Watu wa Musoma tukumbushane stori za Musoma kuanzia 2000-2010

Tarime mhh!! Hapana
Mbona Tarime kuna amani na pako poa tu, angalia hiyo bili iliandikwa na muhudumu kwa mteja hapo Tarime (kwa hisani ya FB).
Uyo inaoneka alileta ujuaji musoma wakamfanya kitu mbaya
Tatizo la watu wa Musoma ugomvi wao hauishi. Hata ukifanikiwa kumpiga sio mwisho wa vita, lazima atalipa kisasi kwa namna yoyote haswa wakurya wa Tarime na Serengeti. Unaeza kusahau kuwa ugomvi umeisha ukapigwa ambush ya hatari.
 

Attachments

  • 1605983157556.png
    54.4 KB · Views: 9
Brai
 
Uwakumbuke pia kina Kejile na musaKankani, na Mnyama Kwinki!
 
Inawezekana wewe ndo unaleta majungu na hujakaa mji huo vya kutosha. Tunaoifahamu Musoma tangu miaka ya 1980 tunakuona unapika majungu mkuu. Changamoto ya mji kutetereka ni baada ya biashara ya minofu ya samaki kupeleka Ulaya ilipodorora na viwanda vichache vilivyokuwepo kufa na kuzikwa kabisa. Tuliojihusisha kidogo na biashara ya samaki tunaikumbuka sana Musoma na watu wake si wavivu kama unavyotaka tuamini.
 
Huyu mzee Barongo ni marehemu,alikuwa muhaya lakini pia alikuwa ndiye afisa utamaduni wa wilaya.
Akipiga pank lake kichwani, mtu nadhifu, amenyoosha suruali yake kisawasawa na urefu na uhandsome ule dah Musoma ilikuwa inatisha.

Wapi kina nyakitopela?...Mapinduzi Muhere na wanyama wengine? Hahahahaaa home sweet home
 
Mkuu umeongea jambo la maana sana!

Pale ndipo wengi tumejifunza Basketball, Vollball na michezo mingi tu achilia mbali maktaba pale.

Hii ndio wengine imetupandisha ndege kwa mara ya kwanza na kutupa maisha tuliyonayo leo!

Musoma!....Dah
 
kati ya musoma na mara wapi kuna wajaluo wengi
Mara ni mkoa na musoma mjini ni wilaya ambayo ndiko yaliko makao makuu ya mkoa wa Mara. Wajaluo wengi wako sehemu kubwa ya wilaya ya Rorya, ingawa pia kuna waruri, wasimbiti, wasuba n.k
 
Masahihisho, Mugumu si wilaya, wilaya ni Serengeti nadhani. Pia umesahau wilaya ya Musoma vijijini na Butiama. Jumla kuna wilaya 7
 
Umenikumbusha mbali sana mzee chibaland na mama tosapela
Enzi izo pale songe sekondari ndo ilikua shule ya wakorofi kuna jamaa alikua anaitwa DIBO alikua anatusumbua sana
Na ndg yake Mnema!
 
Musoma home sweet home sehemu moja safi sana, nime enjoy kuishi sehemu hii, Iringo ndio maeneo ya kujidai kule custom tunawaka sana , vitu vinachukuliwa mwigobero pale mapoti washafanya ambush sana tukiwa tunawaka mara kibao tushakimbilia ziwani ili usidakwe maana mapoti hawaingii ziwani wanaogopa kulowanisha jezi!! nyie mnakimbia ila kuna raia na heshima zao wao wanawaka na hawakimbii mapoti afu fresh, ila wewe choka mbaya msingi mbio vinginevyo utasepa na rondo

mtaa wa uhuru pale sana tu kush kama zote, ikifika jioni uwanja wa mkendo wakush wanapata vitu vyao taratibu bila wasi huku tunacheki mpira

Nyasho kona kuna chimbo moja hivi kwenye miwa dah maisha ya kush yamefanya nijuane na wahuni wengi kichizi hata tukikutana maeneo sijawahi kabwa wala nini kisa tu tushakutana nao kwa sadali!!!

Masstown ni habari nyingine vurugu ni nyingi, nyembe na mapanga nje nje lakini bado life lilikuwa poa sana, sababu sio kila sehemu ilikuwa na utata

wasanii sijui fataki, lazzbaby, best nasso na wengineo aisee respect sana
 
Masahihisho, Mugumu si wilaya, wilaya ni Serengeti nadhani. Pia umesahau wilaya ya Musoma vijijini na Butiama. Jumla kuna wilaya 7
Hakuna wilaya ya musoma vijijini! Wilaya ni moja Musoma...so kuna wilaya 6
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…