ni kua wanapenda umbea, majivuno, roho mbaya na ushirikina .

Butiama wanapatikana wazanaki ( kwa mwalimu hapa na mbunge wao alikua Nimlodi mkono

Tarime wanapatikana Wakurya wazee wa mahasira na mapanga, wajasiri asilimia 90 miaka ya 90 mpk 2000 walikua wanaenda sana jeshini kwasababu ya ushupavu wao.

Rorya hapa wanapatikana wajaruo na wakurya kwa asilimia fulani, wajaluo asili yao ni kenya hapa ndio utaona mila za mtu akifariki linapigwa disco na pombe, pia wako vzr kwenye maswala ya ulozi hawa

Mgumu hapa ni mchanganyiko mana ni njianya kuelekea serengeti ila jamii kubwa hapa ni waikizu na wakurya baadhi na makabila madogo madogo.

Bunda hapa napo ni mchanganyiko kuna watu wanatoka kibala ambao ni wakerewe, pia kuna wasukuma toka Mwanza, wajita pia wapo
Masahihisho, Mugumu si wilaya, wilaya ni Serengeti nadhani. Pia umesahau wilaya ya Musoma vijijini na Butiama. Jumla kuna wilaya 7
 
Umenikumbusha mbali sana mzee chibaland na mama tosapela
Enzi izo pale songe sekondari ndo ilikua shule ya wakorofi kuna jamaa alikua anaitwa DIBO alikua anatusumbua sana
Na ndg yake Mnema!
 
Musoma home sweet home sehemu moja safi sana, nime enjoy kuishi sehemu hii, Iringo ndio maeneo ya kujidai kule custom tunawaka sana , vitu vinachukuliwa mwigobero pale mapoti washafanya ambush sana tukiwa tunawaka mara kibao tushakimbilia ziwani ili usidakwe maana mapoti hawaingii ziwani wanaogopa kulowanisha jezi!! nyie mnakimbia ila kuna raia na heshima zao wao wanawaka na hawakimbii mapoti afu fresh, ila wewe choka mbaya msingi mbio vinginevyo utasepa na rondo

mtaa wa uhuru pale sana tu kush kama zote, ikifika jioni uwanja wa mkendo wakush wanapata vitu vyao taratibu bila wasi huku tunacheki mpira

Nyasho kona kuna chimbo moja hivi kwenye miwa dah maisha ya kush yamefanya nijuane na wahuni wengi kichizi hata tukikutana maeneo sijawahi kabwa wala nini kisa tu tushakutana nao kwa sadali!!!

Masstown ni habari nyingine vurugu ni nyingi, nyembe na mapanga nje nje lakini bado life lilikuwa poa sana, sababu sio kila sehemu ilikuwa na utata

wasanii sijui fataki, lazzbaby, best nasso na wengineo aisee respect sana
 
Masahihisho, Mugumu si wilaya, wilaya ni Serengeti nadhani. Pia umesahau wilaya ya Musoma vijijini na Butiama. Jumla kuna wilaya 7
Hakuna wilaya ya musoma vijijini! Wilaya ni moja Musoma...so kuna wilaya 6
 
Back
Top Bottom