Watu wa Musoma tukumbushane stori za Musoma kuanzia 2000-2010

Hakuwa tajiri bali alikuwa mwenyekiti wa ccm! Alikuwa kimbau mbau fulani hivi.Umaarufu wake ulichagizwa na vibao kubandikwa mlangoni kuonyesha 'YUKO MKUTANONI,YUKO SAFARI,KALALA,BAFUNI,N.K" Bila kusahau kiswahili chake!
Na kanifundisha Kamunyonge Primary enzi hizoo, za kina Mabuba, Ally, Kuyenga, n.k

Pia Kijana wake alikuwa mwalimu hapo Kamunyonge, na watoto wake wamesoma hapo.

Kwetu jirani na kwake.
 
Kuna pantoni toka mjini, japo na hizo mitumbwi zipo
Inaanzia Mwigobelo? mbona huw anaona kama yale ni makarua tu? mnachukua muda gani hadi kinesi? Mtu akizunguka kwa barabara yupi anawahi kufika.
 
Inaanzia Mwigobelo? mbona huw anaona kama yale ni makarua tu? mnachukua muda gani hadi kinesi? Mtu akizunguka kwa barabara yupi anawahi kufika.
Yap inaanzi mwigobelo. Kuvuka ni km daki 20 mpk nusu saa. Kwa barabara sijawahi kupita.
Pantoni inakuwepo pale mara mbili kwa siku.
 
Kuna kijiji kule nimekisahau kina shule ya msingi. Unavuka kwa mtumbwi au boti unafika sehem unapita kwenye mkondo wa mto Mara basi unakutanana na mawimbi sio ya kawaida. Sema unafurahi kuina jinsi maji ya mto yasivyojichanganya na ya ziwa.
 
Ba
Yap inaanzi mwigobelo. Kuvuka ni km daki 20 mpk nusu saa. Kwa barabara sijawahi kupita.
Pantoni inakuwepo pale mara mbili kwa siku.
si kwa Pantoni unatumia muda mfupi sana, asante kwa taarifa mkuu.
buturi jiran na kirumi
Napafahamu sana, miaka ile kabla lami ya kutoka makutano hadi Tarime haijajengwa, tulikuwa tunapita hiyo njia kwenda Tarime toka Mwanza, baada ya kirumi unapita huko buturi, Ochuna, unaenda hadi Kowaki unaibukia Utegi then unaitafuta Tarime.
 
Daraja la Kirumi, jinsi linavyonesa ukipita. Nilii enjoy sana kuishi Musoma
 
Ba
Yap inaanzi mwigobelo. Kuvuka ni km daki 20 mpk nusu saa. Kwa barabara sijawahi kupita.
Pantoni inakuwepo pale mara mbili kwa siku.
Kwa Pantoni unatumia muda mfupi sana, asante kwa taarifa mkuu.
 
kwa marwa jenelo unapafahamu
 
Musoma tunaita Magido, Mapanki watu wa Mwanza ndiyo wanaita hivyo kipindi hicho pale walipojenga shule ya Baruti secondary ndipo kilikuwa kiwanda cha kukaangia
[emoji3][emoji3][emoji3]Eti magido umenikumbusha mbali.
 
Kayabo ndio wale samaki wakavu waliopasuliwa au nimesahau!
ndio alafu wanaanikwa na juani ukiwapika hao harufu yake cyo ya kitoto mtaa mzima watajua kuwa umewapika ila ni watamu wakipata mpishi bora.
 
ndio alafu wanaanikwa na juani ukiwapika hao harufu yake cyo ya kitoto mtaa mzima watajua kuwa umewapika ila ni watamu wakipata mpishi bora.
Halafu ukipata na ugali wa udaga inakuwa safi kabisa.
 
Kayabo ndio wale samaki wakavu waliopasuliwa au nimesahau!
Magido ni sangara walioondolewa minofu.
Mapanki ni sato walioondolewa minofu.
Kayabo ni samaki wadogowadogo hasa sangara waliokaushwa tu na jua bila kupasuliwa.Hawa katika hatuq ya kuwakausha huwa wanatoa harufu hatari.Mara nyingi tulikuwa tunawaanika kwenye mapaa ya nyumba harufu mtaa mzima.

Waliopasuliwa ni vibambara tena hubanikwa.
Asante

Sent using Linux 10.29
 
Musoma Kuna shule moja ya msingi inaitwa Kambarage, nilirud msm juz Kati baada ya muda mrefu kuondoka ila mwaka wa 10 huu majengo yapo vilevile chakavu na yaliyokua hayajaisha pia yapo vilevile miaka yote hakuna mabadiliko labda miti tu ndo inakua... Kule ni kama mkoa ulio telekezwa ase maendeleo yako kushoto
 
Mazara namfahamu alikuwa na kigorofa chake maeneo ya Songe ziwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…